Zanzibar kushusha mabasi ya umeme, gesi, Rais Mwinyi atoa tamko

Zanzibar kushusha mabasi ya umeme, gesi, Rais Mwinyi atoa tamko

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
“Serikali tunataka kubadilisha taratibu za usafiri ndani ya Mji wa Unguja, tunataka kuleta mabasi ya kisasa yanayotumia gesi au umeme ili kupunguza kuchafua hewa.

“Tunataka kuendelea ili tusiwe tunapakiwa kama mizigo, duniani kote mambo yamebadilika hasa katika miji mikubwa, wanaleta mabasi ya kisasa.

"Abiriwa wanatwakiwa kuingia bila ya fujo wala vurugu, lakini kwa sasa wenye biashara ya mabasi wasiwe na wasiwasi kwa kuwa tutayaondoa mjini tu mabasi yao yaliyopo lakini bado yataendelea kufanya kazi maeneo mengine, mji huu ni mkubwa, kuna maeneo mengi

"Mjini lazima magari yawe ya kisasa, anapokuja mtu baada ya miaka mitatu hadi mitano aone kuna mabadiliko Zanzibar,” Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na wanahabari leo Februari 28, 2022.
 
Uko Zanzibar hizo Daladala tu zinafanya kazi Kwa zamu, Unakuta Gali inaingia barabarani Mara 2 au 3 kwa wiki.
 
Ally Kessy aliposemaga bungeni Zanzibar ni ndogo unaweza zunguka kwa baiskeli na ukipiga filimbi watu wote wanasikia. Kumbe alikuwaga muongo mzee Kessy.

Siasa hizi, sijui yupo wapi Ally Kessy mbunge wa Nkasi huko Sumbawanga.
 
Uzunguke na baiskeli mji mkongwe Hadi chake chake!?..hiyo filimbi utapiga ukiwa wapi ili kaskazin wasikie!?...au Zanzibar anamaanisha nini!?
 
Haya ya kwetu sijui mwendokasi yamekopa kama vifaru vya mrusi
 
Ally Kessy aliposemaga bungeni Zanzibar ni ndogo unaweza zunguka kwa baiskeli na ukipiga filimbi watu wote wanasikia. Kumbe alikuwaga muongo mzee Kessy.
Siasa hizi, sijui yupo wapi Ally Kessy mbunge wa Nkasi huko Sumbawanga.
Ugunja badogo sn jamani tuache utani hata Kibaigwa ni kubwa
 
Back
Top Bottom