Uchaguzi 2020 Zanzibar: Jeshi la Polisi lawataka wagombea kuacha kutoa matamshi ya vitisho, lasema hatua kali zitachukuliwa kuhakikisha amani ya nchi inalindwa

Uchaguzi 2020 Zanzibar: Jeshi la Polisi lawataka wagombea kuacha kutoa matamshi ya vitisho, lasema hatua kali zitachukuliwa kuhakikisha amani ya nchi inalindwa

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Kuelekea Oktoba 28, Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi-Kamisheni ya Zanzibar, CP Mohamed Haji Hassan ameonya kuhusu uvunjifu wa amani visiwani humo

Amesema, "Baadhi ya Wagombea wa Vyama vya Siasa wamesikika wakitamka maneno kama vile 'wataingia barabarani', 'watalinda kura', 'mwaka huu lazima kieleweka'. Jeshi la Polisi linaona matamshi haya ni maandalizi ya uvunjifu wa amani"

Ameongeza kuwa, kwasababu matamshi hayo yanakiuka kanuni na miongozo ya Uchaguzi Mkuuu iliyotolewa na ZEC pamoja na NEC, Jeshi kwa kushirikiana na Vyombo vya Ulinzi litachukua hatua kali kuhakikisha amani ya nchi inalindwa.

Msikilize hapa:

 
Hawa ndo wanaofanya watu washindwe kwenda kutwanga kura kwa matamko yao na makaripio ambayo dhahiri yanaonyesha wanalinda ajira zao. Kwa kweli hawa watatu wamechangia pakubwa kudumaza democracy ya nchi yetu.
 
Huwezi linganisha hayo maneno na yale kusema TUTAGAWANA FITO
Hebu thibitisha pasi na shaka kuwa neno kugawana fito lina ashiria uchochezi na kuvuruga uchaguzi au democracy ya kuchagua na kuchaguliwa.

Acheni hizo mambo. Badala ya hivyo vyombo kuhimiza watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura. Wao wamegeuka kuwa mawakala wa wanasiasa. Ni watu wa hovyo kabisa.
 
Kwani wanaofia nini si watulie tu waone moto [emoji23][emoji23]

SUBIRI KIDOGO
 
Naomba sana, Polisi wetu mtumie MANENO HAYA:-

HAKI, WAJIBU NA AMANI.

NENO AMANI HALISIMAMI PEKE YAKE, NI MPAKA LICHANGANYWE NA MANENO " HAKI NA WAJIBU" (UWAJIBIKAJI)
 
Police wakifanya kazi kwa kufuata sheria badala ya maagizo hakuna vurugu yeyeto itakayotokea.
Pia wasijidanganye kutumia nguvu kama njia ya kuwasilence watu wanaodai haki zao imekula kwao uzuri wamegawanyika sababu ya kutoingezwa mishahara five year mabosi zao wasijeshangaa watakavyogeukwa.
 
Hivi watanzania tutaendelea kuwa wapole mpaka lin .hili jeshi linalotumika na ccm kuharibu vifaa vya upinzani kama walivyofanya kule Mara kwa heche
 
Kuelekea Oktoba 28, Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi-Kamisheni ya Zanzibar, CP Mohamed Haji Hassan ameonya kuhusu uvunifu wa amani visiwani humo...
Mgombea mtawala ana nafasi kuelezea mazuri aliyoyafanya na atakayo yafanya akichaguliwa tena. Mgombea mpya anahaki kuwakumbusha wapiga kura mabaya waliofanyiwa na utawala uliopo, ahadi hewa ambazo hazikutekezwa na yapo mapya atakayo tekeleza akichaguliwa. Kumzuia ni uonevu na kuwanyima wananchi haki ya kupima.
 
Kuelekea Oktoba 28, Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi-Kamisheni ya Zanzibar, CP Mohamed Haji Hassan ameonya kuhusu uvunifu wa amani visiwani humo...
Nchi hii ina matatizo makubwa ya kiutawala na kimfumo kwa kiasi kikubwa sana
 
Wamesema wakiibiwa kura zao ndo wataingia barabarani kwaivyo mkitaka wasiingie barabarani msiwaibie kura zao.
Shida yako ni kujiimanisha kuwa mnapendwa na Wazanzibar. Jiulize kwa sera zipi??? Kwa uzoefu upi? Ilani yao ndiyo ilitolewa juzi baada ya kudesa kutoka Ilani nyingine.

Kweli walijitayarisha kugombea au ni waisndikizaji tuuu. Jamani unaanza kampeni bila ilani ambayo ndiyo mkataba mkuu wa chama na wananchi, watu wakueleweje?

Seiff ndiyo mmiliki wa chama chao ndiyo maana anaamua vitu bila kushrikisha wengine. Ndugu yangu Membe pole sana umeishamezwa. Rudi nyumbani kumenoga.
 
Huwezi linganisha hayo maneno na yale kusema TUTAGAWANA FITO
Sasa kulinda kura kosa? Kuingia barabarani kosa? Kueleweka jambo ni kosa? kama ni makosa basi kwenye katiba yapo, labda utuoneshe wapi imesema ivo? Kwanini aseme atalinda amani tu lakini asilinde haki?

Wazanzibari tunataka tugawane fito, Mzee Karume alitwambia Koti likikubana ulivue tu.
 
Hivi wale wanaosema hadharani msipo nichagua sitaleta maji, barabara na maendeleo mengine hivyo siyo vitisho kweli?
Mkuu, mbona unakuwa mgumu kuelewa!? Mbona mgombea aliyesema hayo yupo wazi kabizsa kwenye maelezo yake!? Sasa asipochaguliwa atatekelezaje ilani yake ya UCHAGUZI ambayo inamuelekeza apeleke maji, barabara na maendeleo mengine!? Maana vyama vingine havina mpango wa kufanya hayo kama vitachaguliwa. Huyo, Mgombea anapenda ukweli na hataki kudhihaki watu kwa ahadi zisizo na manufaa!!!
 
Back
Top Bottom