Ningelikushauri kwanza usome historia kabla ya kuropokwa hapa. Muungano wa zanzibar na wadanganyika ulifanyika baada ya sisi kumpindua sultani. Ukumbuke kuwa nyinyi mmepewa uhuru wenu kwa karatasi. Siku karatasi yenu ikiliwa na mchwa msishangae mzungu kurudi kukutawalieni tena. Sisi tumepata uhuru wetu kwa kupindua serikali!
Kuhusu kujitenga kwa nini kwanza huwaulizi viongozi wenu ni kwa nini hawataki tujitenge? Toka enzi za nyerere tumelianza hilo na mpaka leo mnakataa? Kama kweli tunawarudisha nyuma na ni mzigo kwenu kwa nini viongozi wenu bado wangangania muungano huu? Kwa nini viongozii wenu walikataa kuonyesha mkataba wa makubaliano ya muungano yaliotiwa sahihi na nyerere pamoja na karume?
Usije kunipa jawabu eti sisi ndugu, sisi tuna udugu wa kweli wa wakenya kuliko nyinyi watanganyika.
Hivi wewe kama una mke ambae hana afanyalo la kukusaidia katika maisha ye nu zaidi ya hasara na madeni kila siku, na kila kukicha anadai talaka yake, hivi kweli utabaki nae au utamfungia mabegi na kumfukuza kwako? Sasa kama kweli sisi tunawaletea hasara na kukurudisheni nyuma, kwa nini mnangangania kubaki nasi?