Zanzibar: Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Vyama vya Upinzani

Zanzibar: Rais Samia akutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Vyama vya Upinzani

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
413
Reaction score
471
Rais Samia ambaye yuko ziarani katika visiwa vya Pemba huko Zanzibar leo amekutana na viongozi wa vyama mbalimbali vya upinzani kwa majadiliano.

Rais Samia amekutana na kuzungumza na viongozi wa Chama cha CUF, ACT-Wazalendo na ADC Kisiwani Pemba.

Wakati fulani hapa Tanzania ilishakuwa ndoto kwa Rais kukutana na viongozi wa upinzani kujadiliana na kuzungumza.

Angalau Rais Samia ameturudisha kwenye utamaduni wetu wa kupendana na kuheshimiana japo tunakinzana kwenye mitizamo na mirengo ya kisiasa

CAT.jpeg
 
Rais Samia anazidi kutuonesha na kutukumbusha umuhimu wa Mama katika kuijenga nchi na amani
 
Mbwembwe tu hizo..ana walambisha asali ili wasipige kelele kuhusuiana na serikali yake.

Katiba mpya ya warioba iwekwe mezani tuanzie hapo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Dunia nzima siasa haiondoi uzalendo wa watu hata Marekani mahali ambapo huwa tunatolea mfano wa nchi iliyokomaa kidemokrasia na kidiplomasia huwezi kukuta democratic au Republican wanatofautiana kwenye masuala yanayohusu maslahi ya taifa.

Kupitia Marekani tunajifunza mengi hata kama tumeruhusu kokosoana lakini katika masuala ya maslahi mapana ya taifa wote tunakuwa kitu kimoja. Huwezi kukuta Marekani vyama vimekaa vinarumbana ujenzi usifanyike wana namna ya kukosoana ambayo ikitumiwa na Afrika itafika mbali.
 
Mama mnamdanganya sana hao anachezea kodi , ila ni ishara kuwa mama ni mtu mwema kura yangu anayo
 
Rais Samia ambaye yuko ziarani katika visiwa vya Pemba huko Zanzibar leo amekutana na viongozi wa vyama mbalimbali vya upinzani kwa majadiliano.

Rais Samia amekutana na kuzungumza na viongozi wa Chama cha CUF, ACT-Wazalendo na ADC Kisiwani Pemba.

Wakati fulani hapa Tanzania ilishakuwa ndoto kwa Rais kukutana na viongozi wa upinzani kujadiliana na kuzungumza.

Angalau Rais Samia ameturudisha kwenye utamaduni wetu wa kupendana na kuheshimiana japo tunakinzana kwenye mitizamo na mirengo ya kisiasa

View attachment 2291883
Kwani corona bado ipo? Naona wako Full Mask
 
Angekuwa JPM angekuwa kawapa hao viongozi kesi za uhujumu uchumi, wangekuwa rumande baada ya kutrkea na kupigwa sana, wengine wangepotezwa, nyumba zao zingevunjwa,kama Wana biashara wote wangefilisilwa, vihela vyao benki vingeibwa na Benki Kuu.

Mazungumzo hu- defuse tension, wengine wanajionaga tembo au Simba wakiwa mbali, ukimleta mezani muongee, unakuta kajaa hewa tu na tabasamu
 
Asali inaendelea kurambwa
Mzee umemiss kauli tata za "kipigo cha mbwa koko" au " kupigwa mpaka wachakae" mie naipenda Zaburi hebu jaribu kusoma Zaburi 133 regardless ya imani yako.
 
Picha ni muhinu kwa ajiri ya kutunza Akidi kwa siku zijazo.

Hiyo ndiyo siasa, mtulie hapo hapo.
 
Back
Top Bottom