Zari punguza "kimuhemuhe"

Zari punguza "kimuhemuhe"

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
70,916
Reaction score
141,437
Zari taratibu na hiyo kiu yako ya ndoa, bwana atapepea huyo akuachie jina tu ubaki Mrs hewa, haujifunzi tu? Kwa Diamond hivo hivo Mrs Dee Mrs Dee ukanunua na lile sijui joho sijui gauni nyuma limeandikwa Mrs Dee mara kikatokea kibinti kikapewa mimba na jina la Dee kikampa mtoto, Boss Lady ukabakiziwa Joho tu, haya ushampata mpya tayari ushaanza mbwembwe za Mrs kwanini usitulie hadi mambo yakae sawa, sidhani kama kuna mwanaume anaependa hiyo tabia asee nnavojua ukijionesha una kiu iliyopitiliza hukawii kuachwa kwenye mataa, labda kwakua we bosslady ila sie kina mwajuma ndala ndefu wataishia kutimka mbio tu.

Kama ulivofanya mchumba awe siri, hebu hiyo ndoa inyamazie kwanza hata uwe engaged unajionesha kuitaka sana ni kama vile unataka ndoa ili ukomeshe watu, itakushinda kuihudumia bureeee kisa unataka ukomesheee.... Tulia bwana kwa diamond ulitangaza 2018 it gonna be million dollars typa shit, jini mkata kamba akapita kabla hata hujavalishwa pete
Screenshot_20190617-162028.png
 
Maisha ya social media hayajawahi kuwaacha salama hawa watu, sijui ni kumuonyesha mond bado yumo, sijui kuwaonyesha haters wake kama yumo mie hata siwaelewi, kuhesabiwa mabwana kwao kawaida tu , wacha tusubirie uso wa bae wa watu
 
Tatizo ukifanya kwa siri siri diamond hataona na hataumia.
Yeye nia yake ni diamond aumie.
Lakini hajamtangaza baby wake, kwa hiyo hata wakiachana akipata mpya anaweza akaendelea kuigiza kwamba ni huyohuyo.
Atulie tu bwana atasepa kwa hicho kiherehere
 
Huyu Dada nilikua nampenda,,mtu amkimsema vibaya naumia kama namjua ,sa hivi anayoyafanya namuona mpuuuzi ,,,hawezi kuishi bila showoff za kitoto. Kwa jinsi anavojiita bosslady angetakiwa awe expensive kwa kila kitu. Matokeo yake anaoneka cheap kuliko amber lulu
 
Kwa sababu hajamuonyesha sura hivyo hata ndoa ikipeperuka anaweza ibuka na movie kuonyesha ilikua kiki etc. Huwez amini ila ndo hivyo pamoja na yoote ila simfatiliii sana sina snap chat,insta wala fb bali mambo yake nayapatia google na humu ndo maana sikereki sana na nyendo zake.
Unanijua kabisa mie shabiki sana tu wa bosslady ila hizo cheap show off za ndoa no kwakweli lile joho la Mrs dee nadhani unalikumbuka.... Atulie tu
 
Bado yuko busy kumuumiza DP kwa kuonyesha yuko na njemba mwingine aliyeamua kuficha sura yake. Kama ameingia kwenye uhusiano mpya ili kumkomoa kwa namna moja au nyingine DP na kuingia kwenye ndoa haraka haraka ili yeye awe mshindi wa kuingia kwenye ndoa kabla ya DP basi inaweza kabisa kula kwake.

Vitendo vyake vingi vinaonyesha bado anampenda DP.

Zari taratibu na hiyo kiu yako ya ndoa, bwana atapepea huyo akuachie jina tu ubaki Mrs hewa, haujifunzi tu? Kwa Diamond hivo hivo Mrs Dee Mrs Dee ukanunua na lile sijui joho sijui gauni nyuma limeandikwa Mrs Dee mara kikatokea kibinti kikapewa mimba na jina la Dee kikampa mtoto, Boss Lady ukabakiziwa Joho tu, haya ushampata mpya tayari ushaanza mbwembwe za Mrs kwanini usitulie hadi mambo yakae sawa, sidhani kama kuna mwanaume anaependa hiyo tabia asee nnavojua ukijionesha una kiu iliyopitiliza hukawii kuachwa kwenye mataa, labda kwakua we bosslady ila sie kina mwajuma ndala ndefu wataishia kutimka mbio tu.

Kama ulivofanya mchumba awe siri, hebu hiyo ndoa inyamazie kwanza hata uwe engaged unajionesha kuitaka sana ni kama vile unataka ndoa ili ukomeshe watu, itakushinda kuihudumia bureeee kisa unataka ukomesheee.... Tulia bwana kwa diamond ulitangaza 2018 it gonna be million dollars typa shit, jini mkata kamba akapita kabla hata hujavalishwa pete View attachment 1129943
 
Back
Top Bottom