Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si ndio mie uliye ni quote mkuu au?Ungemuuliza niliyem_quote.
Mrangi banaHuyu mwenyewe anapiga vitu
Ova
Na kitimoto wanakula sanaZenji pombe inanywika sana
Ova
Namjuwa vzr,ni member pia wa club moja maarufu hapa darMrangi bana
Dili sana huko ukiingiza tu lazima uuze yoteNa kitimoto wanakula sana
Zenj wanafiki wa kifini wengi sana.Hujamuelewa vizur, Mh Simai ana exposure kubwa sana maana ameishi sana nchi za Ulaya alafu hana njaa na sio mnafiki tofauti na mawazir wengine wa SMZ mm naona yeye ameipigania sana sekta ya utalii na hakuwa tayar kuona utalii Zanzibar unayumbishwa sasa kwa jinsi inavyoonekana Kuna baadhi ya taasis hapo Zanzibar mfano hiyo bodi ya vileo wanamkwamisha katika kazi yake maana hiyo bodi inaendekeza sana mambo ya dini na huko nyuma wameshafungia bar na kumbi nyingi za starehe zanzibar kwahiyo Mh Wazir kaona isiwe taabu aachie ngazi maana huwezi ukawa unataka kukuza utalii alafu unawa limit watalii kwenye starehe zao, Saudia kwenyewe yalipo makao makuu ya Kobaz wote duniani juzi wametangaza pombe kuanza kuuzwa wewe kizimkazi ni nani uwashughulishe watu na starehe zao.
Tatizo Wazanzibari wanata viziwa viwe islamic states. Mahoteli ya kitalii yawepo lakini watalii wasitumie kilevi chochote wakiwa visiwani.Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Simai Mohamed Said ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo leo usiku.
Mhe. Simai ambaye pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, ametangaza kujiuzulu akisema ni kutokana na kile alichokiita "MAmazingira yasiyo rafiki ya kazi."
---
Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said amemuandikia Rais Dkt. Hussein Mwinyi barua ya kujiuzulu nafasi hiyo.
“Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu. Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni.
Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni.” - sehemu ya taarifa yake ya kujiuzulu
Siku mbili zilizopita, Januari 24 Waziri huyo mwenye dhamana ya Utalii alitangaza uhaba wa pombe katika hotel na migahawa
“masikitiko yamekuwa makubwa na imenibidi niitishe kikao kwa sababu nimeanza kunyooshewa mkono na Wadau, mimi kama Baba wa Mahoteli na Migahawa lazima nionane nao kwani Sekta ya utalii si vyema ikachezewachezewa”
“Tumeona maamuzi ya Bodi ya Vileo Zanzibar imewaondosha wale waliokua wanahusika kama ZMMI, Scoch na One Stop, nimeanza kuona athari hoteli nyingi wameanza kukosa huduma ya Vinywaji baada ya Bodi ya Vileo kufanya maamuzi hayo, niwaombe Wawekezaji waendelee kuwa Wavumilivu wakati huu ikitazamwa namna ya kutatua jambo hili”
Mwisho wa kunukuu.
Zaidi soma Waziri: Zanzibar inakabiliwa na upungufu wa Pombe kwenye Mahoteli