Zanzibar: Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna, yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo

Zanzibar: Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna, yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo wakishinikiza kuwa hawataki Kanisa katika eneo lao.

Hii ni kunyume kabisa na sheria za nchi zinazoruhusu Uhuru wa Kuabudu. Kama jambo halitafanyika basi ni wazi kuna kiongozi mbaguzi wa dini anaewalinda wabomoaji na pia hii itachochea sehemu nyingine makanisa na makazi ya wachungaji kubomolewa.

Pia miezi michache ijayo kipindi cha mfungo kikianza huwa ni marufuku kwa wakristo kula sehemu za wazi, ukikutwa unafungwa mpaka mfungo uishe, wengine huwa wanapigwa sana, sasa hapa ni kwamba mtu kama umeamua kufunga kwa imani yako iwaje hutaki kuona wenzako hawali, ni kwamba imani yako no nyepesi sana kuisimamia, kama ni hivyo kuna haja gani ya kufunga.

============================================

TAMKO LA SERIKALI.

Mkuu wa Wilaya wa Mjini Magharibi kisiwani Unguja, Rashid Msaraka amezungumza na waandishi wa habari leo Machi 11, 2022 baada ya kufika eneo la tukio.

“Mamlaka zinazohusiana na utabiri wa hali ya hewa, zimetoa tathmini yao kuhusu mvua zinazotarajiwa kunyesha hivi karibuni, nikatoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuwa na tahadhari ya maeneo hatarishi, moja kati ya maeneo hayo ni hiyo iliyobomolewa.

“Nyumba mojawapo iliyobomolewa ni nyumba ya kawaida lakini taarifa inayosambaa ni kanisa, hapana mimi sina kibali cha kujengwa kwa kanisa.

“Hivyo, imevunjwa kwa kuwa ni sehemu ya nyumba zilizokuwa hatarishi, tunaweka mazingira sawa, siyo hapa tu bali ni maeneo yote.
 
Niliiona jana hii habari, sema Wahusika wametulia kwa sababu wanajua walichokuwa wakifanya sio sahihi

Huwezi ukaejenga makanisa na kwenye makazi ya watu na kuwapigia kelele usiku kucha kwa miujiza ya kitapeli

Zanzibar hawapendi ujinga
Yapo makanisa kama Katoliki ambayo tunaheshimu na kuishi nao kwa amani, ila haya makanisa ya kijasiriamali yaliyojaa utapeli hayawezi kuvumilika.

Hakuna uhuru wa kuabudu usio na miaka, ndio maana hata serikali ilimfungia Nabii Tito pia imefungia Zumaridi
 
KANISA LA TAG LAVUNJWA VIBAYA

Balaa linaendelea kwa spidi kali huko Zanzibar aisee, Nadhani kuna jambo linatakiwa kufanyika kwani shambulio hilo ni kunyume kabisa na sheria za nchi zinazoruhusu Uhuru wa Kuabudu. Kama jambo halitafanyika uzoefu huo unaweza kutumika kuwaonea wakristo hapo Zanzibar. Pole mchungaji na wakristo hapo Zanzibar. Amen

View attachment 2146509
Why
When
Whom
Where
How

[4Ws + 1h] Katika uandishi timiza hayo
 
KANISA LA TAG LAVUNJWA VIBAYA

Hivi majuzi Zanzibar limevunjwa kanisa vibaya sana kwa hilo gari pichani la bomoa bomoa, Nadhani kuna jambo linatakiwa kufanyika kwani shambulio hilo ni kunyume kabisa na sheria za nchi zinazoruhusu Uhuru wa Kuabudu. Kama jambo halitafanyika uzoefu huo unaweza kutumika kuwaonea wakristo hapo Zanzibar.

Pia miezi michache ijayo kipindi cha mfungo kikianza huwa ni marufuku kwa wakristo kula sehemu za wazi, ukikutwa unafungwa mpaka mfungo uishe, wengine huwa wanapigwa sana, sasa hapa ni kwamba mtu kama umeamua kufunga kwa imani yako iwaje hutaki kuona wenzako hawali, ni kwamba imani yako no nyepesi sana kuisimamia, kama ni hivyo kuna haja gani ya kufunga.

View attachment 2146523

View attachment 2146509

Nitajie kanisa lililowahi kujengwa na Yesu japo moja tu.
 
Kanisa la t.a.g pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo wakishinikiza kuwa hawataki Kanisa katika eneo lao.

Zanzibar kuna kirusi cha ubaguzi wa kidini, lakini isifike huku. hii ni kunyume kabisa na sheria za nchi zinazoruhusu Uhuru wa Kuabudu. Kama jambo halitafanyika uzoefu huo unaweza kutumika kuwaonea wakristo hapo Zanzibar.

Pia miezi michache ijayo kipindi cha mfungo kikianza huwa ni marufuku kwa wakristo kula sehemu za wazi, ukikutwa unafungwa mpaka mfungo uishe, wengine huwa wanapigwa sana, sasa hapa ni kwamba mtu kama umeamua kufunga kwa imani yako iwaje hutaki kuona wenzako hawali, ni kwamba imani yako no nyepesi sana kuisimamia, kama ni hivyo kuna haja gani ya kufunga.

View attachment 2146523

View attachment 2146509
Wananchi wamekuja na mtambo kabisa wa kuvunja? Kuna habari hapo kama hujaweka wazi mkuu.
 
Tukichekea Nyani tutavuna Mabua.... Hii nchi inabidi tufuate Sheria na kuacha kupindisha mambo

Kuna sehemu zimetengwa na inabidi ziendelee kutengwa kwa ajili ya TAASISI, haijalishi ni mambo ya Imani au sio Imani kila Mtanzania ana haki ya kuabudu na kutokuabudu...., ila pia HANA haki ya kufanya hayo popote pale..., mfano hizi sehemu za kuabudu kwenye makazi ya watu watu wanakesha....

Tuishi kwa Amani kwa kuheshimiana kwa kila mtu na Imani yake Kivyake bila kuingiliwa wala yeye kuwaingilia wengine Yaani asikerwe na yeye asiwe Kero...
 
Kwann dini ya kiislamu huwa inaogopa Sana competition ya kiimani. Je ni dhaifu dhidi ya imani zingine?
Maana ni nature imani yeyeto dhaifu huwa inamezwa na imani imara.
Mfano dini za weupe zilikuwa na nguvu zaidi hadi zikazimeza dini za asili.
 
Back
Top Bottom