Zanzibar: Rais Magufuli amshangaa Dk. Shein kusaini makaratasi ya mtu aliyekataa mkono wake

Hotuba za Rais MAGUFULI huko Pemba na Unguja ni umwagaji wa petroli kwenye moto unaowaka. Unakuwa mkuu wa nchi na kazi yako ni kuzunguka na kutisha raia, kuchochea na kukoleza moto, kubagua na kukamia. Huna MASULUHISHO ya matatizo ya wananchi zaidi ya vitisho.
 
Kwa hiyo wewe ilitaka ipite tu mizigo ionekane ni mingi imejaa hata kama wanakwepa kodi. Hahahaha. Ukistaajab ya Musa.. sijui utayaona na manyumbu.. huoni kama wale wakwepa kodi wameshindwa biashara wamesepa zao. Hivi unajua idadi ya wafanyabiashara waliokimbia nchi tangu Magufuli aingie. Hivi unajua idadi ya mizigo iliyotelekezwa pale bandarini ambayo ilikuja kwa uongo ili kutumia kodi chache au kukwepa kodi kabisa na imetelekezwa pale. Kamanda kajipange upya
 
Hivi kama ni hotuba umeshawahi zisikia hotuba za Seif ? bora Magu anakoleza moto lakini Seif anakolezaga gesi. Ambayo ikilipuka utaona masizi tu.tuache kudanganya raia. Wananchi wameshazinduka hamuwaongopei tena.
 
Watanzania badala yaa kumchagua Rais mkamchagua baunsa mpigaji push ups...
 
Hilo huyu Mukuru anastahili kukemewa kabisa. Kama watangulizi wake wangekuwa na huruka hii siamini kama hili taifa lingekuwa na amani hii tunayojivunia
 
We unasema nini. Matamshi yapo ya aina mbalimbali. Kama tuliambiwa watuhumiwa wa ufisadi ni wasafi ni mulemule tu. Nyani haoni kundule. Tupo wepesi ku critisize wengine wakati ya kwetu yanatushinda. Tumechoka !liwalo na liwe. Hatudanganyiki kwa sasa. Magufuli aongeze spidi hii haitoshi. Tuko nyuma sana kiuchumi wenzetu wametuacha mbali kule.
 


Unawaza kupita tu hao wabunge wanahoji upunguaji wa mizigo ina maana huo upupu wako hawaujui?

Umefanya yapi mazur kuwavutia watu wafanyebiashara hapo nyie ndo mnadhihirisha unyumbu mkuu wako analia na ufichwaji wa fedha wakat hana anachouza wala kuzalisha wataalamu wanakwambia uchumi unaporomoka nyie mmekalia hayo maupupu yenu mtatafuta hela had uvunguni na kuchampa mpya bila ya kuweka mipango imara ya kukuza uchumi.
 
Inaweza kuwa anafikiri Zanzibar ni Mkoa kama Katavi, mkumbusheni kuwa Zanzibar ni Nchi na haiendeshwi kwa Matamko ya hovyo hovyo.
 
Nahisi safari ya Rais huko Zenj itaharibu utengamano badala ya kujenga. Si kwa kauli kama zile...full mipasho.
 
SAFI SANA TUMEPATA RAIS SAHIHI KWA MUDA SAHIHI
 
Hilo huyu Mukuru anastahili kukemewa kabisa. Kama watangulizi wake wangekuwa na huruka hii siamini kama hili taifa lingekuwa na amani hii tunayojivunia
Tukiongea wapinzani hata mambo ya hatari ni safi. Lakini akionges mwingine ni balaaa. Sielewi hii aina ya siasa.
 
Akili yako ndio imefikia hapo kufikiri,huyo ndiye Rais na matamshi yake yana athari kwa kila mtu bila kujali itikadi yake!Hoja yako ni dhaifu,eti kisa mpinzani Fulani alikosea sehemu basi ni halali kwa Rais kwenda kinyume na sheria na katiba!Mbona mnakuwa wapuuzi kiasi hiki?JPM anamamlaka gani ya kuzuia stahiki za makamu wa Rais mstaafu????????
 
Mungu wa Ikulu huyo yuko busy kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwa Jamii ya Watanzania huku akiwa amejificha mgongoni kwa vyombo vya dola. Eti anataka mshikamano na umoja!

Hivi inawezekana kweli kupata umoja na mshikamano nchini kupitia vitisho dhidi ya raia na wapinzani kila kukicha!? πŸ™

Huyu ni mtaka Shari, fujo, vita ndiyo maana mawazo yake yote yako Rwanda, Somalia,Libya na Iraq.
 
Hivi tunaelekea wapi...? ooh sorry tuko wapi kwanza..? saa hz saa ngapi..!!? πŸ™„πŸ˜•πŸ™„πŸ˜΅πŸ™„πŸ˜•πŸ˜΅
Mkuu kama ni mbuzi basi amefia kwa muuza supu, kama ni gari limeharibikia sekenke. Tuendelee kufunga mkanda tu.
 
Matamshi ya Magu?
Nhuu!
Hata Kinana hawezi tafsiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…