Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 2,536
- 7,194
Wakuu,
Wanachama zaidi ya 200 wakiwemo viongozi 28, watangaza kujivua uanachama CHADEMA Zanzibar, wakilalamikia kile walichokiita ukandamizaji na upotevu wa mwelekeo ndani ya chama hicho.
Uamuzi huo umetangazwa mbele ya waandishi wa habari na Atafat Hamad Ali, aliyekuwa Katibu wa Baraza la Vijana wa CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Magharibi B, ambaye pia alikuwa mjumbe wa Baraza Kuu la chama.
"Tumeamua kujivua uanachama kutokana na ukandamizaji mkubwa, ubaguzi na kukosekana kwa mwelekeo ndani ya chama. CHADEMA kimepoteza dira, na hatuoni tena sababu ya kuendelea kuwa sehemu ya chama hiki," amesema Atafat.
Kwa upande wake, Muslim Khamis Rajab, aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mjini Magharibi, amesema wamechukua hatua hiyo kwa sababu chama kimeshindwa kutimiza matarajio ya Watanzania waliokuwa wakiamini katika harakati za mabadiliko.
"Ndoto za Watanzania zimekwama kutokana na siasa chafu na uongozi usiojali misingi ya demokrasia. Tumepoteza imani na mwelekeo wa chama hiki," amesema Muslim.