Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
TAARIFA KWA UMMA
TUNAITAKA SERIKALI KULIFANYIA MABADILIKO MAKUBWA JESHI LA POLISI, KIMUUNDO NA KIUTENDAJI
ACT Wazalendo tunalaani vikali mauaji haya ya kikatili, na tunalitaka Jeshi la Polisi Zanzibar kuchukua hatua za haraka za kuhakikisha wanawakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria askari wao ambao wamefanya unyama huu wa kukatisha uhai wa watu na kujeruhi wengine eti kutokana na kesi ya uchimbaji wa mchanga. Kwa vyovyote vile, suala la kukatisha uhai wa watu haliwezi kuwa ndio njia ya uzuiaji wa uchimbaji wa mchanga.
ACT Wazalendo tunaamini kwamba kitendo hiki cha mauaji kilichofanywa na Jeshi la Polisi Zanzibar, na matukio mengine kama haya ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni kwa kulihusisha Jeshi la Polisi Zanzibar hayaoneshi taaswira njema kwa nchi na yanatia wasiwasi na mashaka kwa wananchi wa Zanzibar juu ya utendaji na weledi wa Jeshi la Polisi. Kwa hivyo basi, Chama cha ACT Wazalendo tunalitaka Jeshi la Polisi kufanya mambo yafuatayo:-
1. Kutoka hadharani na kuwapa Wazanzibari taarifa ya kina kuhusiana na mauaji haya ya kikatili yaliyofanyika jana Jumamosi tarehe 09/11/2024, na lieleze ni hatua gani zimeanza kuchukuliwa kwa watendaji wake ambao, wamefanya ukatili huu.
2. Liwaeleze Wazanzibari, ni hatua gani wameanza kuchukua kutokana na matukio ya mauaji ya hivi karibuni ambayo yamefanyika katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
3. Kwa upande mwengine, tunaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano kutekeleza haraka mapendekezo ya Tume iliyoiunda kuchunguza mfumo wa haki jinai nchini.
ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kulifumua Jeshi la Polisi na kulifanyia mabadiliko makubwa kimuundo na kiutendaji kwa kuliondosha jeshi hilo katika utendaji wa Police Force kama lilivyo sasa na kuwa Police Service ili kurejesha heshima na hadhi yake ambayo tayari imepotea kwa wananchi wengi kutokuwa na imani na utendaji wa Jeshi hilo.
Imetolewa leo, tarehe 10/11/2024 na,
Hamad Mussa Yussuf,
Msemaji wa Ofisi, Kamati ya Wasemaji wa Kisekta - Zanzibar
Pia soma:
~ Kiongozi wa Mtaa akielezea tukio la Vijana waliodaiwa kupigwa risasi na Askari Zanzibar
~ Jeshi la Polisi kuunda Tume kuchunguza ajali iliyoua vijana wanaosemekana kuuliwa na polisi kutokana na kesi ya uchimbaji mchanga