Zanzibar kufuta mitihani ya Taifa na kuwa na Mfumo Mpya wa Elimu

Kwetu ndo ilikuwa Ya kwanza kupitishwa hii sheria
 
Mwenzio kaleta mambo ya Zanzibar wewe unasema lilishatangazwa na waziri wa JMT huoni unajichanganya?
 
Mwenzio kaleta mambo ya Zanzibar wewe unasema lilishatangazwa na waziri wa JMT huoni unajichanganya?
Sasa nimejichanganya wapi hapo Mleta mada baada ya kusema hivyo na yeye akasema kuwa alikuw hafahamu kama wametangaza!
Kwahyo pengine nimemfumbua macho maana Lengo lake alitamani Iwe ni jambo la pamoja kati ya Tz bara na Zanzibar...
Hata hivyi zanzibar ni sehemu ya Muungano kwahyo sioni kama kuna shida!
 
Ukweli kwa hili lakumfanyia assessment mwanafunzi badala ya kumpima kwa siku moja naunga mkono 100% baada ya miaka 10 Zanzibar itakuwa mbali sn kwenye ujuzi badala ya kukaririshana, kwenye mazuri tupongeze hata sisi Tanganyika tuige hiki kitu.
Hakuja ujuzi hambao hauna foundation nzuri, na foundation modules ndo ngumu maana ndo zina mjemga mtu kuisuka idea yake
 
Shule za Zanzibar kwa miaka nenda rudi zimekuwa za mwisho kwenye mitihani ya taifa, suluhisho si kukimbia na kutafuta namna ya kuwalegezea watoto wao bali wazazi waweke mkazo kwenye elimu dunia pia wajifunze kuumia pindi watoto wao wanapofeli.
Hili limekuwa likifanywa makusudi na NECTA ili ionekane hivyo.
 
Asante kwa taarifa.
 
Bila physics, chemistry, biology, mathematics tutapigaje hatua.
 
Hii nchi mi maishangaa sana badala ya kujenga vyuo vya ufundi na kutoa elimu mbadala ya ufundi tangu msingi wao wanaangaika na kujenga mashule na madarasa.. tukubaliane sio kila kichwa cha kufundishwa physics, chemistry,math, bookkeeping n.k
 
Ukweli kwa hili lakumfanyia assessment mwanafunzi badala ya kumpima kwa siku moja naunga mkono 100% baada ya miaka 10 Zanzibar itakuwa mbali sn kwenye ujuzi badala ya kukaririshana, kwenye mazuri tupongeze hata sisi Tanganyika tuige hiki kitu.
Na kwenye utalaamu je? Maana baadhi ya mifumo inafanya vizuri kwenye nchi ambazo tayari zina wataalamu wao - mfano wanasayansi, watafiti katika masuala mbalimbali, nk. Tunaweza kuiga mfumo fulani wa elimu kumbe tukasahau mambo muhimu yanayofanyika kutoka huko tulikoiga. Pia kama mfumo wetu wa elimu utazaa matabaka ya watu - mfano: wabobezi na wengine wa 'rasharasha' tutatengeneza tatizo lingine.

Kuna articles nyingi nimekuwa nikizisoma kuhusu the 21st century skills (soft skills). Watunzi wanasema kama kuna watu wanatafuta ajira - kwa mfno - employers wanachokitafuta, pamoja na technical (hard) skills ambazo tunazipata darasani ni soft skills ambazo tunajifunza nje ya darasa. Sasa uelewa wa watu wengine ni kwamba technical (hard) skills hazitakiwi, isipokuwa soft skills. Unaona hiyo tofauti?
 
Zanzibar imeathiriwa sana na mafunzo ya kidini/madrasa kiasi kwamba wanafunzi wao hawawezi kuwa na matokeo mazuri sambamba na wenzao wa bara kwenye mitihani ya NECTA/NECTVET. Shule zao haziwezi kushindana kwa matokeo mazuri na shule za bara. Zinafanya vibaya mpaka aibu, kuzipata shule zao kwenye top ten ni shughuli pevu.

Bora wakimbie aibu waanzishe mifumo yao ya mitihani wajipongeze wenyewe huko. Ila kwa upande mwingine wanajitoa taratibu kwenye muungano, hiyo ni hatua mojawapo ya kujitoa kwenye muungano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…