Zanzibar wanatumia mpira wa miguu kunung'unika.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nadhani kuna tatizo la Zanzibar ndani ya muungano hata kama ni hairuhusiwi watu kusema hivi.
Sijui tunamsubiri nani aje kututatulia shida hii.

Nilikuwa ninafuatilia mashindano ya CECAFA kikamilifu yaliyomalizikia kwa Kenya kutwaa kombe na Zanzibar kuwa mshindi wa pili. Mimi nilikuwa nikishangilia timu zote za nyumbani Kilimanjaro na Zanzibar zinazoshiriki michuano ile. Baada ya Kili kutolewa nikahamia kikamilifu Zanzibar.

Lakini kilichokuwa kinanishangaza ni kuona watu wa Zanzibar wakiishabikia timu ya Zanzibar kama timu inayotoka Zanzibar pekee sio Tanzania. Hakuna pahala popote mashabiki na viongozi wa Zanzibar walikuwa wanaiona timu ya Zanzibar kama timu inayotoka Tanzania. Yaani Zanzibar ipo, inaweza na inatakiwa kuwepo.

Timu ya Zanzibar kufanya vizuri kwenye mashindano yale ilikuwa kama kilinge cha kuikweza Zanzibar kama Zanzibar kimataifa na sio Zanzibar ya Tanzania.

Kuna kitu watanzania tunatakiwa tukifanye sisi wenyewe kwa hiari yetu, uwazi na maelewano ili wazanzibari walidhike na waache kutafuta njia mbadala za kunung'unikia kama inavyofanyika sasa.

Hata kama tukijifanya ionekane kuwa hakuna tatizo tutaendelea kujidanganya sisi wewe, tatizo lipo bhana, na wakati ni huu wa kulitatua.
 
Walioonekana kufanya hivyo ni asilimia ngapi ya mashabiki wote? Na ulijuaje kwamba wote walioshabikia hivyo ni Wazanzibari? Na hata kama washabiki wote hao ni Wazanzibari, wao ni asilimia ngapi ya Wazanzibari wote?
 
Huo ndio ukweli wazanzibari kwa Muungano huu hawautaki wala hawatakubaliana nao maisha. Hebu wewe Jiulize Shirika la Soka la Hapo Bara (Tanganyika) wao ndio wanaojulikana FIFA. Kama ujuavyo kuna mgao wa Fedha kutoka FIFA ambazo hutengwa kwa ajili ya kuendeleza soka kwa nchi wanachama (Nakumbuka mwaka 2016 Walipewa 10 Bill. Tsh). Zanazibar wao hupewa kiasi gani? Pale wazanzibari wanaposema Tanzania ndio ile ile Tanganyika imejibadilisha jina huwa hawatanii wanamaanisha hivyo hivyo.
 
Kwanza HONGERA kwa vijana chipukizi kufika fainali na kutolewa kwa penalt!!! mengine ni mitazamo tu......
Kwani maisha ktk nyumba aliyopo MAMA wa kambo... maneno na kusengenyana hayatokwisha bhana... kawaida tusonge mbele!
 
CCM waachieni Zanzibar waende zao....na wote wanaoishi Tanganyika tunawarudisha kwao sidhani kama watatosha kwenye vile visiwa..malori ya Bakhresa yatafute barabara nyingine..maboti yaende Pemba.TV akaonyeshe ligi yao..wauza maduka kariakoo fukuza..nyumba zao zivunjwe,.
 
Una hakika wewe ni wa Tanganyika?
 
Kuna chuki Zanzibar zinazo pandikizwa Sana na wanao jiita wapemba.
Wapemba wengi ukiwa nao stori zao nyingi au mazungumzo ya ni Kuna Zanzibar kujitenga alafu wanapenda kujitenga Sana.
Hili swala ni kweli.
Wapemba acheni kupandikiza chuki nchini wote ni ndugu na muungano wote ni wetu
 
Walioonekana kufanya hivyo ni asilimia ngapi ya mashabiki wote? Na ulijuaje kwamba wote walioshabikia hivyo ni Wazanzibari? Na hata kama washabiki wote hao ni Wazanzibari, wao ni asilimia ngapi ya Wazanzibari wote?
Umeanza ubishi.Mambo yaliyo dhahiri unataka yashindiliwe masikioni mwako kama mpunga unakobolewa?Mjifunze kuukubali ukweli.
 
Kwanza HONGERA kwa vijana chipukizi kufika fainali na kutolewa kwa penalt!!! mengine ni mitazamo tu......
Kwani maisha ktk nyumba aliyopo MAMA wa kambo... maneno na kusengenyana hayatokwisha bhana... kawaida tusonge mbele!
Huko ni kutia pamba msikioni ili usisikie usioyapenda. Ukweli unaujua fika Wazanzibar wanalzimishwa tu kwenye huu Muungano.
 
Mimi nilisikia kuna clip wanatuita sisi Watanganyika ni "machogo" sasa sijaelewa wa namaanisha nini?
 
Mtazamo wako c mbaya
 
Tukiwarudisha Watanganyika wanaoishi kule vitatutosha. Bakharesa atafanya Biashara nyengine, unafikiri tutauza nchi kwa kuangalia Bakharesa?
Kwanza hamuwezi kunfukuza Bakhresa, yule ndio mlipa kodi mkubwa kwa Tanzania sio wale wauza dawa za mende
 
Sisi Wazanzibari wao Watanganyika. Baadae wataanza sisi Wapemba wao Waunguja.

Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana.
 
Sisi Wazanzibari wao Watanganyika. Baadae wataanza sisi Wapemba wao Waunguja.

Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana.
Sisi wasukuma wao wakwere, sisi wazaramo wao wachagga, sisi wahaya wao wagogo, sisi wa kaskanizi wao wa Magharibi. Yale yalee!! ngoma draw
 
Nadhani kwenye hili shida sio wapemba ni wazanzibar. Wote walikubaliana wafanye mchakato wa kuirejesha zanzibar huru. Hii inadhibitishwa na uundwaji wa serikali ya pamoja kati ya CCM Zanzibar na CUF chini ya Maalim na Karume, jr., uandikaji wa katiba mpya, bendera na wimbo wa Zanzibar, OIC, kujiunga CAF. Yote haya yalipokuwa yakitokea walikuwa wamoja kwa pamoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…