Zari, Diamond biashara kwisha

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
BIASHARA imekwisha ! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia ‘kapo’ ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz ’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kudaiwa kuwa waliweka misingi ya penzi zito ili Diamond apate mtoto hivyo baada ya mrembo huyo kujifungua Latifah ‘Tiffah ’ miezi miwili iliyopita, penzi halitakuwa motomoto kama zamani , Risasi Jumamosi lina ‘full ’ stori .
Chanzo cha uhakika kilicho karibu na wawili hao, kimesema makubaliano ya awali baina ya wazazi hao , yalikuwa ni kwa mwanamke huyo raia wa Uganda , kumzalia mtoto Diamond ambaye alikuwa akisaka ubaba kwa udi na uvumba .

TUJIUNGE NA CHANZO

“ Wote mnajua jinsi Diamond alivyokuwa akihangaika kupata mtoto , maana wapenzi wake wote wa awali hawakuweza kumzalia. Sasa alipokutana na Zari ambaye tayari alikuwa na watoto , wakakubaliana kwa masharti kuwa ndani ya muda f ’lani , amzalie .
Rose akipewa zawadi ya keki na Harmonizer kwa niaba ya Wasafi Classic Baby.
“ Sasa ndiyo ikawa hivyo , baada ya Tiffah kuzaliwa , kila mtu sasa yupo huru kufanya yake , ndiyo maana Zari amerudi kwake Afrika Kusini ‘Sauz ’ na hawezi kuja kuendelea kuishi na Diamond kama wakati ule wa ujauzito .
“ Kule Sauz , Zari anaendelea na biashara zake na nimesikia kwa sasa anaandaa Zari All White Party kama ile aliyoifanya Mlimani City hapa Bongo ,” kilisema chanzo chetu .
Msanii chipukizi wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WBC ’ aitwaye Harmonizer akilishwa keki na Rose.

KWA NINI HAWEZI KURUDI ?

Chanzo hicho kiliendelea kutoboa siri kwamba, pamoja na makubaliano ya kuzaa , lakini pia mazingira ya sasa ya makazi ya Diamond hayatoi nafasi kwa mwanamke huyo mwenye fedha ambaye pia ni msanii, kuweza kuishi .
“ Sasa hivi pale nyumbani kwa Diamond kumejaa, imekuwa familia kubwa. Maana kuna mjomba wake Diamond anaishi pale , dada zake wawili , Esma na Queen Darleen wanaishi pale. Mama yake Diamond ( Sanura Kasim ) yupo pale .
“ Haya, achana na ndugu wengine. Lakini pia kuna wasichana wa kazi wawili na mlinzi mmoja. Sasa kwa mtu kama Zari ambaye maisha yake ni ya kisupastaa hawezi kuishi kwenye nyumba yenye watu wengi hivyo .”

ZARI ANAOGOPA UMBEYA

“ Pia inasemekana Zari hataki kuishi na wifi zake kwa sababu anaogopa umbeya . Hata wakati ule alipokuwa mjamzito mpaka kujifungua, hakuwa mtu wa kujichanganya nao sana . Alikuwa mtu wa peke yake peke yake tu.”

HAKUNA TENA MAPENZI ?

“ Taarifa nilizonazo ni kuwa , Diamond na Zari watakuwa wanaendelea na uhusiano wao wa kimapenzi lakini si ule wa kama awali . Ila wataendelea kuwa watu waliozaa mtoto na maisha ya Tiffah yataendelea kuwa kwa mama yake hadi hapo watakapoamua vinginevyo . Zari anaweza kuja Bongo na Diamond anaweza kwenda Sauz kwa Zari . ”
“ Zari hataki kuishi Tanzania , anataka Tiffah aishi na ndugu zake kule Sauz hadi akue na kuanza masomo. Kwa hiyo usitegemee ule ukaribu kama wa mwanzo . ”

KUHUSU DIAMOND !

Jitihada za kumpata Diamond ili aweze kuzungumzia suala hilo ziligonga mwamba ikielezwa kuwa yupo nchini Marekani katika shughuli za kimuziki . Hata alipotumiwa meseji kwa njia ya Mtandao wa WhatsApp hakujibu.
Hata hivyo , mtu wake wa karibu ambaye hakupenda jina lake lichorwe gazetini, alitatizwa na suala hili akisema:
“ Dah ! Wabongo bwana ! Ninachojua mimi ni kuwa, bado watakuwa wapenzi japokuwa siwasemei maana Diamond naye haaminiki sana . Si unajua ameshapata mtoto , lolote linaweza kutokea .
“ Ila Diamond akimhitaji Zari aje Tanzania anaweza kuja , akitaka aende Sauz atakwenda kwa sababu Tiffah lazima alelewe na wazazi wote .
“ Halafu lazima ujue kwamba , Zari ni mfanyabiashara , ana biashara zake Afrika Kusini na Uganda . Kwa hiyo siyo mtu ambaye unaweza kumtegemea akae sehemu moja tu
 
Nilochopenda ni wao kikiri mtoto ni wa Diamond...

MWANAMKE ukitaka uwe na raha ujitegemee na uwe na pesa yako na uwe na kiburi HASWA .mambo ya kuwa golikipa utaishia matusi , minyanyaso .Hivi kwa nini watu hawawezi kujitegemea Hao ndugu zake Diamond wanasuburi kulishwa maisha gani hayo .Mtu ukishamaliza high school bye Tafuta kwako
 
Ukweli ni kwamba drug lords can do anything to win the market.. Diamond katumiwa tu na akina Ivan through Zari ili hao waganda wapate soko la madawa Bongo lakini pia wapate sehemu ya kusafishia pesa zao.. Bad lucky punda Diamond anayajua hayo yote...
 
We kweli fisadi!ni nani amekulisha sumu hiyo?!kwa taarifa yako Ivan ametajirika kabla hata Diamond hategemei kuimba!story za kitoto hizo zinachekesha
 
Ukweli ni kwamba drug lords can do anything to win the market.. Diamond katumiwa tu na akina Ivan through Zari ili hao waganda wapate soko la madawa Bongo lakini pia wapate sehemu ya kusafishia pesa zao.. Bad lucky punda Diamond anayajua hayo yote...

Kweli we fisadi.Maana hii taarifa ya kifisadi ndio naisikia kwako tena umewataja na mafisadi wenyewe.
 
Kweli we fisadi.Maana hii taarifa ya kifisadi ndio naisikia kwako tena umewataja na mafisadi wenyewe.

Mjini hapa sio mnashangaa shangaa.. Au mnafikiri na ile X5 ni yake?? Si mnakumbuka alivyonyang'anywa ile VX na aliyempa?? Mjini hapa kaeni vizuri
 
Mjini hapa sio mnashangaa shangaa.. Au mnafikiri na ile X5 ni yake?? Si mnakumbuka alivyonyang'anywa ile VX na aliyempa?? Mjini hapa kaeni vizuri

Shikamoo fisadi.
 
Marhabaa.. Na huyo Zari ameshaona moto wa EL utamchoma kakimbia Tz na wala hatokaa harudi hapa kama Ukawa itaingia madarakani..

Kama wale YA UVUGUVUGU BENDI waliotembea mikoani wakimnanga mzee LAIGWAAAA jana walikuwa wanafanya show huku wakijichekesha wenyewe while people zimenuna kwenye BSS.Kweli Fiesta ya chama imewaponza.
 
Kama wale YA UVUGUVUGU BENDI waliotembea mikoani wakimnanga mzee LAIGWAAAA jana walikuwa wanafanya show huku wakijichekesha wenyewe while people zimenuna kwenye BSS.Kweli Fiesta ya chama imewaponza.

Njaa zao zitawaponza.. Na ngoja aingie Ikulu
 
Ukweli ni kwamba drug lords can do anything to win the market.. Diamond katumiwa tu na akina Ivan through Zari ili hao waganda wapate soko la madawa Bongo lakini pia wapate sehemu ya kusafishia pesa zao.. Bad lucky punda Diamond anayajua hayo yote...

Hahahaha! Hii ina 100% ukweli ndani yake ujanja siyo kumpiga demu mimba ujanja ni walikuwa wanapiga hela kupitia mgongo wa diamond! Na hawa kina ivan wamefanikiwa kwa hilo! Pole sana diamond mjini hapa
 
Ukweli ni kwamba drug lords can do anything to win the market.. Diamond katumiwa tu na akina Ivan through Zari ili hao waganda wapate soko la madawa Bongo lakini pia wapate sehemu ya kusafishia pesa zao.. Bad lucky punda Diamond anayajua hayo yote...

Hahahaha! Hii ina 100% ukweli ndani yake ujanja siyo kumpiga demu mimba ujanja ni walikuwa wanapiga hela kupitia mgongo wa diamond! Na hawa kina ivan wamefanikiwa kwa hilo! Zari anafanya umalaya kumbe kuna biashara nyingine ndiyo kitu wema sepetu alishindwa! Pole sana diamond mjini hapa!
 
Kwa hiyo hawa akina Ivan wapo tayari demu wao agongwe na azalishwe kisa tu biashara?? Ukawa bhana teh teh teh
 
Gazeti lenyewe halina tofauti na gazeti la UHURU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…