Zanzibar 2020 Zanzibar wapiga kura ya mapema. Makundi yanayoshiriki ni Watumishi wa ZEC na Vyombo vya Ulinzi na Usalama (Oktoba 27, 2020)

Zanzibar 2020 Zanzibar wapiga kura ya mapema. Makundi yanayoshiriki ni Watumishi wa ZEC na Vyombo vya Ulinzi na Usalama (Oktoba 27, 2020)

Zanzibar hali ni shwari na leo kura ya mapema ndio inapigwa na tukio liko mubashara ITV.

Karibu.

Maendeleo hayana vyama!
 
What so special kwa vyombo vya ulinzi vya Zanzibar na ZEC yao mwaka huu 2020?

Hivi bara hakuna vyombo vya ULINZI?


NI WAZI KWAMBA SISIEMU INATUPELEKA PABAYA KWA MASLAHI YA MATUMBO YAO
IMG_20201026_193726.jpg
 
Kuna mchezo mchafu unaendelea katika huu Uchaguzi, inakuaje Zanzibar ina watu kiduchu wapige kura siku mbili?

Ni nchi ina mamlaka kamili watafanya ZEC inavyoona sawa huko bara NEC ingeamua hivyo wangefanya
 
Itendee haki nafsi yako kesho ni siku maalumu ya kulipiza kisasi kwa mabaya yote uliyotendewa na Utawala huu dhalimu.

Weka tiki (vema) kwenye jina la mwisho la mgombea, hakikisha hiyo vema ama tiki yako haitoki nje ya kibox (kisanduku).

Pia usitoboe macho kwa mgombea number moja kwa hasira maana kufanya hivyo utakuwa umeharibu kura yako.
 
Tunaomba ZEC Watoe idadi kamili ya hao watu wa makundi yanayopiga kura leo na baada ya zoezi hili kura zao zote zihesabiwe na matokeo yawekwe wazi!
 
Kura zinapigwa mara mbili kuwapa vyombo vya ulinzi na usalama nafasi ya kuhudumu vizuri siku ya kesho, sasa mnapo vuruga na siku ya leo mnaendelea kuthibitisha kuwa mnapenda vurugu na walioweka siku mbili tofauti walikuwa sahihi kabisa
Kwa nini huo utaratibu uwe mwaka huu tu??
 
Huu mtindo wa ZEC unajenga mazingira ya watu kupiga kura mara mbili! ZEC wanaposema sio Polisi wote watapiga kura je nani ataamini kama Polisi aliyepiga kura leo hatarudi kupiga kesho?

Pia ni vema ZEC ingekuwa inatoa idadi kamili ya watakaopiga kura na baada ya zoezi hilo matokeo yawekwe wazi ili wananchi tulinganishe na idadi tuliyopewa!

Vinginevyo utaratibu ungekuwa kama ilivyo Bara au ungefutwa kabisa sababu wahusika ni kundi dogo tu!
 
Kura zinapigwa mara mbili kuwapa vyombo vya ulinzi na usalama nafasi ya kuhudumu vizuri siku ya kesho, sasa mnapo vuruga na siku ya leo mnaendelea kuthibitisha kuwa mnapenda vurugu na walioweka siku mbili tofauti walikuwa sahihi kabisa
Wako sahihi kivipi? Kesho pia watarudi kumpigia kura Rais wa JMT. Sasa huko siyo kupotezeana muda? Lengo la kupiga kura leo ni kuiba kura za Rais wa Zanzibar ambazo zitarundikwa mahali bila kuhesabiwa ili zichanganywe na za maruhani na za mazombi. Wanajua Mwinyi hakubaliki Zanzibar. Bila wizi wa aina hii Mwinyi hatoboi.
 
Back
Top Bottom