Wakuu nimeona nichangie kidogo kwa vile mimi ni mzaliwa na mkaazi wa Unguja
Nimesoma coment nyingi ila nimeona baadhi ya watu hawajui Zanzibar ni muunganiko wa vusiwa viwili UNGUJA NA PEMBA
Mostly watu wa bara wanapoesama Zanzibar huwa wanakusudia Unguja sababu ndio kisiwa baba kati ya hivo viwiwili
Wakuu suala la viwanja hakuna sheria inayomkataza mtanganyika kumiliki kiwanja, mie binafsi nimeuziwa kiwanja na mtanganyika na ndio yalipo makaazi yangu mpaka muda huu naandika
Maeneo mazuri kwa kununua kiwanja kwa sasa ni KISAUNI, MAUNGANI, FUONI, MWERA, KIANGA, KIJICHI
Kiwanja cha wastan wa nymba na fensi kwa maeneo tajwa hapo ni around 8m- 20m
Mkuu mmoja amegusia kuhusu ubinafi/ubaguzi akatolea mfano kukodi chumba ngumu kama ni mtu wa bara. Mkuu hapana sio kweli, Unguja anaejenga kwa ajili ya kukodisha basi taget yake ni watu wa bara sababu waZanzibar hawana utamaduni wa kukodi na wazazi hawaruhusu watoto wao kukodi, wakati mwengine hata baada ya kuoa still atakaa nae kwakwe mpaka atakapopata makazi yake.
Gharama za maisha ni juu kidogo kulinganisha na bara sababu kubwa ni kua zanzibar hakuna kilimo
90% ya mazao(chakula) zanzibar ni import kutoka bara(mikoani) mf mchele maharage kunde mtama nk
Maji ya 1.5lt dar 500 Unguja 1000
Umeme dar ni nafuu unit kulioko Unguja hii ni kutokana na kua Unguja wananunua umeme kutoka bara, na mengineyo
Guest zipo zote Za kilocal na za VIP (kuna guest mpaka za gorofa) bei sina hakika nazo mtanisamehe bure
Mimi ni mfanya biashara mdogo sana ambae biashara yangu inatekemea pande zote mbili (bara na Zanzibar) hua nasafiri kuja dar mostly mara mbili kwa mwezi
Kama unaplan ya kutalii ZANZIBAR kua huru kuniuliza chochote
Tusipromote chuki hasa jambo ambalo unaliskia tu hujawai shuhudia.
Shukran