Zanzibar: Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe Bi Awena waambukizwa virusi vya Corona

Zanzibar: Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe Bi Awena waambukizwa virusi vya Corona

Wacha kumsingizia Mungu kwenye mambo yenu ya kipuuzi ya siasa.
Mkuu, unanionea. Mimi sio muasisi wa uamini huo unaonikaripia juu yake, labda kosa langu ni kutoyaweka maneno hayo katika 'quotation marks' ili yaonekane kuwa siyo yangu.
Wiki hii tu nimezika watu wangu wa karibu wanne na wengine wa mbali 6 kwa Corona. Endeleeni kutania. Makaburi bado hayajajaa . Puuzeni huu ugonjwa, ubadilisheni majina.
OOooh, POLE SANA mkuu! Hali ni mbaya kiasi hicho, huku tukiambiwa tupo salama?
Toeni vitisho Leteni Jokes lkn Kifo ndio msema kweli.
Binafsi siyo sehemu ya hao unaowasema hapa, kwa sababu naelewa vizuri kabisa makosa wanayoyafanya hawa watu.

Naona maana ya bandiko langu imepotea katika kosa nililolitaja hapo juu! Niliuliza kwa maksudi mazima 'incubation period' ya gonjwa hilo na uhusiano wake na safari alizozifanya mgonjwa hivi karibuni - 'all that was lost in translation'!
 
January 30, 2021
Nimeguswa kuona mkutano huu wa kampuni tanzu ya Barrick hapa Tanzania watu asilimia kubwa yaani 95% wamevaa barakoa na kujiwekea nafasi baina ya mtu na mtu kipindi hiki cha Corona

30 Jan 2021
Mjumbe wa bodi ya kampuni ya madini ya Twiga, Casmir Kyuki amedokeza kuwapo kwa matumaini ya Serikali ya Tanzania kulipwa deni lake la Dola200 milioni ( sawa na Sh463 bilioni) ambazo inaidai kampuni ya Barrick, ikiwa mwenendo wa soko la dhahabu duniani utaendelea kuwa mzuri kama ulivyo sasa. Fedha hizo ni sehemu ya Dola 300 milioni (Sh695 bilioni) ambazo Barrick iliahidi kuzilipa kama fidia, kutokana na kampuni yake tanzu ya Acacia kudaiwa kodi na tozo mbalimbali na mamlaka za serikali ya Tanzania Malipo ya fedha hizi zilikuwa miongoni mwa makubaliano kati ya Kampuni ya Barrick na Serikali ya Tanzania ya uendeshaji wa shughuli za madini yaliyosainiwa Julai, 2019 na baadae kuanzishwa kwa kampuni ya madini ya Twiga, Oktoba, 2019.
Source : Mwananchi digital
 
Haya ndio matatizo ya kuwapa nafasi vyama vya mifukoni kama ACT na Chadema kila kitu wanaleta uchama uchama tu, wewe unavyoona ni sawa mfano Samia taarifa zake zitolewe na Ofisi ya CCM badala ya ofisi yake??

Ndio maana Mungu anatuepusha Sana na vyama Kama hivi visutuletee majanga tu
umeongea ishu ya msingi sana hata mm huwa ninashangaa hata mambo ya kitaifa utasikia sante sana chama cha mapinduzi
 
Wacha kumsingizia Mungu kwenye mambo yenu ya kipuuzi ya siasa. Corona ipo na km hakuna hatua za maana zitachukuliwa watanzania wataendelea KUFA siku hadi siku.

Wiki hii tu nimezika watu wangu wa karibu wanne na wengine wa mbali 6 kwa Corona. Endeleeni kutania. Makaburi bado hayajajaa . Puuzeni huu ugonjwa, ubadilisheni majina.

Toeni vitisho Leteni Jokes lkn Kifo ndio msema kweli.
Asalam alaykm warahmatullah wabarakatuh. Pole.sana mkuu
 
Wacha kumsingizia Mungu kwenye mambo yenu ya kipuuzi ya siasa. Corona ipo na km hakuna hatua za maana zitachukuliwa watanzania wataendelea KUFA siku hadi siku.

Wiki hii tu nimezika watu wangu wa karibu wanne na wengine wa mbali 6 kwa Corona. Endeleeni kutania. Makaburi bado hayajajaa . Puuzeni huu ugonjwa, ubadilisheni majina.

Toeni vitisho Leteni Jokes lkn Kifo ndio msema kweli.
Ila hata ule waraka wa maaskofu katoliki nao ulisema corona ilipungua mwaka jana na walihusisha Mungu,nafikiri ndio maana hata kampeni zilifanyika bila tahadhari kwa imani ya kwamba corona ilipungua.
 
TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19

Chama cha ACT Wazalendo kinawajuilisha wanachama wake, Wazanzibari, pamoja na umma wa Watanzania, kuwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe, Bi Awena, pamoja na Wasaidizi wake kadhaa wa karibu, wamethibitika kupata maambukizi ya Virusi vya Covid 19 baada ya kufanyiwa vipimo.

Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi Madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalumu katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu dhidi ya Korona. Hivyo basi, tangu juzi Ijumaa jioni, Maalim Seif alipumzishwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar, ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa Madaktari.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa hali ya Maalim Seif pamoja na mkewe zinaendelea vyema kabisa, Viongozi wenzake pamoja na Wanafamilia wamekuwa na mawasiliano naye ya kawaida kila siku.

ACT Wazalendo tunawaomba wanachama wetu, Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kumuombea dua Maalim Seif katika kipindi hiki ambacho amepumzishwa ili aweze kupona kwa haraka na arudi kuendelea na majukumu yake. Pia, tunarejea wito wetu kwa Watanzania wote kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ugonjwa huu.

Ado Shaibu,
Katibu Mkuu,
ACT Wazalendo
31 Januari, 2021.

Chanzo: TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19

MY TAKE:

Hivi karibu Januari 14, 2021 Seif alitembela Chato. Je, Watu aliyokutana nao tahadhari?

Soma: Rais Magufuli: Maalim Seif ni Kiongozi kweli, aliacha 'interest' zake na kutanguliza za Wazanzibari

Je ni kwa nini wazee wote kuanzia miaka 65 wasipewe chanjo???
 
Mkuu wa nchi ana Ph.D ya Chemistry, atakuwa kashaipitia hiyo. Anajua mpaka boiling point ya Silver kichwani.

Kama hujaelewa, sema tu wewe hujaelewa. Usimsingizie mkuu.
Anaelewa mengi sana ya kisayansi huyo bwana. Hata kule kujifukizia kakuelezea kisayansi, kwamba mvuke ule una joto kali sana kiasi cha kumbabua virus yule akiyeko ndani ya 'cells' za binaadamu bila kuidhuru 'cell' husika!

Hakuishia hapo, akaamuru uhakiki wa vipimo vya COVI-19 ufanywe kwa kutumia mapapai, kondoo, mbuzi,n.k., na vikaonekana havifai kabisa kwa kuwa vitu hivyo vilionekana kuwa na corona.

Huo ukawa ndio ushahidi wa Tanzania kusitisha kupima na kutangaza idadi ya maambukizi ya ugonjwa huo, kabla ya kugundua kwamba maombi yetu kwa Mungu yalikuwa ndio kinga ya kipekee kabisa. Mungu wetu katuondolea kabisa corona, na hatukusita kuitangazia dunia juu ya matokeo ya maombi yetu hayo.

Uchunguzi wa dawa yetu ya Madagascar unaendelea? Pengine matokeo yake ndio sababu ya sisi kutohitaji hii chanjo hatari inayolenga kuwamaliza watu weusi, kwa sababu tu ya utajiri wetu tulionao nchini mwetu.

Mwanasayansi wetu huyu anajua mengi sana. Tumsikilize kwa makini.
 
Nadhani wamesahau kuwa huyo ni Makamu wa Kwanza wa Rais,

Hivi vyama bado ni vichanga mno vikishika dola tutashuhudia maajabu zaidi ya haya.
Kwani ugonjwa ni aibu !!. Wafuasi wa u dictator mnatupeleka wapi ?!

Odhis *
 
Haya ndio matatizo ya kuwapa nafasi vyama vya mifukoni kama ACT na Chadema kila kitu wanaleta uchama uchama tu, wewe unavyoona ni sawa mfano Samia taarifa zake zitolewe na Ofisi ya CCM badala ya ofisi yake??

Ndio maana Mungu anatuepusha Sana na vyama Kama hivi visutuletee majanga tu
Unajua maana ya chama kushika hatamu au unabwabwaja tu ?
 
Wacha kumsingizia Mungu kwenye mambo yenu ya kipuuzi ya siasa. Corona ipo na km hakuna hatua za maana zitachukuliwa watanzania wataendelea KUFA siku hadi siku.

Wiki hii tu nimezika watu wangu wa karibu wanne na wengine wa mbali 6 kwa Corona. Endeleeni kutania. Makaburi bado hayajajaa . Puuzeni huu ugonjwa, ubadilisheni majina.

Toeni vitisho Leteni Jokes lkn Kifo ndio msema kweli.
Dogo inakuwaje kumbe bado hupo?
 
Hii CORONA naona inagonga nyavu za pembeni na kutoka nje, inabidi itumbie golini kabisa watu tuinuke, ebo!
Waziri wa mambo ya nje wa China si alinidunga chanjo kule nyumbani kwangu chatle?
 
Back
Top Bottom