Zawadi kwa Mwalimu

Zawadi kwa Mwalimu

Mohammed wa 5

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2022
Posts
1,215
Reaction score
3,035
Based on true story

Nakumbuka wakati tuko form 3 na 4 class letu lilikuwa linaongoza kwa sifa mbaya za utoro.umalaya hasa watoto wa kike,wizi,kwenda kuiba vitu kwenye mashamba ya walimu,bangi,watoaji mimba,viburi na wazee wa kula hela ya Ada.

Hizo sifa zote tulipewa sisi darasani kwetu na baadhi ya walimu wasiotupenda ambao walikuwa Wana chuki na sis sijui akiri zile walizitoa wapi wale ma father,makosa tulikuwa nayo Ila walizidisha chumvi.

Chuki ilizidi Hadi kwenye masomo walimu walikuwa wanafundisha darasani kwetu kama kukamilisha ratibu tu ili siku ziende sio wanafunzi tuelewe nakumbuka wakija walimu wa field tulikuwa tunaenjoy sababu hawatujui sis Japo wakiwa staff walikuwa wanasimuliwa mabaya yetu.

Nakumbuka wanafunzi wa madarasa ya chini ilikuwa ni kosa umekutwa darasani kwetu au unaongea na form 4 Kama tulitengwa hivi kwa kila kitu pale shuleni.

Sir Mshana popote ulipo mungu akuzidishie uendelee na moyo huo be blessed Sana sir
Ni moja ya walimu ambayo walitupigania kwenye kile kipindi kigumu tulichotengwa pale shuleni alikuwa bega kwa bega na sis alikuwa anatufundisha masaa ata 4 ili tuelew na yeyote mwenye swali, past paper muda wowote ampelekee kwa ajiri ya kumsaidia somo lolote lile nakumbuka mpak topic za masomo mengine alikuwa anafudisha Ili zitusaidie kwenye necta.

Wiki moja kabla ya Mtihani wa NECTA wale walimu wengine walikuwa wanakuja kutusema tujiandae kupata ziro za kutosha sis na wazazi wetu.

Sir Mshana 'alisema hapa wote mna akili na mtafaulu vizuri hata kama zimebaki dk 5 kwenda kwenye chumba cha Mtihani usiache kusoma Mungu atawasaidia.'

Baada ya matokeo kutoka darasa letu tuliongoza kwa kufaulu kuliko form 4 zilizomaliza na somo la sir Mshana liliongoza kwa ufaulu.

Tumekutana na classmates zangu tuliomaliza pamoja na wale waliopo mbali tuna group whatsapp. Tumekubaliana tuchange pesa wote ili tumpelekee sir Mshana zawadi Japo imepita miaka Kama 13 tokea tumalize bado yupo shule tuliomaliza form 4' age imeenda kidogo.

Kila classmates anamkubali sir Mshana

Respect sir Mshana be blessed father....🙏🙏🙏
 
Nitagonga kengele kabxa tuweke parade kwa ajili ya kuwaasa wadogo zenu wasipite njia mlizopitia Kwan mlifanya hadi nikawa na uhasama na waalimu wenzangu....nitangulize shukran za dhati kabixa....nipo kuzisubiria
 
Nitagonga kengele kabxa tuweke parade kwa ajili ya kuwaasa wadogo zenu wasipite njia mlizopitia Kwan mlifanya hadi nikawa na uhasama na waalimu wenzangu....nitangulize shukran za dhati kabixa....nipo kuzisubiria
Itakuwa vizuri tuwape 1&2 wadogo zetu
 
Back
Top Bottom