Zanzibar: Rais Mwinyi apandisha Pensheni kwa Wastaafu na Wazee

Zanzibar: Rais Mwinyi apandisha Pensheni kwa Wastaafu na Wazee

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
RAIS DK.MWINYI APANDISHA PENSHENI KWA WASTAAFU NA WAZEE ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itapandisha pensheni kwa wastaafu kwa asilimia mia moja akitolea mfano wa mstaafu wa kima cha chini anayepokea shilingi elfu 90,000/= atapanda mpaka shilingi 180,000/=. Ametekeleza ombi la wastaafu hao walilolitoa mwaka jana .

Ameyasema hayo leo tarehe 01 Mei 2023 katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Skuli ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itapandisha pensheni jamii kwa asilimia mia moja na hamsini kwa Wazee kuanzia miaka 70 ambapo kwa sasa wanaopata elfu ishirini watapanda hadi shilingi elfu hamsini.
Utekelezaji wa mabadiliko hayo utaanza Mwezi Julai mwaka mpya wa bajeti utakapoanza.

Serikali inashukuru kwa namna Wafanyakazi walivyopokea kwa furaha mabadiliko ya mishahara yaliyofanyika.

Vilevile Dk.Mwinyi amesema mipango na mikakati ya Serikali ni kuimarisha uwajibikaji kwa kuzingatia namna ya kuboresha mazingira ya kufanyia kazi yakiwemo mishahara bora na stahiki nyengine za watumishi.

Dk Mwinyi amesema serikali ipo hatua za mwisho za kuanzisha mfumo wa Bima ya afya kwa wafanyakazi wote umma Zanzibar.

Amesema Serikali imepokea ombi la Wafanyakazi kupatiwa fedha za nauli kuwawezesha kwenda kazini na kurudi nyumbani nje ya mishahara yao.

📅 01 Mei 2023

📍Viwanja vya Skuli ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
IMG-20230501-WA0015.jpg
IMG-20230501-WA0019.jpg
IMG-20230501-WA0021.jpg
IMG-20230501-WA0013.jpg
IMG-20230501-WA0012.jpg
IMG-20230501-WA0018.jpg
IMG-20230501-WA0020.jpg
IMG-20230501-WA0010.jpg
IMG-20230501-WA0011.jpg
IMG-20230501-WA0009.jpg
IMG-20230501-WA0014.jpg
IMG-20230501-WA0016.jpg

IMG-20230501-WA0017.jpg
IMG-20230501-WA0008.jpg
 
Haka kanchi (ooh! Samahani Zanzibar siyo nchi) kana hela za kuwalipa hao wastaafu ama ndo kanategemea bara??
 
Faida ya Znz wako wachache, ila wafanya kazi wakiwa wengi huwezi pandisha hivyo
 
Sasa kama wanapewa tu pesa 52 bilioni na bara pesa eti kwa vile kuna Muu.gano kwa nini wasilipe wazee? Kwa nini hii 52 waslpewe hata mkoa wa Geita unaochangia 2 bilioni U S D kila mwaka expoerys Gold? MUUNGANO HUU UNA SHIDA KUBWA SIO KUWA WATU WABARA HAWAONI ILA MDA TU
Hata huku kwetu inawezekana sema wapigaji huishia kuzikwiba tu
 
Huyu alipaswa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
 
Mwinyi anajitahidi, japo naamini anayoyafanya Zanzibar yanachagizwa na uchache wa wastaafu waliopo kule ukilinganisha na Bara, tena zaidi kama hiyo pensheni inawahusu wazee wenye miaka kuanzia sabini.
Kiuchumi uko wrong!!
 
Back
Top Bottom