Come on baby! Hakuna asiyejua kwamba pale Mond alikosea sana tena sana! Na kwa kufahamu hilo ndo maana Diamond akaenda hadi redioni na kutamka wazi! Na suala la Mond kukanusha kuzaa na Hamisa ilikuwa ni kumjali Zari kwa sababu wanaume ndivyo wanavyofanya! Ukipigwa mimba na mwanaume ambae yupo committed somewhere, trust me, atakukana hadi mbele ya baba paroko (labda muwe watatu tu) kwa sababu hayupo tayari kuharibu kule alikokuwa committed!
Na akasema wazi kwamba yupo tayari kwenda hadi SA kwa mguu kuomba radhi! Na hiyo kama haitoshi, kwenye wimbo wake Sikomi akaelezea kujutia kwake! Yote hayo inaonesha ni namna gani jamaa alijutia! Na kwenye lile sakata, mimi nilisimama upande wa Zari kwa sababu nilifahamu fika lengo la Hamisa lilikuwa kumkomesha Zari ndo maana alivunja makubaliano ya kwamba wafanye siri hadi at the right time!
Na yale kimsingi ni kama yaliisha!
Jambo ambalo Zari alisahau ni kwamba since day one anaanza na Diamond, watu walihakikisha anatengana na Diamond! Zikawa zinavujishwa kashifa za Zari kila siku watu wakidhani Diamond ange-react, lakini jamaa akawa anapuuza! Ikavujishwa hadi orodha ya wanaume 40 ambao Zari amelala nao; Mond akapuuza! Ikavujishwa hadi sex tape, Mond akapuuza! Ajabu, miongoni mwa watu waliokuwa wanafanya haya ni King Lawrence, ndugu wa Ivan; ikimaanisha kwamba hata Ivan na mwenyewe alikuwa nyuma ya yote lakini Mond akapuuza!
Tz akina Mange nao walihakikisha uhusiano wao unakufa! Kama unakumbuka, enzi zile ilikuwa kila siku mara Tunda kalala Madale, mara Lynn na Mond wameenda Rwanda! Yote ile ilikuwa ni maadui wa Zari na Mond kuhakikisha wanatengana! Finally, Zari akaingia mkenge baada ya kuvujishwa video Wema akimshika shika Diamond! Zari aka-panic huku akisahau yote hayo yalilenga kuwatenganisha! Na hivi sasa sijasikia tena habari za Tunda na Diamond huku nikiwa nimesikia habari za Lynn na Diamond mara moja tu wakati haikuwa kawaida!