Zanzibar 2020 Zanzibar: RVS online TV yafungiwa kwa miezi miwili kwa kutotoa uwiano sawa kwa vyama vya siasa

Zanzibar 2020 Zanzibar: RVS online TV yafungiwa kwa miezi miwili kwa kutotoa uwiano sawa kwa vyama vya siasa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Tume ya Utangazaji Zanzibar imefungia kituo cha RVS Online TV kwa kutoa habari zisizo na uwiano kwa vyama vyote vya siasa na kurusha maudhui yanayoashiria uvunjifu wa amani.

Tume ya Utangazaji imesema ilikiita kituo kiliitwa mara ya kwanza Septemba 9, 2020 ili kujibu hoja za ukiukaji wa mwongozo wa huduma za utangazaji wakati wa uchaguzi 2020.

Tume iliendelea kufuatilia kituo hiko na kubaini kuwa bado hakina uwiano na kilivunja kifungu 5(i) cha muongozo wa Huduma za Utangazaji wakati wa Uchaguzi Zanzibar na Kifungu 14(j) cha maudhui ya mtandaoni ya 2019.

Kwa mamlaka iliyopewa Tume ya Utangazaji Zanzibar imekisimamisha kituo hiko kuanzia Oktoba 21, 2020 hadi Desemba 21, 2020.

1603299534713.png
 
RVS imefungiwa ila KTV imeachwa kisa inarusha habari za CCM na vichwa vya habari vya kizushi?
 
Vyombo vya Habari vitulie kidogo tu mpaka 27/28 tufunge kazi ili vyombo viwe huru
Vyombo vya habari ambavyo haviwezi kupigania uhuru wake vina maana gani kwa wananchi ?

Heri vifungiwe vyote tu havijui hata maana ya uwepo wake
 
Mimi source yangu ya Habari za Visiwani ni WEYANI wako vizuri
Na mimi sasa ivi ndio natizama hio, nimeachana na KTV kwanza wanaweka vichwa vya habari vya kizushi, pili walikuwa hawaweki kampeni za upinzani. Kwa uchawi wa hio tume ya utangazaji mara nayo wataifungia.
 
Soma upepo, Wakurugenzi wa Halmashauri ambao ndio Wasimamizi wa uchaguzi Wamenyooka
Mpango wao wa wizi hatimae umeanikwa hadharani


Continue to sleep, by the time you wake up you will know who's in charge.
 
Vyombo vya Habari vikiwa Goigoi kama Tanzanite toilet papers ujue tumekwisha
Mimi naona hatuna sababu hata ya kuvipigania.

Vyenyewe haviwezi kujipigania and yet vinashindwa hata kutangaza agenda za vyama vya upinzani
 
Mimi naona hatuna sababu hata ya kuvipigania.

Vyenyewe haviwezi kujipigania and yet vinashindwa hata kutangaza agenda za vyama vya upinzani
Vimetengenezewa utitiri wa Sheria za kuvibana hata vikijikuna vinaambiwa vimevunja Sheria hatuna budi kuvipigania
 
Back
Top Bottom