Uchaguzi 2020Zanzibar: Jeshi la Polisi lawataka wagombea kuacha kutoa matamshi ya vitisho, lasema hatua kali zitachukuliwa kuhakikisha amani ya nchi inalindwa
Kuelekea Oktoba 28, Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi-Kamisheni ya Zanzibar, CP Mohamed Haji Hassan ameonya kuhusu uvunjifu wa amani visiwani humo
Amesema, "Baadhi ya Wagombea wa Vyama vya Siasa wamesikika wakitamka maneno kama vile 'wataingia barabarani', 'watalinda kura', 'mwaka huu lazima kieleweka'. Jeshi la Polisi linaona matamshi haya ni maandalizi ya uvunjifu wa amani"
Ameongeza kuwa, kwasababu matamshi hayo yanakiuka kanuni na miongozo ya Uchaguzi Mkuuu iliyotolewa na ZEC pamoja na NEC, Jeshi kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi litachukua hatua kali kuhakikisha amani ya nchi inalindwa.
Hawa ndo wanaofanya watu washindwe kwenda kutwanga kura kwa matamko yao na makaripio ambayo dhahiri yanaonyesha wanalinda ajira zao. Kwa kweli hawa watatu wamechangia pakubwa kudumaza democracy ya nchi yetu.
Hebu thibitisha pasi na shaka kuwa neno kugawana fito lina ashiria uchochezi na kuvuruga uchaguzi au democracy ya kuchagua na kuchaguliwa.
Acheni hizo mambo. Badala ya hivyo vyombo kuhimiza watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura. Wao wamegeuka kuwa mawakala wa wanasiasa. Ni watu wa hovyo kabisa.
Police wakifanya kazi kwa kufuata sheria badala ya maagizo hakuna vurugu yeyeto itakayotokea.
Pia wasijidanganye kutumia nguvu kama njia ya kuwasilence watu wanaodai haki zao imekula kwao uzuri wamegawanyika sababu ya kutoingezwa mishahara five year mabosi zao wasijeshangaa watakavyogeukwa.
Mgombea mtawala ana nafasi kuelezea mazuri aliyoyafanya na atakayo yafanya akichaguliwa tena. Mgombea mpya anahaki kuwakumbusha wapiga kura mabaya waliofanyiwa na utawala uliopo, ahadi hewa ambazo hazikutekezwa na yapo mapya atakayo tekeleza akichaguliwa. Kumzuia ni uonevu na kuwanyima wananchi haki ya kupima.
Shida yako ni kujiimanisha kuwa mnapendwa na Wazanzibar. Jiulize kwa sera zipi??? Kwa uzoefu upi? Ilani yao ndiyo ilitolewa juzi baada ya kudesa kutoka Ilani nyingine.
Kweli walijitayarisha kugombea au ni waisndikizaji tuuu. Jamani unaanza kampeni bila ilani ambayo ndiyo mkataba mkuu wa chama na wananchi, watu wakueleweje?
Seiff ndiyo mmiliki wa chama chao ndiyo maana anaamua vitu bila kushrikisha wengine. Ndugu yangu Membe pole sana umeishamezwa. Rudi nyumbani kumenoga.
Sasa kulinda kura kosa? Kuingia barabarani kosa? Kueleweka jambo ni kosa? kama ni makosa basi kwenye katiba yapo, labda utuoneshe wapi imesema ivo? Kwanini aseme atalinda amani tu lakini asilinde haki?
Mkuu, mbona unakuwa mgumu kuelewa!? Mbona mgombea aliyesema hayo yupo wazi kabizsa kwenye maelezo yake!? Sasa asipochaguliwa atatekelezaje ilani yake ya UCHAGUZI ambayo inamuelekeza apeleke maji, barabara na maendeleo mengine!? Maana vyama vingine havina mpango wa kufanya hayo kama vitachaguliwa. Huyo, Mgombea anapenda ukweli na hataki kudhihaki watu kwa ahadi zisizo na manufaa!!!