Zanzibar ni nzuri kwa kuisikia ila ni chafu kwa kuiona

Zanzibar ni nzuri kwa kuisikia ila ni chafu kwa kuiona

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,340
Reaction score
4,659
Kwanza salaam

Unguja na Pemba ndiyo zao la nchi ya Zanzibar ila nitoe exclusion kwa Pemba sijawahi kufika ila unguja/Zanzibar imejawa kila aina ya uchafu licha kuwa watu wake asilimia 90 ni waislamu.

Mifumo ya maji taka ni mibovu hakuna streets chember au mifereji ya maji taka mfano maji ya kuoshea vyombo.

Utupaji wa Taka holela unaweza kukuta mtu anatoka ndani taka mkononi akaitupa nje bila kwenda kutupa sehemu maalumu

  • Hakuna maeneo ya kudumu ya utupaji taka
  • Magari ya ubebaji taka yanachelewa kuchukua taka.

- Shekha wengi wanakula pesa za watu Mfano kuna sehemu inaitwa Mwanyanya niliishi pale zone D aisee yule shekha ni tapeli anapenda pesa kuliko chochote na licha ya kukusanya pesa alikuwa anawazurumu wabebaji taka mpk walishindwa kuja kuchukua taka licha ya kutokuwa kuchukua taka then akawa anakuja kukusanya pesa.

Nchi yenye waislamu wengi lakini kitendo viovu vya kuingilia watoto, ubakaji na udhalilishaji umeenea sana.

Serikali ifanye jitihada zaidi ya kushughulikia hizo changamoto la sivyo akiingia kipindupindu atapindua wengi.

NAWASILISHA.
 
Dunia sio chafu, ni chafu... uchafu ukiutizama

images (97).jpeg
 
So tupinge chafu au tupige vita uislam Kwa kuwa waislam wa Pemba wachaf?. Mbona udinism hapa jf una mizizi ya chuma?
Moderator
YinYang
Comment za kidini ziondoeni mana sioni kama zitaendeleza mjadala nje ya kuleta watu kutukanana humu
Sio kwamba ni Udini ila uislmu umekataza uchafu na maovu.


"Al islamu nadhif fata nadhwafu""
 
Kwanza salaam

Unguja na Pemba ndiyo zao la nchi ya Zanzibar ila nitoe exclusion kwa Pemba sijawahi kufika ila unguja/Zanzibar imejawa kila aina ya uchafu licha kuwa watu wake asilimia 90 ni waislamu.

Mifumo ya maji taka ni mibovu hakuna streets chember au mifereji ya maji taka mfano maji ya kuoshea vyombo.


Utupaji wa Taka holela unaweza kukuta mtu anatoka ndani taka mkononi akaitupa nje bila kwenda kutupa sehemu maalumu

-hakuna maeneo ya kudumu ya utupaji taka
-magari ya ubebaji taka yanachelewa kuchukua taka.
-shekha wengi wanakula pesa za watu Mfano kuna sehemu inaitwa Mwanyanya niliishi pale zone D aisee yule shekha ni tapeli anapenda pesa kuliko chochote na licha ya kukusanya pesa alikuwa anawazurumu wabebaji taka mpk walishindwa kuja kuchukua taka licha ya kutokuwa kuchukua taka then akawa anakuja kukusanya pesa.


Nchi yenye waislamu wengi lakini kitendo viovu vya kuingilia watoto,ubakaji na udhalilishaji umeenea sana.


Serikali ifanye jitihada zaidi ya kushughulikia hizo changamoto la sivyo akiingia kipindupindu atapindua wengi.



NAWASILISHA.
Niseme nn mm zanzibar nzuri ukiwa na hela na uende kama mtalii tu.
Utafurahi sana.
 
This is very sad! Sisi wanadamu katika maisha yetu ya kila siku tuna machaguo mengi (Many choices)ya nini tufanye na nini tusifanye, nini tuseme na nini tusiseme, nani tumseme vizuri na nani tumseme vibaya, na wakati mwingine tunajua wazi kabisa kwamba mtu fulani kwa ujumla ni mtu mzuri au mbaya lakini tunachagua (Making a choice) kusema tofauti na ukweli ... hili chaguo au machaguo tunayoyafanya kila siku katika maisha yetu. Swali ni kwamba kwanini tunafanya machaguo haya? Nini kinatusukuma kufanya maamuzi kama haya, sababu ni nyingi lakini mojawapo ni ujinga (ignorance = lack of knowledge or information)

Mleta mada, kwa makusudi kabisa, kwa sababu anazozijua mwenyewe AMECHAGUA kuainisha 'uchafu' wa watu wa Unguja, (Mfumo wa majitaka, utapeli wa viongozi wa vitongoji, ubakaji, kuwaingilia watoto,) na amekwenda mbali zaidi kwa kusema "Nchi yenye waislamu wengi lakini kitendo viovu vya kuingilia watoto,ubakaji na udhalilishaji umeenea sana". Uislamu unaingiaji hapa!!??? Hii inamaanisha nini? Kwamba ni sawa kwa nchi isiyo na waislamu wengi kuwa chafu? Au wasio wasio waislamu ni wasafi zaidi kuliko walio waislamu - NI UJINGA TU.

Hoja yangu ni kwamba SI HAKI, kutumia mfano wako wa kuishi Area D ya Mwanyanya kama kigezo cha kuhukumu kwamba eti watu wa Unguja ni wachafu na kwamba 'eti wengi ni waislamu. Ni sawa uende Uwanja wa Fisi Tandale au Machinjioni Vingunguti halafu useme watu wa Dar wachafu. SI HAKI kuutumia mfano wa kiongozi mmoja wa kitongoji na kisha kuhukumu kwamba watu wa Unguja ni matapeli.

Mleta mada, hivi unajua kiwango cha 'uchafu', 'utapeli', 'ubakaji' 'changamoto za majitaka', zilizo maeneo mengine ya nchi nje ya Unguja? Au leo umejisikia KUCHAGUA kuizungumzia Unguja.

Namna tunavyochagua nini cha kusema, nani wa kumsema inadhihirisha kiwango chetu cha ujinga (Ignorance) tulichonacho, tuendelee kuombeana tuondokane na ujinga na tupape maarifa na taarifa zaidi kuliko ujinga.
 
Back
Top Bottom