Zanzibar: Rais Mwinyi apangua Baraza la Mawaziri, aingiza wanne wapya

Zanzibar: Rais Mwinyi apangua Baraza la Mawaziri, aingiza wanne wapya

Yaani Zanzibar ni nchi ndogo huenda kieneo ni ndogo kuliko wilaya ya Ngorongoro lakini ina utitiri wa wizara, mawaziri na manaibu waziri.
Sijui wazanzibar tunakwama wapi?
Tamaa za madaraka..hivyo visiwa ata akiwepo mwinyi bila hata baraza maisha yanaenda tu.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama Zanzibar wanaweza kugharamia maisha ya utitiri wa viongozi ni sawa. Wasichote kutoka Bara, maana deni la umeme walishindwa kulipa hadi JPM akawasamehe.
 
Huyu naye anahangaika, ka nchi kanalingana na Dsm kanamsumbua kuendesha
 
Hivi hoja kubwa mliyoiona hapo ni dini/ukristo? Nilijua mtauliza kuhusu uwezo na uadilifu wa walioteuliwa, badala yake mmekimbilia kwenye dini/ukristo..

Hii nchi imejaa wapumbavu.
Hata mm nimeshangaa! What is dini? Kuna mambo siyo ya lazima, siyo kila kitu kuna usawa! Tena nisisikie hoja kama hii tena inakera sana. Nadhani nimeeleweka!
 
Yaani Zanzibar ni nchi ndogo huenda kieneo ni ndogo kuliko wilaya ya Ngorongoro lakini ina utitiri wa wizara, mawaziri na manaibu waziri.
Sijui wazanzibar tunakwama wapi?
Kwa vile una familia ndogo chakula chako unapunguza baadhi ya mboga? Kwa mfano, hutoweka nyanya, vitunguu na chumvi kwenye mchuzi wako kwa vile una familia ndogo,
 
Kama Zanzibar wanaweza kugharamia maisha ya utitiri wa viongozi ni sawa. Wasichote kutoka Bara, maana deni la umeme walishindwa kulipa hadi JPM akawasamehe.
Wewe utawezaje kumsamehe mtu unayemdai halafu anakwenda vyombo vya habari anakwambia fanya unavotaka hata kunipeleka polisi wewe nenda tu.

Ukweli ni kwamba kutokana na mkataba, SMZ hawatakiwi kuuziwa umeme bali ni kuchangia gharama tu za uendeshaji. Wengi humu hamujui ila SMZ wana ubia kwenye mtambo wa kuchakachua umeme unaokwenda ZNZ na miundo mbinu wamegharamia wenyewe SMZ.
 
Wajuzi tuelimisheni , mbona press za ikulu huku bara zinatolewa na zuhura yunus lakini ni tofauti na Zanzibar mbona hazitolewi na Charles Hilary?
 
Tunataka tume hulu ya Uchagusi hizi hamlele za kuteuwana na kuzikana ni yao wasitupigie gitaa la kimbuzi,maana namna teusi sinavyofanywa zinakosa hata sehemu ya kuandikwa kwenye magaseti,aisee hivi MaCCM wanaona kujenga nchi ni kufanya teusi asubui na mchana.
Uhitaji wa uchaguzi wa haki bila ya kuonewa wala kuuliwa mtu ndio hitajio la Taifa hili. Hata mchaguliwa kwa kupitia sanduku la kura lililopitia uchaguzi ulio wazi na wa haki basi hata kutembea na utendaji wake wa kazi utakuwa na kifani na sifa kedekede,
Ila hawa waliopita kwa nguvu za polisi na jeshi ,lana ya uchaguzi itawatafuna wakiwa hai ,hata wajenge na kufanya kila kitu bure bado laana ya uchaguzi haiwezi kufutika maana hata kutubu hawajatubu na kuwaomba samahani wapiga kura kwa yaliyotokea ambayo yalifanywa na chama chao,wajitokeze hadharani na kukiri ,watubu na kutuomba wapiga kura samahani.
 
Back
Top Bottom