Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Sana.Ni mambo ya kuzingatiwa na kuwa nayo makini mnoo.Baniani mbaya,kiatu chake "mapato mazuri ya dolari za utalii"/dawa.
 
Kama ni Gari BINAFS la meneja sio issue sana ila kam ni gari la ki ofisi meneja amekosea
Kufukuza watalii kwa kuhoji vipi hapo? Wako kwenye vita na Palestina.Hapo hotelini waweza hisi kuna wapiganaji wa palestina kwa hiyo mrseji ya free Palestine. Hoteli iliyakiwa kutumia hekima kuwa slogans zozote au magari yenye maneno kama hayo yasiingie hotelini au wenyewe wayabandue
Hapo ni sehemu ya biashara
 
Hahahahaha watazimia.
Watanzania huwa wanafanya vitu sensitive kwa aidha kujifurahisha,kupigana vijembe au mara chache sana kumaanisha kweli wakifanyacho bila kujua ni matokeo gani yatajiri mbeleni.Kuna mambo siyo ya kufanya au kuonesha tu bila kupima na kutabiri matokeo.We've to be professionals rather than amateurs. Going by the book/directives!
 
Hawajajifunza kwa yaliyotokea kwenye hoteli ya muizraeli kule Mombasa.
 
Hao jamaa wa Israel sio wanafiki kabisa, wameona kitu cha kuwakwaza wakaona wasinyamaze.

Sasa huyo meneja wa hiyo hoteli akatafute wapalestina awajaze hapo hotelini kwake, unafanya biashara huku ukiwa huna akili ya hiyo biashara unayofanya, wateja wakipungua unaenda kwa mganga kusafisha nyota.
 
Ndio hichohicho, complaining ya nini? Wangehama tu hoteli, simple.
🀣🀣🀣🀣Kuna tofauti ya malezi,makuzi na mazoea kutoka jamii moja hadi nyingine hasa wazungu,waafrika na mongloids.Wazungu(jumlisha na waizraeli)si watu wa kunyamazia/quit jambo au kunyongea popote.Huuliza na kudadisi.Very inquisitives!Kunyamaza na unyonge ni kwa waafrika,mongloids na waasia baadhi.
 
Kama walipingia walishalipia tayari mfano siku kumi .Wakitaka kuondoka na kudai refund unafikiri bila kutoa sababu za msingi wangerejeshewa hela zao ili wahamie hoteli nyingine?
Tatizo mnaweka hisia zenu za kidini katika hili, post yako kabla ya hii inajieleza kuhusu wewe.

Hivi unafikiri meneja wa hoteli ni mjinga awafukuze watu waliolipia siku nyingi bila refund? Acha tu kuwatimua, hukusoma walienda kufanya fujo mapokezi kwa kulalamikia hilo gari lenye bendera za Palestina?

Ifikie wakati kama binadamu tujifunze ustaarabu na kukubaliana na mawazo huru, kila mmoja ana uhuru wa kuamini anachotaka na ikiwa tofauti na wewe sio vita.
 
Hilo halina shida, ila sio kwenye nchi za watu unataka kuwapangia watu namna ya kuishi.

Mamlaka za nchi hazina tatizo na hilo la mwenye gari kuweka itikadi zake kwenye gari, wewe wa kuja unamletea shida? Tena nawashangaa sana nyie watu mnaowashabikia hii ni dharau kubwa sana kwetu mgeni kujipa mamlaka nchini kwetu.
 
Watu wanajisahau sana, kama hawakupendezwa na hilo wangehama hoteli kimyakimya na sio kuanzisha fujo. Upo nchi za watu unataka kupangia watu maisha?
Na ndio tabia ya waisraeli, ni wasumbufu sana, wanapenda fujo, wajiona ni watu special sana, wanapenda kuwatawala watoa huduma, kila anachotaka umpatie
 
H

Hata Marekani Kuna watu wanavaa tisheti zimeandikwa free palestine, wakati fulani free Mandela. Hiyo sio tatizo, ingekuwaje wangekuta mtu kaweka bendela ya Israel kwenye gari lake wangelalamika
Labda kama bango lemewekwa hotelini hiyo sio sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…