Nimeshangaa sana kiongozi mkubwa kutumia fedha kufanya ushawishi na kampeni wakati huo huo ulikuwa na nafasi ya kubadilisha maisha ya hao wanaopokea fedha hiyo kwa kuandaa mazingira rafiki ili uchumi wao uweze kukua! Fedha hiyo ingetumika kujenga masoko mazuri na miundombinu bora ili kina mama wauze samaki zao bila shida yoyote ingekuwa na manufaa zaidi kuliko kutumia fedha hiyo kufanya "Cheap Politics".
Your browser is not able to display this video.
"Nipo Mgogoni, kwa Mama Samia Suluhu Hassan, nimekuja kuchukua msaada, lakini nimefungua bahasha nimekuta shilingi 5,000, hata haijafikia nauli niliyotumia kufika hapa. Kweli sijaitwa lakini nilipata taarifa kutoka kwa waliombiwa pelekeni ujumbe kwa wenzenu waje kupata msaada. Bora wangetuacha majumbani kwetu wasingeleta hata hiyo taarifa! Elfu tano mama Samia Suluhu Hassan, kweli ungewapa wafanyakazi wako?" Amesikika mama huyo kwenye video.
Dola inatukosea Sana watz!!MTU kama kashindwa SI mwambieni.akae pembeni TU kistaarabu!!?
Ujinga huu,jamhuri inaaibika kabisa kama hiki ndicho kilichotokea maana yake vetting ilifeli,ujasusi was kiuongozi umefeli Sasa nyie kama Dola mmefaulu nini kumpa huyu anaefanya haya!!?
Tumepiga hatua kubwa sana kiuchumi.
Kwanza ilikuwa ni CHUMVI,MCHE WA SABUNI.
Kila nikipita barabarani kila baada ya magari manne linalofuata ni NUMBER E,hivyo anayedai kuwa sisi ni masikini huyo ana lake jambo labda AHAMIE BURUNDI.
Sasa kutoka kwenye kupewa CHUMVI,MCHE WA SABUNI sasa hivi ni 5K!
MAKOFI TAFADHARI!!!!πππππππ
Tuko mfungoni lkn tunashuhudia maajabu na ulaghai sasa mfungo ukiisha sijui itakuwaje!!
Teuzi za kulazimisha ushindi kinguvu alafu mtu anajinasib na 4 Ara huku rushwa zinamwagwa na maigizo kibaoo!!