Nina shamba hapo Morogoro la Karafuu. Mwaka wa jana walikuja wa indonesia (Barozi wa Indonesia Tanzania), kuingia mkataba Kijiji cha Konde Matombo Morogoro, Mkataba uliingiwa mbele ya Mkurugenzi wa Halimashauri Rehema Bwasi, Mkuu wa Wilaya(Albert Msando) na Wanasheria wa Ubarozi na Halimashauri. Wa indonesia hao pia wamewekeza Zanzibar kwahiyo wamekuja na Wazanzibar wengi. Mkataba unataja ujenzi wa kiwanda cha majani ya Karafuu kuzalisha mafuta, na Ununuzi wa Karafuu yenyewe. Utekelezaji wa mradi hauweleweki mpaka sasa. Kuna benki ilikuja kutoka Mikopo, pia nayo ikaingia mkataba na wanakijiji ikawaadaa ikaondoka. Naona hata waziri wa Zanzibar anaenda nae atawapiga kiswahili pia ataondoka. Morogoro Milima ya Uluguru (Matombo) kwa sasa wanaongoza kulima mazao ya viungo (Karafuu) kwa Tanzania, na miaka 3 ijayo itatoa karafuu mara 4 ya Zanzibar, lakini Serikali imewaacha wakulima, ambao kwa nguvu zao na kujitafuta wamebuni Njia za kulima zao hilo bila msaada wa serikali wala ushauri wao. Wanaofaidika na karafuu ya Morogoro ni Kenya, ambao utumia madalali wa kitanzania kukodisha Miti kabla haijazaa na kuwanyonya wakulima huku Serikali ikiangalia. Karafuu hiyo uenda Kenya sababu madalali wameshika soko. Nini cha kufanya. i. Kuanzisha chama cha ushirika ambacho wakulima watauza, watapata mikopo, na watapata ushauri wa kilimo, Mkurugenzi na Mkuu wa Wilaya walisema wataanzisha mbele ya mkutano wa wananchi lakini hakuna kilichoanzishwa yalikuwa maneno. ii. Wananchi wanajitaidi kulima lakini moundombinu ni duni, Barabara ya Matombo - Konde KM 4 ni mbovu na Injinia wa Halimashauri aliwaambia wananchi kwamba ataijenga lakini hakuna kinachoendelea. iii. Umeme umevutwa kijijini na transfoma zimefungwa 2 lakini huu ni mwaka wa 3 haujawashwa kwahiyo wananchi wamechoka. iv. Wananchi wameongopewa sana na wanasiasa kwa namna nyingine wamechoka. Kijiji kimoja kinatoa tani 300 za karafuu, kg 1 inauzwa 14,000/. hadi elf 22,000/. Lakini kijiji barabara mbovu, zahanati hakuna, shule msingi mbovu, sekondari hakuna na Umeme hakuna. Serikali vikumbukeni vijiji watu wanapambana lakini msaada hakuna. Vijiji vinavyolima Karafuu Milima ya Uluguru ni Konde, Lubwe, Tegetero, Kinore, Sanzani, Kitungwa, Lugogo, Kibwege, na vinginevyo.