Zanzibar Kujiunga na Dubai (U.A.E)

Naona Zanzibar ‘wanajiunga’ na Dubai hatimae


Update: 25/08/2021
Naona Dubai wameanza kuichukua taratibu, kampuni ya xCassia toka Dubai inatarajia kuanza ujenzi wa jengo refu zaidi la pilili kwa Afrika ili kukuza utalii Zanzibar



The Zanzibar domino tower
 
Nadhani siku ikitokea hivyo wazanzibari watafrai sana maana wanahisi hawafaidiki na lolote na huu Muungano wa kulazimishana, wanahisi huu Muungano umesimamishwa na kuwepo kwa nguvu za dola, sasa wakijiunga na Dubai alau watajikwamua kiuchumi
Tangu lini ukawa koloni la mtu mweusi hasa mwenye akili kama za CCM na ukafanikiwa?

Kwa CCM hii, hata ukionekana una mawazo ya kuwavusha kama taifa wao watakuua au kukubambikia mambo ya uongo ili ushindwe au ukimbilie huko.

Walianza kumfukuza Oscar Kambona miaka hiyo. Wakaua biashara zote za watu waliokuwa wamefanikiwa, wakawaita wahujumu uchumi. Wakaua siasa na mawazo mbadala, waliojaribu kulalamika wakapotezwa au kubambikiwa makesi ya kuwa siyo raia. Ukianza kusimulia hufiki mwisho.
 
Hujapenda au umependa hilo?
 
Njaa kitu kibaya. Hawa watumwa wa kujitakia. Wangejua waarabu wanavyodharau waswahili wala wasingepoteza muda. Je JMT itawaruhusu kufanya uhaini huu?
 
Itawaruhusu kwasababu ile ni nchi kamili.
Ilikuwa nchi kamili kabla ya muungano. Kuna haja ya kuacha kujidanganya na kujiridhisha. Ingekuwa nchi kamili isingepewa mgao wa bajeti yake badala ya kujiamulia itumie na kuweka kiasi gani. Zanzibar haina ubavu ndani ya Muungano kama nchi. Rejea baada ya Nyerere kuondoka na kutaka urais uwe wa zamu. Baada ya Mkapa si aliingia Kikwete na kufuatiwa na Magufuli? Na kama siyo kifo cha Magufuli huenda hata rais ajae angetoka Bara na bado Znz ikanywea na mwenyekiti wake wa BMZ ambaye hana seniority astahikiyo bara.
 
Muungano wetu unadumaza maendeleo kwa pande zote mbili.
Serikali ya Tanganyika irudi haraka ili sasa tuamue aina ya Muungano kama ni lazima uwepo au tutosheke na ushirikiano kama nchi jirani.
Kila nchi idemke kivyake
 
Huu muungano ni bure kabisa Tanganyika tunaihudumia zanzibar wakati bara changamoto ni nyingi
 
Tanganyika hatufaidiki na zanzibar..waende tu!! na kwetu watoke wote dadek...
 
Wajiunge tu ila na huo ndio uwe mwisho wa muungano, lakini huo uwekezaji wao sisi watanganyika autotufaidisha na lolote zaidi ya kulipuliwa na mabomu maana sasa watakuwa na wafadhili wa kutosha
Shida iko pale Loliondo na Ngorongoro, shida ipo pale tu
 
Hao Oman ndio wanapewa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo sasa kama hujui
 
Mu Imarat hatakagi ujinga mambo ya copy na paste hanaga imetoka hiyo check mdosi atakavyo mwagika zenji
 
Roho zitawauma sana, Zanzibar itaendelea kuwa kaka zenu wakubwa, daima.
 
Wewe ndiyo wale mnaogawanywa mtawaliwe unachekelea. Zanzibar ndiyo lilikuwa taifa lako kabla ya kuja mzungu na kukugawa. Punguani wahed.

Hata Nyerere aliyetawala miaka 23 tu kwake analipiwa kila kitu, itakuwa waliokutawala miaka na miaka ya mamia kama si maelfu? Ilitakiwa hata usiliseme hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…