Zanzibar kufungua shule na kurejesha shughuli za kijamii kuanzia Juni 29

Zanzibar kufungua shule na kurejesha shughuli za kijamii kuanzia Juni 29

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
DR SHEIN ARUHUSU SHUGHULI ZA KIJAMII KUENDELEA JUNI 29.

Raisi wa zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ametangaza rasmi kufunguwa skuli zote nchini pamoja na shughuli za kijamii kuanzia Juni 29 baada ya kupunguwa kwa kasi ya maradhi ya covid-19 Nchini .

Akizungumza katika hutuba ya kulivunja baraza la wawakilishi la tisa huko Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar amesema hatua hiyo inapaswa kwenda sambamba na tahadhari kubwa ya ugonjwa huo ili maradhi hayo yasirejee tena Nchini .

Dr Shein ameiyagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kuaandaa mpango utakao zingatia kukabiliana na wimbi kubwa la Wanafunzi pamoja na vifaa vya skuli ili kuepusha kuenea kwa kasi kwa maradhi hayo .
 
Back
Top Bottom