Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Nimeshangaa sana kiongozi mkubwa kutumia fedha kufanya ushawishi na kampeni wakati huo huo ulikuwa na nafasi ya kubadilisha maisha ya hao wanaopokea fedha hiyo kwa kuandaa mazingira rafiki ili uchumi wao uweze kukua! Fedha hiyo ingetumika kujenga masoko mazuri na miundombinu bora ili kina mama wauze samaki zao bila shida yoyote ingekuwa na manufaa zaidi kuliko kutumia fedha hiyo kufanya "Cheap Politics".
"Nipo Mgogoni, kwa Mama Samia Suluhu Hassan, nimekuja kuchukua msaada, lakini nimefungua bahasha nimekuta shilingi 5,000, hata haijafikia nauli niliyotumia kufika hapa. Kweli sijaitwa lakini nilipata taarifa kutoka kwa waliombiwa pelekeni ujumbe kwa wenzenu waje kupata msaada. Bora wangetuacha majumbani kwetu wasingeleta hata hiyo taarifa! Elfu tano mama Samia Suluhu Hassan, kweli ungewapa wafanyakazi wako?" Amesikika mama huyo kwenye video.
Pia soma: Aliyerekodi video akieleza amepewa bahasha yenye Tsh. 5,000 huko Kizimkazi asibughuziwe, kama mamlaka zina ushahidi kadanganya waseme
RC Amour: Rais Samia hahusiki na sadaka ya Tsh. 5000 Pemba, ni upotoshaji