Zanzibar yanunua mashine yake ya kupimia sampuli za COVID19, itapokelewa visiwani humo kesho

Zanzibar yanunua mashine yake ya kupimia sampuli za COVID19, itapokelewa visiwani humo kesho

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Waziri wa afya wa Zanzibar mh Hamad Rashid amesema Zanzibar imeamua kununua mashine yake ya kupimia maambukizi ya Covid 19 ili kurahisisha upimaji na kupata vipimo kwa wakati.

Mh Hamad amesema mashine hiyo itawasili nchini Zanzibar kesho na baada ya kufungwa takwimu zitaendelea kutolewa kwa wakati bila kusitisha sitisha.

Source: BBC Dira ya Dunia

Maendeleo hayana vyama!
 
Sasa sielewi kabisa kuhusu hizi mashine kumbe na ya ZNZ ilikuwa inazingua
 
Inabidi watalaam wetu wajiridhishe nayo kwanza, waicheki na kuuidhinisha ndio ianze kutumiwa...Hawa mabeberu hawaaminiki..
 
Bora aisee Zanzibar wataokoa utalii wao, kwa maana utalii baada au kipindi hiki cha Corona 100% unategemea ni kwa kiasi gani wageni wana imani na hali ya nchi inaweza kuhakikisha usalama wao

kwa sasa tunaweza waona Kenya mafala kwa kutoa namba za wagonjwa, vifo na waliopona ila utalii ukifunguka tutawaelewa.... kurejesha utalii sio kufungua mipaka ya nchi tu inahitaji transparency, trust and good reputation .
 
Bora aisee. ....... Zanzibar wataokoa utalii wao, kwa maana utalii baada au kipindi hiki cha Corona 100% unategemea ni kwa kiasi gani wageni wana imani na hali ya nchi inaweza kuhakikisha usalama wao kwa sasa tunaweza waona Kenya mafala kwa kutoa namba za wagonjwa, vifo na waliopona ila utalii ukifunguka tutawaelewa.... kurejesha utalii sio kufungua mipaka ya nchi tu inahitaji transparency, trust and good reputation .
Waangalie na madangulo ya mabwabwa ...maana waitaliano wale si ndio walasambazia huko upendo.
 
Hongereni sana, huku bara toka tupime mapapai,kware,mbuzi na oil hata takwimu hatupewi kwa kisingizio eti kuna uchunguzi wa vifaa na wataalamu.
 
Wamenunua wao au wamenunuliwa na Rostam? tuwekane clear kwenye hili
 
Back
Top Bottom