Zanzibar wanaongezwa mishahara halafu sisi Watanganyika TUCTA inasema hatuhitaji mshahara kupanda. Kwa mantiki hii najitoa CWT

nyinyi wezi mlichoma vituo vya mwendokasi na kuharibu mali za watu tunaenda kukarabati miundo mbinu na kulipa fidia kwa waliopoteza mali zao
 
Yaani mimi na diploma yangu ya ualimu unaniita mwizi?
 
Mafuta yamepanda bei. Maisha yamekuwa ghali.

Wazanzibari wanaongezwa mshahara Watanganyika tunaambiwa eti pesa zilitumika kwenye uchaguzi na nyingine zitatumika kwenye kukarabati uharibifu uliofanywa na Gen Z waliotaka kupindua nchi.

Jumatatu najaza fomu na kujitoa CWT.
Uzuri n kwamba ata hyo fomu ukiijaza hautatoka cwt badala yake itaenda kutupwa tu
 
Rais wa TUCTA alitakiwa amshauri Rais namna bora ya kupunguza mfumuko wa bei kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza.

Kusema hawana sababu ya kuomba kuongezewa mshahara na huu mfumuko wa bei na nauli, hakuwezi kuwa na unafui kwa wafanyakazi. Na hata maana halisi ya Mei Mosi inapotea.
 
Zanzibar na Tanganyika ni mataifa mawili tofauti, labda nyie mmechelewa kujua au pengine kukubali, mimi nilishanya utafiti na ulinganifu wangu kwa kina na kuhitimisha huu sio muungano ni utapeli.

Ila kwa sasa Tanganyika ni koloni la Zanzibar, na hiyo isikushangaze ufahamu tu mwaka 2024 Zanzibar walianza kulipwa 50,000 kwa watumishi wa umma kama posho ya usafiri.
images (70).jpeg
Zanzibar hiyo hiyo huduma ya kufanya usafi wa damu kwenye figo [haemodialysis]ni bure ila kwa Tanganyika mtu anatakiwa kulipa 350,000 hadi 400,000 na utajiuliza inawezekana vipi na wakati mikopo na madeni yanachukuliwa na kulipwa kwa kivuli cha muungano.

Tundu Lissu alikua mbele ya muda sana kuhusu huu muungano kuna siku tutamkumbuka.

View: https://youtu.be/hsNMiqFLPVU?si=de-wl484aYJ2XbDc
 
Dada n kaka wanatumia kodi z tanganyika kuwapa ongezeko wazenji wenzao. Mcheza kwao hutunzwa.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Ukiona mshahara mdogo, Fanya kazi kulingana na mshahara unao lipwa.

Tanzania haijawai mkumbuka Mfanyakazi bora.
 
Nyie wajinga na wapumbavu kwani mtawafanya nini
 
Acha kututukana
Mkuu umeanzisha uzi huu, nakushauri ujishushe ili busara iweze kutawala.

Hao wa 'acha kazi' na 'toilet paper' waweza kuta wana mantiki, sema labda namna walivyotumia uwasilishaji wa kauli zao humu!

Tukianza na huyu wa 'acha kazi', ana maana kwamba, kama unaona kuna uzinguaji wa kimaslahi katika kazi husika ambayo ndiyo yenye chama cha walimu, ni bora kuacha kazi ili kujiepusha na ukandamizaji pamoja na dhulma ili kuweza kupata haki na stahiki zako.

Kusema ujiondoe kwenye CWT inayowapa pesa mafisadi, siyo rahisi, sana sana utaishia kuonywa, kuandamwa ama kufukuzwa, lazima fitina utapambana nazo tu.

Tukija kwenye 'toilet paper", maana yake ni kwamba, umuhimu wenu huonekana tu kwenye kipindi cha uchaguzi kwa namna mnavyotumia wanafunzi pamoja na rafu zingine kukisaidia chama Ccm kushinda.

Baada ya hapo ni kama hivi, hakuna anayewatetea wala kuwakumbuka katika maslahi yenu.

Kwa hiyo mkuu, pokea kila neno kwa unyenyekevu bila jazba, waTanganyika washajichokea na siasa za uongo za nchi hii ujue.
 
Toa upuuzi wako
 
MWEZI WA KUMI WATUMISHI WALISEMA TUNATIKI ,MITANO TENA.SAIZI WANALIA TAFSIRI YAKE HAWAJITAMBUI ,VIONGOZI WAKE WAMEJIEGEMEZA KWA GENGE LA CCM NA KUHISI KWAMBA NI SEHEMU YA CCM KUMBE WAO SIO SEHEMU HIYO ,WANATAKIWA KUWA KATIKATI
 
Mafuta yamepanda bei. Maisha yamekuwa ghali.

Wazanzibari wanaongezwa mshahara Watanganyika tunaambiwa eti pesa zilitumika kwenye uchaguzi na nyingine zitatumika kwenye kukarabati uharibifu uliofanywa na Gen Z waliotaka kupindua nchi.

Jumatatu najaza fomu na kujitoa CWT.
Uzeni Kangala
 
TUCTA imeturudisha kwenye enzi za chama kimoja na kuwa Juwata kama ilivyo UVCCM tu.
 
Back
Top Bottom