Zanzibar: Rais Mwinyi apangua Baraza la Mawaziri, aingiza wanne wapya

Zanzibar: Rais Mwinyi apangua Baraza la Mawaziri, aingiza wanne wapya

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869
08 March 2022

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi leo amepangua Baraza la Mawaziri. Ateua mawaziri 4 wapya na wanane wamebadilishwa vituo vya kazi. Pia kwa katika baraza lake, mheshimiwa Rais wa Zanzibar Dr. Hussein Mwinyi ameteuwa kwa mara ya kwanza mawaziri wadogo saba katika serikali yake .
20220308_220226.jpg
20220308_220230.jpg
20220308_220456.jpg

 
Mh. Engineer Zena A. Said katibu wa baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu kiongozi akisoma majina ya baraza la mawaziri la SMZ

 
hivi Zenji HAKUNAGA MKRISTU hata mmoja kwenye serikal ya mapinduzi?
Sawa


Hivi Zanzibar hamnaga Wakristo ee?

Hivi hoja kubwa mliyoiona hapo ni dini/ukristo? Nilijua mtauliza kuhusu uwezo na uadilifu wa walioteuliwa, badala yake mmekimbilia kwenye dini/ukristo..

Hii nchi imejaa wapumbavu.
 
Yaani Zanzibar ni nchi ndogo huenda kieneo ni ndogo kuliko wilaya ya Ngorongoro lakini ina utitiri wa wizara, mawaziri na manaibu waziri.
Sijui wazanzibar tunakwama wapi?
Hiyo nchi ya Zanzibar inapatikana bara gani?
 
Kuna Wakristo wengi tuuu
Kumbe ndio mtindo huu haya tuendeleee
Mwl alisema udini mbaya
 
Kamkoa kanajitutumua..hakuna effect hata kusiwe na baraza..maisha yanaenda tu huko..mana wanakula na kusaza kupitia Tanganyika.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom