Zanzibar kujiunga OIC ni lazima, si la Mzee wa CHADEMA tu. Dr. Salmin Amour alipokuwa Rais alishalipitisha na kugonga Mhuri. Muda utaongea

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Salaam Wakuu,

Naona kuna watu wanataka kupotosha kuhusu swala la kujiunga OIC kwamba ni la leo. Yule Mzee wa CHADEMA kakumbushia tu Wazanzibari ajenda yao ya Miaka mingi.

Swala la OIC ni Ajenda ya Siri ya kila Mzanzibar. Asikudanganye mtu.

Mwaka 1992, Dk Salmin akiwa na miaka miwili madarakani, Serikali ya Zanzibar ilijiunga na Jumuiya ya kimataifa ya Kiislamu (OIC).

Hoja hiyo ilizua mvutano ndani ya Bunge la Jamhuri ikielezwa Zanzibar imevunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hali hiyo ilipelekea wakina Njelu Kasaka kuibuka na kundi la wabunge 55, maarufu G-55 wakidai wapewe Serikali yao ya Tanganyika kama Zanzibar imejiunga OIC.

Bunge lililokuwa linakaa Dar kwenye Ukumbi wa Karimjee, Agosti 23, 1993 Njelu Kasaka alitoa hoja binafsi bungeni ya kutaka kuundwa Serikali ya Tanganyika ndani ya Muungano.

Pamoja na hoja hiyo kuwa 'nyeti' na yenye kuhatarisha kuuvunja Muungano, Spika wa Bunge wa wakati huo Adam Sapi Mkwawa aliiruhusu kujadiliwa na akamuachia Naibu wake, Pius Msekwa asimamie Bunge kwenye huo mjadala kutokana na Spika Sapi kukabiliwa na matatizo ya kiafya.

Swala la OIC lioitikisa nchi mpaka kuhatarisha kuuvunja Muungano.

Mtafaruku huo wa Serikali ya Zanzibar chini ya Dk Salmin kujiunga na OIC ulisababisha Rais wa Muungano, Ali Hassan Mwinyi kufanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri na kumuondoa aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, John Malecela pamoja na Katibu Mkuu wa CCM Horace Kolimba.

Unaambiwa mwaka 1992, Zanzibar ikiwa chini ya uongozi wa Dr. Salmin Amour ilijiunga na jumuiya ya Kiislam ya OIC kwa maslahi ya nchi na wananchi wa Zanzibar. Nyerere akamuamuru rais wa Zanzibar kuitoa Zanzibar katika jumuiya hiyo kwa madai ati kuwa amekiuka katiba ya Tanzania.

Madai mbali mbali yaliibuliwa kuwa Zanzibar inataka kuleta utawala wa SHARIA kama vile yanavopandikizwa madai ya kutaka kurudisha usultani Zanzibar. Wananchi wa zanzibar wakaanza kuhoji "Ikiwa Zanzibar inataka kuleta utawala wa SHARIA au hata usultani, kwani Zanzibar ni ya nani?. Wao Tanganyika inawahusu nini"? "Kumbe wametufanya kuwa sisi ni koloni lao?".

Watu wanaotetea haki za wazanzibari na wanaopigania uhuru wa Zanzibar wamepitia mengi. Haya hayakuanza leo. Historia inajielezea, Hakika Maalim Seif, Dr Salmin, Aboud Jumbe Historia haitawasahu.

January 09, 1993:
Zanzibar inakiri kwamba ilijiunga na OIC

January 20, 1993:
Kamai ya BUnge ikiongozwa na Mh. Philip Marmo inaamua kuchunguza na kuona kama kweli Zanzibar imejiunga na OIC

Waziri Kiongozi wa Zanzibar, Dr. Omar Ali Juma anaitisha kikao na viongozi wa dini na kuwabembeleza kwamba Zanzibar si taifa la kiislamu kwani katiba ya nchi haina dini.

January 28, 1993:
Hassan Diria anahamiswa kutoka kuwa Waziri wa mambo ya nje na kuwa waziri Kazi na Vijana, anabadilishana Wizara na Joseph Rwegasira.

February 02, 1993:
Rais wa Zanzibar, Dr. Salmin Amour anatangaza kwamba ni kweli Zanzibar ilijiunga na OIC na haijavunja katiba ya Tanzania.

February 15, 1993:
Rais wa Zanziba, Dr. Salmin Amour anahutubia semina ya Bunge la Muungano anasema Zanzibar hajavunja mkataba wa muungano.

February 17, 1993:
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Philip Marmo, anasema Zanzibar imevuna mkataba wa Muungano.

February 18, 1993:
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba, Philip Marmo, anawasilisha ripoti bungeni kuhusu Zanzibar kujiunga na OIC. Bunge linataka hatua kali kwa waliohusika.

July 30, 1993:
Wabunge 55 (G55) wa CCM wanaleta taarifa ya kuleta hoja ya kuwa na serikali ya Tanganyika ndani ya muungano.

August 13, 1993:
Rais wa Zanzibar baada ya shinikizo la bunge na vikao vya NEC-CCM vilivyohudhuriwa na Julius Nyerere, Zanzibar inajitoa kwenye OIC.

August 24, 1993:
Bunge la Tanzania linapitisha hoja ya kuwa na serikali ya Tanganyika ndani ya muungano.

November 02, 1994:
Julius Nyerera anazindua kitabu cha "Uongozi wetu na hatina ya Tanzania'. Anaeleza mfululizo wa OIC, Utanganyika na Umakamu wa Rais. Anasema Waziri Mkuu, John Malecela na Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba wanapaswa kujizulu kwa kumshauri vibaya Rais Ali Hassan Mwinyi

November 02, 1994:
Katibu mkuu wa CCM, Horace Kolimba anakataa kwamba hana kosa lolote na haoni sababu ya kujiuzulu. KWamba hakuchaguliwa na Julius Nyerere, alichaguliwa na wana CCM.

December 02, 1994:
Katibu mkuu wa CCM, Horace Kolimba anajiuzulu. Rais Mwinyi analivunja baraza la Mawaziri na kumwondoa John Malecela, kisha Cleopa Msuya anakuwa Waziri Mkuu mpya.

Swala la OIC likazimwa hivyo kimabavu lakini halikufa.

Mwaka 20214 wakati wa Tume huru ya Katiba likaibuka tena. Safari hii Wazanzibar wakaorodhesha matakwa yao wakimanisha hawataki kuingiliwa kiuchumi.

Ikaundwa Kamati ya Kuwaunganisha Wazanzibari. Kamati hiyo ikaja na mambo tisa ya Msingi yapelekekwe Dodoma na Mapendekezo hayo yamewasilishwa kwa Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir kificho, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.

Kamati hiyo ya Zanzibar iliyoongozwa na Ali Abdullah Suleiman ilipendekeza mambo yanayopaswa kutetewa na kuzingatiwa na wajumbe wa Bunge la Katiba ikiwamo Zanzibar kupewa mamlaka kamili ya kusarifu na kushughulikia uchumi wake bila ya kuingiliwa na taasisi yoyote katika mfumo wa Muungano.

Mwenyekiti wa kamati hiyo ambayo iliundwa na Taasisi ya Utafiti na Sera za Umma (ZIRRP), Ali Abdullah Suleiman, wakati anaongea mbele ya wanahabari alisema "lazima Katiba Mpya itoe haki na hadhi sawa kwa nchi mbili zilizoungana kama Ibara ya 64(5) ya Rasimu ya Katiba inavyopendekeza ili kuondokana na upande mmoja wa muungano kuonekana unanyonywa kama ilivyo sasa".

Pia walitaka Zanzibar ipewe mamlaka ya kuanzisha Benki yake (State Bank) pamoja na kuwapo kwa Benki Kuu ya Tanzania kama inavyopendekezwa katika masharti ya Ibara ya 234 ya Rasimu ya Katiba ya Warioba.

Mambo mengine mengine yaliyopendekezwa ni kuhakikisha Zanzibar inapata mamlaka ya kujiunga na mashirika ya kikanda na kimataifa kama vile FIFA, OIC, SADC, EAC, UNESCO, WHO na FAO.

Kamati ilitaka Rais wa Tanzania awe anapatikana kwa utaratibu wa zamu baina ya pande mbili za Muungano na Rais wa Zanzibar arejeshewe hadhi yake ya kuwa Makamu wa Rais wa Muungano.

Kamati ilitaka Zanzibar kuanzisha idara yake ya polisi, pamoja na kuwapo kwa jeshi la polisi la Muungano kama Ibara ya 232 (1) (2) ya Rasimu ya Kwanza ya Katiba ilivyokuwa imependekeza na kuhakikisha Zanzibar inapata mamlaka yake ya kuanzisha idara ya usalama wa Taifa pamoja na kuwapo kwa idara kama hiyo ya Muungano.

Kamati ilitaka ajira katika utumishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinatolewa kwa utaratibu wa uwiano kama ilivyoshauriwa na kupendekezwa katika Rasimu ya Ibara ya 185(1) na (2) ili kuweka usawa baina ya pande mbili za Muungano.

Tarehe 01 Oktoba siku ya Wazee Dunia, Mzee katika Kongamano la Wazee wa CHADEMA alikuja na hoja ya Zanzibar kujiunga OIC. Wananchi wanamshambulia sana kana kwamba yeye ndo wa kwanza kupendekeza hivyo.

kwenye Mkutano huo ulioandaliwa na CHADEMA, mmoja wa washiriki alitoa kauli akitaka Serikali kujiunga na OIC (Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu) akidai kwa sasa Viongozi wengi wa Serikali ni wa dini ya Kiislamu. Anaamin Bara ndo wanakwamisha Mpango huo.

Je, Tanzania wataweza kuzima hoja ya Zanzibar kujiunga OIC? Kwa maoni yangu naona haiwezekani. Ni swala la Muda tu.
 
View attachment 3114044

Many lay men are ill informed about OIC, sijui ni kwasbb za chuki źa kidini au ignorance OIC ina faida nyingi za kiuchumi kuliko udini kwa mfano uganda waislamu ni 30% ila ni wanachama kamiri wa OIC, wanapata mikopo na uwekezaji wa bila riba, sijui kwanini nchini kwetu kuna negativity kuhusu OIC.
 
chuki za uislamu ni kubwa sana kwenye hii nchi
 
Uganda Waislam hawafiki hata 15%
 
Many lay men are ill informed about OIC, sijui ni kwasbb za chuki źa kidini au ignorance OIC ina faida nyingi za kiuchumi kuliko udini kwa mfano uganda waislamu ni 30% ila ni wanachama kamiri wa OIC, wanapata mikopo na uwekezaji wa bila riba, sijui kwanini nchini kwetu kuna negativity kuhusu OIC.
Uganda na Somalia kwa mfano zimejiunga na OIC nipe mafanikio yao?
OIC bila kupepesa macho ni jumuia ya kidini na suala la kidini ni very sensitive, kwa wenye akili timamu wataliona na wameliona hili.
 
Suala lenye uhusika wa dini ni very sensitive, kama wazanzibari wengi wanataka kuona Zanzibar ikijiunga na OIC, na wanajua sababu kubwa ni kuwa part ya jamhuri ya muungano ndio inawazuia azma yao hii kwa nini wasilazimishe kura ya maoni wajitoe tu kwenye huu muungano?

Huwezi kula mbuzi halafu ukabaki nae! Waamue moja kama OIC benefits zake zinazidi muungano wajitoe tupate amani.
 
chuki za uislamu ni kubwa sana kwenye hii nchi

..kujiunga na OIC haimaanishi Tanzania tumekuwa nchi ya Kiislamu.

..Misri, Morroco, Libya, Tunisia, wamejiunga African Union, na aliyewabadilisha kuwa Waafrika, bado ni Waarabu.
 
Mfano wako ni irrelevant hakuna kigezo kwa nchi hizo kuweza kujiunga African Union? Inawezekana Syria nao kujiunga African Union?
 
Wajitoe kwenye Muungano then wajiunge itakuwa poa tu

. Lakini watakuwa tayari wooote waondoke Bara waende kisiwani kuanza maisha upya. Wataweza?

OIC ina faida chache na hasara nyingi

Mzee alikurupuka haikuwa mahali pake

Haiwezi kujiunga sababu sio nchi kamili.
 
..kujiunga na OIC haimaanishi Tanzania tumekuwa nchi ya Kiislamu.

..Misri, Morroco, Libya, Tunisia, wamejiunga African Union, na aliyewabadilisha kuwa Waafrika, bado ni Waarabu.
Unajua malengo ya OIC?
 
Dr. Salmin Amour alipokuwa Rais alishalipitisha na kugonga Mhuri
Ukiona mtu anagonga muhuri na kupitisha halafu halitekelezwi, ujue cheo chake hakina mamlaka hayo. Urais wa Zanzibar ni wa kuutambia humu humu ndani ya nchi, akitoka tu nje lazima ataulizwa rais wako yuko wapi
 
Mfano wako ni irrelevant hakuna kigezo kwa nchi hizo kuweza kujiunga African Union? Inawezekana Syria nao kujiunga African Union?

..kujiunga OIC sio lazima uwe nchi ya Kiislamu kama Saudi Arabia, au Kuwait.

..Na nimeuliza mbona Tunisia ni nchi ya Kiarabu lakini ni mwanachama wa Umoja wa Afrika?
 
Hujielewi kwani Tunisia iko bara la Afrika au arabuni, fanya homework yako vizuri wana asili ya kiarabu lakini wako bara la afrika kama vile Turkey wana asili ya kiarabu lakini wako Ulaya.

Hebu nieleze malengo ya OIC na kwa nini wajiite jumuia ya nchi za kiislamu?
 
..Zanzibar asilimia 99 ni Waislamu, na wanapenda kuwa wanachama wa OIC. Sasa kwanini Tanganyika iwazuie.

..Mimi ni Mtanganyika na sioni shida kama Tanzania ikijiunga na OIC ili kutimiza ndoto ya ndugu zetu wa Zanzibar.
 
Uganda na Somalia kwa mfano zimejiunga na OIC nipe mafanikio yao?
OIC bila kupepesa macho ni jumuia ya kidini na suala la kidini ni very sensitive, kwa wenye akili timamu wataliona na wameliona hili.
paschal mayalla atakwambia inamanufaa lakini hawezi kukueleza kinagaubaga ni jinsi gani watanufaika zaidi kuliko ilivyo Sasa. Binafsi ninaona ni upuuzi mwingine miongoni mwa choko choko nyingi walizonazo wazanzibar pindi Rais wa JMT anapokuwa muisilamu.
 
Mfano wako ni irrelevant hakuna kigezo kwa nchi hizo kuweza kujiunga African Union? Inawezekana Syria nao kujiunga African Union?

Hata hajui kuwa Kuwa mwarabu ni swala la "race" ... yaan sijui anahisi kuwa africa kigezo uwe mweusi .. huyu kweli hata geography ya primary schools alisona kweli..

Sitashangaa akiwaweka Iran kundi la waraabu au Turkey akiwaweka Mashariki ya kati
 
Unapofanya jambo hilo kuwa la lazima unaibua hoja ya kuvunja Muungano.

Trust me the moment wanajiunga na hiyo jumuiya zitaibuka hoja za utanganyika na Muungano utavunjika.

Tuwe makini katika hili.
 
Back
Top Bottom