Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Zanzibar: Watalii wanne kutoka Israeli watimuliwa Hotelini kwa kulalamika kuhusu gari kuandikwa "Free Palestine"

Hapa tunaangalia usalama wa biashara ya utalii sio haki za uanaharakati wa kivita, kidini au kisiasa.

Kosa linapimwa kwa matokeo, matokeo ya kufanya harakati za kivita kwa upande A ni kupoteza wateja wa upande B na tunahitaji wateja wote A na B na ndipo kosa la meneja lilipo.
Kwahiyo usalama wa utalii upatikane kwa ku-entertain extremismm? Unaanzaje kuchukizwa na uhuru wa taifa lingine halafu bado unataka uwe entertained kwa kisingizio cha biashara? Hivi ikiwa wanakerwa hadi na stika waliyoiona thousands of miles away from their country; ulishawahi kujiuliza reaction yao inakuwaje wakikutana na hao wanaotaka waendelee kukandamizwa? Marekani na EU pamoja na support yao yote kwa Israel KATU hawawezi ku-support hao watu wazi wazi, na ndo maana hata kama ni kinafiki, juzi kati tu hapa kuna Jew Extremists wamepigwa ban kuingia US na EU Countries.
 
Umepiga penyewe. Kuna hoteli moja Arusha(sijafika, nimesimuliwa na rafiki yangu), wao wameamua kuwajaza Wakenya mpaka walinzi wa getini baada ya kuona kuwa Watanzania "wanazingua".

Unaambiwa hiyo hoteli mpaka walinzi wa getini wanao uelewa wa "customer care", na wanapractice effectively.
Ukishakuwa mfanyabiashara ni vema kukubali kuitwa mtumwa.Kwani kweli unakuwa mtumwa?Unatafuta pesa.Unyenyekevu ni kucheza na akili ili mteja atoe hela.Na ikiwezekana hadi amalize zote na kukuazima nauli kwa riba.
 
Hebu soma tena ulicho andika sikuelewi hata unaandika nini ?
Ujumbe upo wazi huo.

Ukisoma hiyo habari upande wa kingereza inasema waisraeli walikuwa "concern" na itikadi ya meneja.

Ni sawa na mkristo awe concern na meneja muislamu mwenye mindevu yake anayemhudumia akiwa kavaa kanzu imeandikwa kafiri hana haki.
 
Ukishakuwa mfanyabiashara ni vema kukubali kuitwa mtumwa.Kwani kweli unakuwa mtumwa?Unatafuta pesa.Unyenyekevu ni kucheza na akili ili mteja atoe hela.Na ikiwezekana hadi amalize zote na kukuazima nauli kwa riba.
Kunyenyekea siyo kuwa dhaifu au kuogopa, watanzania tuna shida sana ya kuwa na nidhamu ya woga.
 
Kwahiyo usalama wa utalii upatikane kwa ku-entertain extremismm? Unaanzaje kuchukizwa na uhuru wa taifa lingine halafu bado unataka uwe entertained kwa kisingizio cha biashara? Hivi ikiwa wanakerwa hadi na stika waliyoiona thousands of miles away from their country; ulishawahi kujiuliza reaction yao inakuwaje wakikutana na hao wanaotaka waendelee kukandamizwa? Marekani na EU pamoja na support yao yote kwa Israel KATU hawawezi ku-support hao watu wazi wazi, na ndo maana hata kama ni kinafiki, juzi kati tu hapa kuna Jew Extremists wamepigwa ban kuingia US na EU Countries.
Utalii ni biashara. Biashara inahitaji wateja, wateja ili waje wanahitaji huduma bora, huduma bora ni pamoja na kuficha hisia zako dhidi ya unaowahudumia.

Unachaguaje sehemu ya biashara yako ndo iwe platform ya kupigania uhuru wa nchi nyingine?

Si utapoteza hata waisraeli wasiokubaliana na wenzao sababu hawajui kama wapo salama wakihudumiwa na wewe sababu ya uisraeli wao?
 
Hotel au sehemu yenye kutoa huduma kwa watu wenye itikadi,imani,maono mchanganyiko unawekaje vitu vitakavyowakwaza?Kutokujielewa huko na kuharibu biashara.
Kwa hiyo mfano kwako hauwezi kuweka bango linalozuia ushoga, kwa kuhofia kuwakwaza mashoga? Na je mbona sehemu nyingi hubandikwa picha ya Yesu ilihali hata waislam huhudumiwa hapo?
 
Ujumbe upo wazi huo.

Ukisoma hiyo habari upande wa kingereza inasema waisraeli walikuwa "concern" na itikadi ya meneja.

Ni sawa na mkristo awe concern na meneja muislamu mwenye mindevu yake anayemhudumia akiwa kavaa kanzu imeandikwa kafiri hana haki.
Hii nini sasa unaandika wewe
 
Mkuu hadi wewe unakuja na hoja dhaifu namna hii?

Unaona hoja dhaifu kwa kuwa hujaelewa mtazamo wangu...

Mtu anayetaka kulipiza kisasi aje na gari lenye bendera kabisa hotelini?
Hizi ni akili za wapi?

Mkuu inaonesha huna ufahamu sana wa mahusiano ya Wapalestina na Wayahudi na namna wanavyochukuliana...

Nimeishi na Wapalestina chuo kimoja na nakumbuka vyema kisa kimoja namna walivyotaka kumfanya dada mmoja Myahudi ambaye ndio kwanza alijiunga na chuo pasipo kujua uwepo wa Wapalestina...

Hivyo nimeandika kutokana na uzoefu pia...

Yani watu waulize tu juu ya usalama wao wafukuzwe hotelini?

Kwa hiyo wewe unadhani wamefukuzwa kwa sababu ipi ambayo imeandikwa hapo juu na mimi sijaisoma au sijaiona?
 
Kama hakuna hoja sasa jikite kwenye mambo unayoyaelewa achana na usiyoyaelewa.
Nina uhuru wa kujikita katika jambo lolote au uhuru wangu wakukarahisha ? Na kama hakuna hoja sipaswi kukuambia hakuna hoja ?!
 
Utalii ni biashara. Biashara inahitaji wateja, wateja ili waje wanahitaji huduma bora, huduma bora ni pamoja na kuficha hisia zako dhidi ya unaowahudumia.
Hao wateja ambao biashara inawahitaji hawawezi kuwa extremists kwa sababu Extremism ni sumu kwenye biashara! Hotel ni sehemu ambayo kila mgeni anahitaji kujisikia yupo salama lakini mtu hawezi kujisikia salama ikiwa miongoni mwa wageni hawataki kusikia utetezi dhidi ya wanaokandamizwa na kuuawa!! Na wala msijidanganye eti Watalii wanaweza kususa kisa kuna ma-extremists yamepigwa ban hapo hotelini kwa sababu hayo ma-extremists yanapingwa nchi nyingi tu.
 
Back
Top Bottom