Zanzibar yaingia kwenye ushirikiano na Uholanzi ili kufanya uwezekezaji zaidi kwenye bandari. Kuna usalama kweli au ndo yale yale ya DP World?

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu inaonekana sekta ya bandari huko Zanzibar inazidi kukua na kuonesha ubora wake duniani

Na hii ni baada ya hivi karibuni Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi kwa kushirikiana na Shirika la Bandari Zanzibar (ZPC) pamoja na Ubalozi wa Ufalme wa Uholanzi nchini Tanzania wamekaribisha wajumbe, wafanyabiashara, na wawekezaji katika sekta ya bandari na usafirishaji kutoka Uholanzi.

Mkutano huo umejumuisha kampuni 20 kutoka Uholanzi ambazo zimeonyesha nia ya kuwekeza katika sekta ya bandari Zanzibar.

Soma pia: Seoul yasaini Mkataba wa Kujenga Bandari ya Uvuvi Zanzibar

Hafla hiyo imehusisha utiaji saini wa makubaliano muhimu na ziara katika bandari za Malindi na Mangapwani, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya Zanzibar na Uholanzi katika sekta ya bandari

Huu mkataba wa "Ushirikiano" umekaaje? Au ndo yale yale ya DP World?





 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…