DOKEZO Responded Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
kwani daraja linaondoa ulazima wa bandari?

Haiondoi ulazima lakini inaweza kupunguza hitaji na kazi zake.

Katika tathmini ya traffic ya mizigo itakoyopita kwenye daraja, uwepo wa bandari yenye kufanya kazi hiyo tayari, ni factor kubwa ya kuzingatiwa.

Uwepo wa daraja utaathiri vipi bandari na uwepo wa bandari utaathiri vipi daraja ni details ambazo haziwezi kupuuzwa kuzingatiwa
 
Wakati mwingine inabidi kujiuliza kama tunajiamini tunaweza au tunasubiri wengine waamue tunaweza.. NSSF na wadau wengine kama mko serious kwa hili you have my support....

nimesikia kuhusu huo mpango katika mitandao kama ni kweli ni jambo la zuri sana.
 
Wakati mwingine inabidi kujiuliza kama tunajiamini tunaweza au tunasubiri wengine waamue tunaweza.. NSSF na wadau wengine kama mko serious kwa hili you have my support....
Tumeanza na daraja la Kigamboni kuunganisha pande mbili za jiji la Dar es Salaam. Soon tutahamia ujenzi wa daraja la Bara na Visiwani
 
Kabla hatujafikiria kuwaunganisha wabara na wazanzibari, tuwafikirie kwanza Wakerewe na Wamafya
 
Kwanini wasijenge tube iwe inapita train kama ile ya uk to france,maana daraja kwa umbali huo bahari ikichafuka mawimbi si yataleta balaa kwa watumiaji?
 
Je, Rais Magufulu kutokana na maono yake ya "Tanzania Inayoweza" anaelekea kufikiria kitu kikubwa kama hiki? Kuna watu wanaweza kuunga mkono wazo kama hili? Ni nini kitakuwa kizuizi kikubwa cha kifikra kufikiria, kupanga na kutekeleza mradi mkubwa kama huu?
 
Project hii kwa nchi kama Tanzania haiwezekani na wala haina tija. Tuendeleekutumia usafiri wa tija kama ferry, meli, boti na ndege toka Tanganyika kwenda Unguja na kurudi.

Tutazame daraja refu liliotumia miaka tisa kumalizika (2008 -2018 )

Mega project! Taking a ride on world's longest sea bridge, which, linking Hong Kong, Zhuhai and Macao, is yet to be formally opened to traffic.


Source : NewChina TV
 
Bagamoyo, usiangalie kwa miaka kumi ijayo; ni lazima uangalie miaka 100 ijayo. Na kila daraja linaweza kuangaliwa tija yake - kuanzia ujenzi n.k Lakini, pia ni muhimu kujaribu kujibu swali la kwanini tuunganishe; kutakuwa na faida gani kuunganisha kwa daraja...
 
Siku ukigombea nitakupa kula zangu na familia yangu na ndugu zangu ....nimekua nikifikilia hiki kitu ...nikaamua kusesearch uzi wa kuhusu idea ya kujenga daraja n nikauona ....big up mkuu
Kunywa Pepsi big ntalipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…