My Take
Hakuna kunyanyasana na watu wenye maneno meengi na fitina wa bara lakini.
----------------
Serikali ya Zanzibar imeweka mipango ya kuanzisha shirika lake la ndege, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufungua safari za moja kwa moja za kimataifa na kukuza sekta ya utalii visiwani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari Siku ya jumatatu Aprili 27,2026 katika maandalizi ya mkutano wa uwekezaji wa Zanzibar (Zanzibar Investment Summit 2026), Waziri wa Kazi na Uwekezaji, Shariff Ali Shariff, alisema kuwa changamoto kubwa kwa sasa ni ukosefu wa safari za moja kwa moja, jambo linalowalazimu watalii wengi kusafiri kwa kubadilisha ndege njiani. Hali hii hupunguza urahisi wa safari na kuathiri ukuaji wa utalii Zanzibar.
Alieleza kuwa kwa sasa serikali ipo katika mazungumzo ya awali na wawekezaji wenye nia ya kushiriki katika mradi huo, kwa lengo la kuanzisha kampuni ya ndege itakayoweza kuwaleta watalii moja kwa moja Zanzibar bila kupitia nchi au miji mingine.
Mpango huo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uchumi wa Zanzibar na kuifanya kuwa kitovu muhimu cha utalii katika ukanda wa Afrika Mashariki.