Pang Fung Mi
JF-Expert Member
- Nov 10, 2022
- 6,653
- 13,919
Hawa vibwengo watake wasitake Muungano hautavunjika ngoja tunasuburi muda sahihi ufike ndio watajua hawajui.Muungano wa Tanganyika na Zanzibar naumithilisha na ndoa ya baina ya mwanaume (Tanganyika) na Mwanamke (Zanzibar) ambapo mwanaume ndio anaforce mahusiano na mwanamke ikiwa mwanamke hataki kuwa katika hiyo ndoa. Hatima yake sasa ni ndugu wa mume kudhalilishwa na upande wa mwanamke, mwanamke kujiona bora zaidi ya mwanaume.
Huu muungano umekaa kinafiki sana, ni wakati sasa kila mtu akashika hamsini zake tujue ni nchi mbili tofauti tu. Kuliko haya manyanyaso na kudhalilishana kunakofanywa na wazanzibari dhidi ya watanganyika.
Mtanganyika akiwa zanzibar anachukuliwa kama takataka lakini wenyewe huku wanajiachia bila bughudha yeyote.