Makwizi Band
JF-Expert Member
- Aug 19, 2024
- 1,535
- 2,565
Ni assumption tu hiyo. Sasa hivi Marais wote ni Wazanzibari, Zanzibar sasa hvi inapendelewa to the maximum. Hivi ndege za ATC zipo wizara ya muungano? Mbona zinakabidhiwa Zanzibar wakati Wazanzibari hawana mchango wowote kwa ununuzi wa hizo ndege? Waache uvivu; wana uhuru uliopitiliza. Kwanza hebu ngoja kwanza, hivi ni muungano ndio umetaka bongo flavor isipigwe Zanzibar? Unataka kuupeleka utalii mbali zaidi halafu hutaki bongo flavor, stupid...., hivo vitu ni mapacha. Halafu nenda Zanzibar hata leo, lala hotel yoyote Unguja na viunga vyake, angalia idadi ya wafanyakazi wa Kizanzibari, hukuti hata 1, wote wametoka bara. Niliwahi kulala Waikiki hotel, nilimkuta mhudumu 1 wa Kizanzibari, alinishangaza. Baadae nilifanya nae mazungumzo kuhusu wao kutokupenda kufanya kazi hotelini, this is what he told me, "wengi wanasema, kufanya kazi hotelini kuna haribu desturi zetu" nikamuuliza, wewe vipi? This is what he told me again, "mimi nimesomea bara, hata jamaa zangu wananishangaa" nimelala hotel tofauti Unguja, ni huyo tu ndio alikua Mzanzibari, hadi kina dada wanaofanya usafi vyumbani, wote wanatoka bara, majority niliongea nao wanatokea Morogoro.Pengine ni mambo ya muungano
Sasa una jamii ya namna hiyo, ndio unambie eti muungano unaharibu biashara yao ya utalii? Nonsense