Zanzibar yatangaza bei mpya za umeme

Zanzibar yatangaza bei mpya za umeme

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (Zura), imetangaza bei mpya elekezi kwa watumiaji wote wa umeme kisiwani humo ambapo zitaaza rasmi Januari 20, mwaka huu.

IMG_2603.jpeg
Kwa mujibu wa Zura, ilipokea maombi ya kubadilisha bei za umeme kutoka Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya matumizi ya umeme Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Zura leo Januari 18, 2025, bei hizo zimetoa punguzo la Sh190 kwa watumiaji wadogo ambao walikuwa wakilipa TSh 480 kwa uniti kila wanapovuka matumizi ya uniti 50 kwa mwezi ambapo kwa sasa watalipa Sh290 badala ya TSh 480.

Meneja wa kitengo cha Uhusiano Zura, Mbaraka Haji amesema tozo ya kutoza huduma kwa watumiaji wadogo kuanzia unit 0 hadi 50 itaendelea kuwa TSh 2,100 huku bei ya kuungiwa kwa uniti moja ikiongezeka kutoka TSh 79 hadi TSh 84.

Wateja wenye matumzi ya kawaida wenye matumzi ya uniti moja hadi 1,500 bei ya kuungiwa kwa uniti moja imepanda kutoka Sh266 hadi Sh280 huku kila uniti inayoongezeka ikitoka TSh 288 hadi TSh 310 na tozo ya kutoa huduma itaendelea kuwa TSh 2100.
 
Wameongea na wazalishaji wa umeme au wamejiamulia tu ? 😏
 
Haya ndio matunda ya bwawa la Rufiji kwa wenye maarifa acha wadanganyika wakamuliwe hadi mbupu zikonde.
 
Back
Top Bottom