Zanzibar kufuta mitihani ya Taifa na kuwa na Mfumo Mpya wa Elimu

Hivi elimu ikiwa inatolewa tu mtu anaenda mpaka chuo kikuu kuna ttz gani kwenye ajira sasa ndio kunaangaliwa utendaji kazi wa mtu kama anaweza au la
 
Na sisi Tanzania tufute tunasubiria nini?

---
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Mussa leo October 18,2023 ametangaza baadhi ya mabadiliko na mageuzi ya elimu ikiwemo sera na sheria mpya ambazo zitatarajiwa kuendana na mabadiliko hayo kwa Zanzibar yanayotarajiwa kuanza kwa Wanafunzi waliopo madarasa ya chini kuanzia darasa la kwanza, mabadiliko hayo ni pamoja na kufuta mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili.

"Serikali itaondoa mitihani ya Taifa ya darasa la nne na mitihani ya kidato cha pili, Serikali imeamua kufuta hii mitihani, kwanza sio kwamba inamfanya Mwanafunzi ahitimu au inamfanya Mwanafunzi asiendelee kusoma lengo la mitihani ni kumpima kafaulu au hakufaulu, tutaandaa utaratibu mwingine mzuri”
 
Hawa waislamu kuhusu elimu munawalazimisha tu! Hawapendi elimu! Wao wanasema "elimu dunia" sio muhimu! Wanasisitiza elimu aela! Ndio maana kundi la kigaidi halipendi angalau kwa uchache mtoto wa kike kwenda shule! Alafu hawa jamaa_vikofia kwa kulalamika wakitaka nyazifa za juu huku elimu hawana!
 
ohoooooooo
 
Hilo lina uhusiano gani na Uzi, kwanini unaingiza waislamu wote kwenye uzi usio wahusu, ......hivi unajua waislamu Tanzania bara ni wengi zaidi ya mara 10, kwa waislamu walioko zazobar?........
 
Kwa hiyo bara kuna waislamu takribani milioni 20 tu? Duh bora ujenge hoja kwa namna nyingine lakini sio kwa kubaka takwimu
Hilo lina uhusiano gani na Uzi, kwanini unaingiza waislamu wote kwenye uzi usio wahusu, ......hivi unajua waislamu Tanzania bara ni wengi mara 10, kwa waislamu walioko zazobar?........
 

Hawa jamaa jinsi wanafunzi wao wanavyokuwa weupe ukikutana nao chuo, sijui itakuaje wakiendelea kuifanya elimu yao kuwa nyepesi...
 
Hapa umechanya vitu viwili ambavyo ni kimoja Tanzania na Zanzibar.. Japo ungesema Tanganyika na Zanzibar

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point yako nini?
 
Zanzibar kitambo tu hakuna darasa la saba Bali form 2 ndio ilikuwa kama la 7, ila hilo la mafunzo ya amali ndio jipya.
 
Mifumo ya kuchujana imepitwa na wakati ni muda sasa wakutazama competence ya mtu katika fani husika.
 
Nje ya mada... huyo dada ana sauti tamu sana asee.... Dah kanifikisha mbali sana.
 
Duh! Sasa kumbe umuhimu wa majaribio kwa mwanafunzi umesahaulika. Mi naona wangekuwa wanaishia la 6 halafu elimu kwa vitendo. Kuondoa hadi Mitihani?
 
Zanzibar kitambo tu hakuna darasa la saba Bali form 2 ndio ilikuwa kama la 7, ila hilo la mafunzo ya amali ndio jipya.
We wajua me natokea wapi mpaka wataka kunidanganya hivi πŸ˜…πŸ˜… unajua me nimesoma wapi πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜€ acha hizo bhna
 
Elimu ya msingi na Sekondari sio ishu ya muungano!
 
Duh! Sasa kumbe umuhimu wa majaribio kwa mwanafunzi umesahaulika. Mi naona wangekuwa wanaishia la 6 halafu elimu kwa vitendo. Kuondoa hadi Mitihani?
Mitihani ni utumwa mwanafunzi anakuwa hasomi kwa ajili ya kuelewa ila kwa ajili ya kufanya mtihani tumetengeneza taifa lenye Madaraja Makubwa ya kitaaluma yasiyo na tija kwa muda mrefu...

Unakuta mtu ana A ya Physics olevel na advance ila hajui kufanya hata Wiring na muoga wa umeme wakati enzi za mwalimu mtu kama huyo anatakiwa awe amajiriwa TANESCO au Sehemu anapga engeneer

Sasa inatosha!
 
Kwenye hili la mafunzo ya amali, Zanzibar wametutangulia, au wametuzidi!. Huku Tanzania bara mafunzo ya amali ni kwa vilaza tuu, yaani failures!. VETA ilikuwa ni kwa waliofeli!.

Hili la Zanzibar kufuta mitihani ya NECTA nalo zuri, maana Zanzibar wanafeli hadi kuonekana kama ni vilaza!, niliwahi kuwauliza humu Inawezekana Vipi Zanzibar Kuna Div I, Div II, na Div III Chache, Ila Div IV na Div Zero Nyingi?!.

Nashauri kwa mabadiliko hayo, Zanzibar wajiandae kuwa na vyuo vikuu vyao nje ya TCU, na ajira zao, zisizo hitaji cheti cha GCE, maana mtihani muhimu kuliko mitihani yote ni mtihani wa form 4, bila cheti cha form 4, haujiungi chuo kikuu chochote zaidi ya Open University, wala huendi scholarship yoyote au kudahiliwa chuo kikuu chochote cha nje, labda waanzishe na vyuo vikuu vya kuwapokea hao wahitimu wa mafunzo ya amali, kuwe na chuo kikuu cha uvuvi, chuo kikuu cha mwani, chuo kikuu cha karafuu etc, lakini kuingia chuo kikuu chini ya TCU, huwezi kudahiliwa bila cheti cha NECTA, unless kama ni maandalizi ya Kwaheri Mkoloni Mweusi!.

P
 
Elimu ya msingi na Sekondari sio ishu ya muungano!
Hakuna sehemu nilipozungumiza Swala la Muungano!
Nilichosema ni kwamba Swala hilo lilikwisha Tangazwa na Wizara Ya elimu ya JMT (Jamhuri ya Muungano Tangu mwezi may 2023)

Ok hata hivyo bado unaonekana hata katiba hauijui vizuri Elimu ya Msingi na secondary zinaendeshwa chini ya baraza la Mitihani NECTA...

NA BARAZA LA.MITIHANI LIPO CHINI YA ISHU ZA MUUNGANO

Chukua katiba yako Taratibu nenda kwenye Misc. 1 Au Nyongeza ya 1 Mambo yanayohusu Muungano Soma jambo la 16
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…