Zanzibar: Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe Bi Awena waambukizwa virusi vya Corona

TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19

Chama cha ACT Wazalendo kinawajuilisha wanachama wake, Wazanzibari, pamoja na umma wa Watanzania, kuwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe, Bi Awena, pamoja na Wasaidizi wake kadhaa wa karibu, wamethibitika kupata maambukizi ya Virusi vya Covid 19 baada ya kufanyiwa vipimo.

Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi Madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalumu katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu dhidi ya Korona. Hivyo basi, tangu juzi Ijumaa jioni, Maalim Seif alipumzishwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar, ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa Madaktari.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa hali ya Maalim Seif pamoja na mkewe zinaendelea vyema kabisa, Viongozi wenzake pamoja na Wanafamilia wamekuwa na mawasiliano naye ya kawaida kila siku.

ACT Wazalendo tunawaomba wanachama wetu, Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kumuombea dua Maalim Seif katika kipindi hiki ambacho amepumzishwa ili aweze kupona kwa haraka na arudi kuendelea na majukumu yake. Pia, tunarejea wito wetu kwa Watanzania wote kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ugonjwa huu.

Ado Shaibu,
Katibu Mkuu,
ACT Wazalendo
31 Januari, 2021.

Chanzo: TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19

MY TAKE:

Hivi karibu Januari 14, 2021 Seif alitembela Chato. Je, Watu aliyokutana nao tahadhari?

Soma: Rais Magufuli: Maalim Seif ni Kiongozi kweli, aliacha 'interest' zake na kutanguliza za Wazanzibari

Je ! Ni kweli hii taarifa ni feki au la ❓
Hata kama ni kweli ACT-WAZALENDO wamekosea kutangaza kuwa Maalim Seif anamepatikana na Corona; kwa sababu ni haki ya serikali kusema kuwa mhe.Maalim ana Corona kweli au la❗
Kimsingi ACT Wazalendo walipaswa kuvuta subira kwa kufahamu wa kutoa maelezo ni serikali katika kudumisha umoja wa kitaifa na si chama kama inavyonekana video katika mitandao ya jamii.
1612103205407.png

Is this where we at?

Mtu anaweza akafa mkasema hajafa huyo... , ni stunt tu ya kitu fulani ?
Easy bro, no harm meant. I didn't anticipate someone taking my comment that far.

President Mwinyi ni mtu mwenye kumheshimu sana President Magufuli. I expect him to pull off a stunt like that if he doesn't reiterate with Magu's current stand on the pandemic, in his quest to excuse Zenji from the said stand.
 
TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19

Chama cha ACT Wazalendo kinawajuilisha wanachama wake, Wazanzibari, pamoja na umma wa Watanzania, kuwa Mwenyekiti wake wa Taifa, Maalim Seif Sharif Hamad, Mkewe, Bi Awena, pamoja na Wasaidizi wake kadhaa wa karibu, wamethibitika kupata maambukizi ya Virusi vya Covid 19 baada ya kufanyiwa vipimo.

Katika hali ya kuchukua tahadhari zaidi Madaktari walimshauri Maalim Seif kuwa ni vyema awepo chini ya uangalizi maalumu katika kipindi chote atakachokuwa anaendelea na matibabu dhidi ya Korona. Hivyo basi, tangu juzi Ijumaa jioni, Maalim Seif alipumzishwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Unguja, Zanzibar, ambako anaendelea kuwa chini ya uangalizi wa karibu wa Madaktari.

Tunapenda kuchukua nafasi hii kuujulisha umma kuwa hali ya Maalim Seif pamoja na mkewe zinaendelea vyema kabisa, Viongozi wenzake pamoja na Wanafamilia wamekuwa na mawasiliano naye ya kawaida kila siku.

ACT Wazalendo tunawaomba wanachama wetu, Wazanzibari na Watanzania wote kwa ujumla kumuombea dua Maalim Seif katika kipindi hiki ambacho amepumzishwa ili aweze kupona kwa haraka na arudi kuendelea na majukumu yake. Pia, tunarejea wito wetu kwa Watanzania wote kuchukua hatua za kujilinda dhidi ya ugonjwa huu.

Ado Shaibu,
Katibu Mkuu,
ACT Wazalendo
31 Januari, 2021.

Chanzo: TAARIFA KWA UMMA Maalim Seif Apumzishwa Baada ya Kupata Maambukizi ya Covid 19

MY TAKE:

Hivi karibu Januari 14, 2021 Seif alitembela Chato. Je, Watu aliyokutana nao tahadhari?

Soma: Rais Magufuli: Maalim Seif ni Kiongozi kweli, aliacha 'interest' zake na kutanguliza za Wazanzibari

Mkiambiwa hamjafika umri wa kushika dola mnajaa mapovu.Maalimu Seif akubali tu arudi cuf hivi vyama vya wavuta bangi aachane navyo.Yaani chama kimejigeuza madaktari,
 
Easy bro, no harm meant. I didn't anticipate someone taking my comment that far.

President Mwinyi ni mtu mwenye kumheshimu sana President Magufuli. I expect him to pull off a stunt like that if he doesn't reiterate with Magu's current stand on the pandemic, in his quest to excuse Zenji from the said stand.
Nimekuelewa and will be a calculated clever and helpful tactic..., but with propaganda and controlling media and people unaweza kushangaa muhusika mwenyewe anakana kwamba huo ni uzushi I was Okay...
 
Anaelewa mengi sana ya kisayansi huyo bwana. Hata kule kujifukizia kakuelezea kisayansi, kwamba mvuke ule una joto kali sana kiasi cha kumbabua virus yule akiyeko ndani ya 'cells' za binaadamu bila kuidhuru 'cell' husika!......
I am not sure if you are being sarcastic or hagiographic.
 
Kipi Cha ajabu?
Mbona makamu wa pili Seifu Iddi aliwahi kujifungia.
 
Haya ndio madhara ya kuruhusu Wapinzani kuingia kwenye serikali, wanatoa siri za kambi!!!

Magufuli huko alipo atakuwa amenuna vibaya.
 
Nimekuelewa and will be a calculated clever and helpful tactic..., but with propaganda and controlling media and people unaweza kushangaa muhusika mwenyewe anakana kwamba huo ni uzushi I was Okay...
Zanzibar ni muhimu sana kwa utalii, binafsi ningependa irudi kwenye miongozo ya kisayansi hata kwa kuzuga tu ili kuwapa imani wateja wetu.

Hili jambo halina faida yoyote kulifanyia propaganda. But I trust President Mwinyi, he seems to be a visionary leader and Zanzibar will be ok
 
And Proffesionally ni Daktari sio Mganga wa Kienyeji......
 
Haya ndio matatizo ya kuwapa nafasi vyama vya mifukoni kama ACT na Chadema kila kitu wanaleta uchama uchama tu, wewe unavyoona ni sawa mfano Samia taarifa zake zitolewe na Ofisi ya CCM badala ya ofisi yake??

Ndio maana Mungu anatuepusha Sana na vyama Kama hivi visutuletee majanga tu
Corono ipo haipo!?😷😷
 
Back
Top Bottom