Zanzibar wanatumia mpira wa miguu kunung'unika.

Zanzibar wanatumia mpira wa miguu kunung'unika.

Kuna chuki Zanzibar zinazo pandikizwa Sana na wanao jiita wapemba.
Wapemba wengi ukiwa nao stori zao nyingi au mazungumzo ya ni Kuna Zanzibar kujitenga alafu wanapenda kujitenga Sana.
Hili swala ni kweli.
Wapemba acheni kupandikiza chuki nchini wote ni ndugu na muungano wote ni wetu
Hakuna Mpemba hata mmoja anayepandikiza chuki hapa. Tatizo wenzetu Tanganyika (sisemi ni wote) mumegeuka mbuni, munahisi mikisha kujificha kichwa basi kwa vile wewe hutoaki kuyaona matatizo basi hakuna anyeyaona.
Muungano huu unamatatizo tokea kuanzishwa kwake. Wapeni watu Uhuru waujadili, na wanapoona panakaso parekebishwe. Vyenginevyo watakuja vijana wengine sisi Hatupo, watafanya wanavyotaka wao.
 
wewe una kaa wapi,ujue wanayo yaongea kila siku.hata siku moja utapata maongezi mengine wao ni kudili na kujitenga sio la kusimiliwa,tembelea sana maeneo ya ilala,magomeni nzima na sehemu kubwa wanapo ishi.ujue chuki zina toka kwa hawa mda wote
 
Huo ndio ukweli wazanzibari kwa Muungano huu hawautaki wala hawatakubaliana nao maisha. Hebu wewe Jiulize Shirika la Soka la Hapo Bara (Tanganyika) wao ndio wanaojulikana FIFA. Kama ujuavyo kuna mgao wa Fedha kutoka FIFA ambazo hutengwa kwa ajili ya kuendeleza soka kwa nchi wanachama (Nakumbuka mwaka 2016 Walipewa 10 Bill. Tsh). Zanazibar wao hupewa kiasi gani? Pale wazanzibari wanaposema Tanzania ndio ile ile Tanganyika imejibadilisha jina huwa hawatanii wanamaanisha hivyo hivyo.
Walipewa4%.
 
Kwani na nyinyi si mlienda na timu yenu? Sasa mnataka mlazimishe kwamba na Zanzibar inawawakilisha nyinyi? Yaleyale yakulazimisha kila cha Zanzibar ni cha Tanganyika
Kumbe hata ilo kombe tungelipata mungesema ni la muungano, bora tulivolikosa kumbe
 
Nadhani kuna tatizo la Zanzibar ndani ya muungano hata kama ni hairuhusiwi watu kusema hivi.
Sijui tunamsubiri nani aje kututatulia shida hii.

Nilikuwa ninafuatilia mashindano ya CECAFA kikamilifu yaliyomalizikia kwa Kenya kutwaa kombe na Zanzibar kuwa mshindi wa pili. Mimi nilikuwa nikishangilia timu zote za nyumbani Kilimanjaro na Zanzibar zinazoshiriki michuano ile. Baada ya Kili kutolewa nikahamia kikamilifu Zanzibar.

Lakini kilichokuwa kinanishangaza ni kuona watu wa Zanzibar wakiishabikia timu ya Zanzibar kama timu inayotoka Zanzibar pekee sio Tanzania. Hakuna pahala popote mashabiki na viongozi wa Zanzibar walikuwa wanaiona timu ya Zanzibar kama timu inayotoka Tanzania. Yaani Zanzibar ipo, inaweza na inatakiwa kuwepo.

Timu ya Zanzibar kufanya vizuri kwenye mashindano yale ilikuwa kama kilinge cha kuikweza Zanzibar kama Zanzibar kimataifa na sio Zanzibar ya Tanzania.

Kuna kitu watanzania tunatakiwa tukifanye sisi wenyewe kwa hiari yetu, uwazi na maelewano ili wazanzibari walidhike na waache kutafuta njia mbadala za kunung'unikia kama inavyofanyika sasa.

Hata kama tukijifanya ionekane kuwa hakuna tatizo tutaendelea kujidanganya sisi wewe, tatizo lipo bhana, na wakati ni huu wa kulitatua.

Unanikumbusha ujinga nilio uona bunge la katiba...
 
wewe una kaa wapi,ujue wanayo yaongea kila siku.hata siku moja utapata maongezi mengine wao ni kudili na kujitenga sio la kusimiliwa,tembelea sana maeneo ya ilala,magomeni nzima na sehemu kubwa wanapo ishi.ujue chuki zina toka kwa hawa mda wote
Kama ni Chuki, wewe ndio unasambaza Chuki wewe Umesikia wapi kabila la Wapemba na na Waunguja? Hapa hapana Mpemba na Unguja kuna Wazanzibari tu. Na Huko Unguja kuna watu ambao hawaupendi huo Muuitao Muungano kuliko huko Pemba.
Hata kama wanaonesha chuki lazima muwaelewe, Nyinyi tunawasikia Kila siku hapa mukilalamika kuwa kuna wanyaruanda wanapandikizwa kwenye Jeshi na sehemu nyengi nyeti. Sasa imagine Mtu alietawaliwa kwa almost 53 Yrs, hawezi kujiamulia anavyotaka mwenyewe aseme nini?
 
Mimi nilisikia kuna clip wanatuita sisi Watanganyika ni "machogo" sasa sijaelewa wa namaanisha nini?
Ni kweli hapo zamani waliitwa wa Tanganyika vichogo nadhan (samahani lakini) kuna kabila watu wake wengi huenda Zanzibar kulima sasa hua wnavichogo na ndomana watu wakadhani watanganyika wote vichogo.Ni kama vile tu wanavyoitwa wao wala urojo na ubuyu sababu kuna watu huko Zanzibar wanapenda ubuyu.Lakini cha msingi kichogo ni kitu kinacho onekana wewe kaa Kariakoo kisha cheki wenye vichogo kama hukuwaona hawa wazanzibari itakua wanafanya makosa makubwa kukosoa maumbile ya mungu
 
Sisi kwetu Tabora misibani na harusini ndio utajua kama kuna mgawanyiko kwenye familia , maana hata uliaji kama mliaji analia huku akipeleka message kwa anaemdhania ndie alie mdhuru nduguye utamsikia tu na anavolia ki mansyete mansyete .... mwanywezi origina wanajua mansyete ninayo maanisha , so kilichotokea kwa ndugu zetu ni mansyete ambayo yatasaidia sana kwa wanaohusika na muugano sio vizuri kufumbia macho mambo yenye ku alert jambo.. my opinion
 
Kama ni Chuki, wewe ndio unasambaza Chuki wewe Umesikia wapi kabila la Wapemba na na Waunguja? Hapa hapana Mpemba na Unguja kuna Wazanzibari tu. Na Huko Unguja kuna watu ambao hawaupendi huo Muuitao Muungano kuliko huko Pemba.
Hata kama wanaonesha chuki lazima muwaelewe, Nyinyi tunawasikia Kila siku hapa mukilalamika kuwa kuna wanyaruanda wanapandikizwa kwenye Jeshi na sehemu nyengi nyeti. Sasa imagine Mtu alietawaliwa kwa almost 53 Yrs, hawezi kujiamulia anavyotaka mwenyewe aseme nini?
Nafikiri wewe mwenyewe uliona Bunge la katiba, Warioba alisema katika jambo ambalo Wazanzibari hawatofautiani (Wako wamoja) ni siala la Zanzibar kuwa nchi kamili. Lakini mukaona ni wapumbavu mukaja na Katiba yenu Mfukoni . Sitta alipigisha kura mpaka Marehemu alimradi lenu liwe tu. Yuko wapi sasa Huyo Sitta?
 
Sisi Wazanzibari wao Watanganyika. Baadae wataanza sisi Wapemba wao Waunguja.

Dhambi ya ubaguzi ni mbaya sana.
Hayo ndo mambo yenu Wabara, Zanzibar ipo kabla ya Tanzania na insha Allah itaendelea kuwepo baada ya Tanzania kwanini mnaing'ang'ania Tushasema zaidi ya mara Alfuu hatutaki tuachieni nchi yetu. Mnabaki kusema znz sisi wamoja, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, mukitubagua sisi na nyie mtabaguana. Ebu iacheni Zanzibar yetu tuwe nchi Jirani. Kwa sababu mnaendelea kuing'ang'ania popote tutakapopata fursa iwe kwenye soka, msiba, harusi na chengine chochote tuta express feeling zetu kwamba hatukubaliani na MUUNGANO huu
 
Naona Tumkey umetoa maneno makali na yenye hisia kali sana. Kwani ni lazima uungane nao Zenji? unashida na ardhi haikutoshi? Unafikiria hata kuchoma maduka yao na kuwafukuza wakikataa kuendelea kuungana na wewe hayo ni maneno hatarishi kwa amani yetu adhimu na adimu epukana nayo.
 
Walioonekana kufanya hivyo ni asilimia ngapi ya mashabiki wote? Na ulijuaje kwamba wote walioshabikia hivyo ni Wazanzibari? Na hata kama washabiki wote hao ni Wazanzibari, wao ni asilimia ngapi ya Wazanzibari wote?
Tafuta video za mapokezi ya timu ya zanzibar ndio utajua, kama ni washabiki au wazalendo
 
wewe una kaa wapi,ujue wanayo yaongea kila siku.hata siku moja utapata maongezi mengine wao ni kudili na kujitenga sio la kusimiliwa,tembelea sana maeneo ya ilala,magomeni nzima na sehemu kubwa wanapo ishi.ujue chuki zina toka kwa hawa mda wote
Mlicho kipanda ndio mtakacho kichuma, kulazimisha muungano, kuharibu uchaguzi zanzibar, kuwauwa wanzanzibari kwenye maandamano, kuwabaka watoto wao huko pemba, kuikataa rasimu ya wairioba, yote hayo yanajenga imani tofauti, kwamba nyinyi ndio mkoloni wa zanzibar, lazima muchukiwe kama anavyo chukiwa mkaburu south Africa, hilo lazima mu kubali.
 
Tuachieni jamani, kama udugu tutakutana East Africa community, muungano wa tanganyika na zanzibar hatuutaki
 
Tafuta video za mapokezi ya timu ya zanzibar ndio utajua, kama ni washabiki au wazalendo
Sasa nimekuelewa. Kwamba unataka kwenye kusherehekea ushindi kila shabiki awe mstaarabu, muungwana, mzalendo na mnyenyekevu kwa kadri unavyohisi wewe ni sahihi. Hilo haliwezekani popote pale duniani. Unapaswa kusikiliza maoni na matamshi ya wahusika wakuu wa timu inayoshangilia. Laiti kauli hizo zilizokuudhi zingetolewa na Kocha (aliyewashukuru Watanzania wote) na/au viongozi wengine, ungekuwa na hoja. Ni lini Simba na Yanga zinapofungana umesikia mashabiki wa aliyeshinda wakimpa pole mtani wake mitaani? Umepata kusikia shangwe za mtani aliyeshinda zisimnange mpinzani wake? Wakati wa kusherehekea ushindi, aliyeshindwa anapaswa kujua, kujiandaa na kustahamili kauli za maudhi, ambazo mara nyingi ni mfululizo wa kutambiana kulikoanza kabla ya mpambano. Simba kuitwa wa mchangani/matopeni hajatukanwa na Yanga. Yanga kuitwa gongowazi hajatukanwa na Simba. Kama pilipili inavyonogesha ladha ya chakula licha ya kuwasha, ndivyo utani kama huu unavyonogesha ladha ya mpira licha ya kuwa haumpendezi aliyeshindwa.
 
Mimi nilisikia kuna clip wanatuita sisi Watanganyika ni "machogo" sasa sijaelewa wa namaanisha nini?

"Machogo" sio matusi ni utani wa zamani sana watu wa Unguja walikuwa wanawaita watu kutoka Mrima(Tanganyika aka Tanzania Bara aka Bongo), vile vile watu wa Unguja walikuwa wanawaita Wapemba "Vibuwa",vibuwa ni samaki wanaovuliwa kwa wingi

""Chogo" maana yake ni kichwa kilicho vimba nyuma...alikuwepo mchezaji mmoja maarufu sana wa simba yeye alikuwa na jina la utani "Chogo chemba"

Hakuna matusi hapo isipokuwa utani wa zamani umerudi,wasiojua wanaona matusi
 
Mlicho kipanda ndio mtakacho kichuma, kulazimisha muungano, kuharibu uchaguzi zanzibar, kuwauwa wanzanzibari kwenye maandamano, kuwabaka watoto wao huko pemba, kuikataa rasimu ya wairioba, yote hayo yanajenga imani tofauti, kwamba nyinyi ndio mkoloni wa zanzibar, lazima muchukiwe kama anavyo chukiwa mkaburu south Africa, hilo lazima mu kubali.
Umesahau Masheikh wa UAMSHO,wamewatoa jela waliobaka lakini wanaohubiri maneno ya Mungu wako ndani mwaka wa 5 sasa
 
Back
Top Bottom