Zawadi ni Silaha ya Maisha

Zawadi ni Silaha ya Maisha

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
ZAWADI NI SILAHA YA MAISHA

Na, Robert Heriel

Maandishi ya Robert Heriel Kwa Lugha ya Kiswahili.
Haki zote zimehifadhiwa.

Katika ulimwengu wa viumbe wenye utashi, zawadi ni moja ya nyenzo ya maisha. Zawadi hutolewa kwa viumbe wenye akili, utambuzi na tafakuri. Zawadi haitambuliki katika ulimwengu wa viumbe wasio na utashi, wasio na utambuzi, viumbe mfu. Hii ni kusema huwezi mnunulia ng'ombe au mbuzi zawadi, kwani viumbe hivyo havijui nini maana ya zawadi.

Zawadi ni kitu chochote cha kuonekana au kisichoonekana apewacho mtu bila dhamira ya malipo, ikiwa na lengo la wema, furaha, msamaha, na upendo.

Kama nilivyosema hapo juu, Zawadi ipo katika ulimwengu wa Utashi, utambuzi na tafakuri.

AINA ZA ZAWADI
1. ZAWADI ZISIZOONEKANA (INVISIBLE GIFTS)
2. ZAWADI ZINAZOONEKANA ( VISIBLE GIFTS)

1. Zawadi Zisizoonekana - Invisible Gifts
Hizi ni zawadi ambazo hazionekani na zinatolewa na viumbe wasioonekana, au hata miungu, mizimu, majini, Mungu miongoni mwa wahusika katika ulimwengu usioonekana.

Kikawaida kila kilichopo kilitokana na ulimwengu usioonekana, hii ni kusema kila kitu ni zawadi kutoka ulimwengu usioonekana. Lakini kwa vile sisi tupo kwenye ulimwengu unaoonekana na tumevikuta vinavyoonekana, hivyo vinavyoonekana nitaviita Zawadi zinazoonekana ambazo chimbuko lake ni zawadi zisizoonekana.

Mifano ya Zawadi zisizoonekana, Akili, Uhai, Furaha, upendo, utamu, miongoni mwa mengine yasiyoonekana.

2. Zawadi zinazoonekana. - Visible Gifts
Hizi ni zawadi zinazoonekana kwa macho ya nyama ambazo zipo za asili na zilizotengenezwa na binadamu.
Zawadi hizi ni kama vile, Ardhi, , misitu, mikusanyiko ya maji kama bahari, ziwa na mito, wanyama, binadamu, hewa, Nuru, joto n.k

zawadi za kutengenezwa na binadamu ni kama vile Nyumba, mavazi, magari, ndege, vyombo vya muziki, mawasiliano, n.k

Jambo moja muhimu kujua ni kuwa, zawadi zote asili yake zinatokana na zawadi zisizoonekana ambazo chimbuko lake ni wahusika wasioonekana, miungu, Mungu, majini, mizimu n.k

Gari linatengenezwa kwa zawadi ya akili, maarifa na ujuzi. Bila akili huwezi kutengeneza gari, kujenga nyumba, kutengeneza nguo n.k

SILAHA
Silaha ni kifaa, kitu, chombo au jambo lolote ambalo linaweza kutumika kama sehemu ya kujilinda au kuangamiza. Jambo lolote duniani ni silaha, hii ni kumaanisha jambo lolote laweza kutumika kulinda au kuangamiza.

Zawadi ni silaha katika maisha. Inaweza kutumika kulinda au kuangamiza.

Mwanadamu ni zawadi katika ulimwengu huu. Mimi na wewe ni zawadi katika maisha ya hapa duniani. Mwanadamu ndiye amepewa jukumu la kusimamia hii dunia. Hii ni kusema mwanadamu ndiye anaweza kuilinda dunia au kuiangamiza.

Zawadi ya kwanza aliyopewa mwanadamu ni uhai, baadaye akapewa akili, kisha akapewa nguvu ya kutawala, kutiisha viumbe wengine, nguvu bila akili huwezi kutawala. Mwisho kabisa akapewa mahusiano.

Zawadi hizo ni lazima zitunzwe, zisipotunzwa zaweza kuwa silaha mbaya ya maangamizi za kumuangamiza mwanadamu.

Mtu unapopewa nafasi ya kuishi ujue hiyo ni zawadi, Mungu hahitaji malipo yoyote zaidi ya kutunza zawadi aliyokupa, naam ndio zawadi ya uhai.

Upende uhai wako, penda zawadi aliyokupa Mungu wako. Utakapoanza kuipuuza zawadi ya uhai utashangaa kuona mambo yanaenda mrama.

Uhai unatunzwa kwa kuzingatia kanuni maalumu, kanuni za viingiavyo mwilini iwe ni chakula, maji au hewa, kanuni za vinavyogusa ngozi yako iwe ni mavazi, mafuta, unga unga, wadudu wang'atao,

Lakini pia uhai unalindwa kwa mahusiano mema na watu wengi, viumbe wengine vinavyoonekana n a visivyoonekana.

Mke au mume ni zawadi kubwa sana ambayo ni lazima uitunze na kuiheshimu. Usipomheshimu mke au mume wako ambao kimsingi ni zawadi kutoka kwa Mungu ni wazi umeamua kutokumheshimu aliyekupa.

Hakuna ambaye aliidharau zawadi ya Mungu akabaki salama. Ukimdharau Mkeo au mumeo ni kwamba umeidharau zawadi aliyokupa Mungu. Na matokeo yake utaangamia, zawadi iliyokusudiwa iwe furaha kwako itageuka silaha ya kukuangamiza.

Sijawahi kuona mke au mume asiyemheshimu mweza wake alafu asihangaike, wengi wa watu wanaodharau wenza wao huwa na miisho ya kusikitisha, wengi huharibu maisha ya watoto, wengi huishia kufa kwa maradhi, wengi huishia kufa kwa majuto, wengi huishia kufa kwa ukiwa.

Unapopewa mwili mzuri, na sura nzuri aidha wewe ni mwanaume au mwanamke. Hiyo ni zawadi uliyopewa na Mungu lazima uitumie ipaswavyo, uiheshimu, na kuitunza ili kuonyesha unyenyekevu kwa Mungu aliyekupa uzuri huo.

Wanawake waliopewa zawadi ya matako makubwa yenye kuvutia baadhi yao hukosa akili, huzuzuliwa kwa zawadi hiyo. matokeo yake huishia kuleta dharau kwa waume zao, huishia kuwa malaya, hatimaye hujikuta wakipata mapepo wabaya, hujikuta wakipata maradhi na kusababisha umri wao kufupishwa.

Hakikisha zawadi zisidhuriane, uzuri wako usidhuru uhai wako, maarifa, elimu au akili zako zisidhuru uzuri wako au uhai wako. Hizo zote ni zawadi.

Usitumie zawadi moja kudhuru zawadi nyingiine. Wanaume tumepewa zawadi ya akili na mamlaka kuliko wanawake, Tusitumie mambo hayo kudhuru zawadi ya mke ambayo Mungu ametupa. Tutumie akili, mamlaka, mali na utajiri kufurahia zawadi hizo kwa pamoja.

Kuna watu hutumia mamlaka zao vibaya, kwa mfano, baadhi ya watu watembeapo mtaani wakiona mbwa au paka wanampiga au kumfukuza hata kama mbwa au paka huyo hasababishi madhara yoyote.

Zawadi ni silaha ya wema, lakini ni silaha ya ubaya ya kuangamiza kabisa

Ni vyema unapopewa zawadi uithamini, Uilinde, uipende na kuitunza. Kinyume cha mambo hayo itageuka kukuangamiza.

Ulikuwa nami;'

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
 
Rushwa ama takrima unaiweka kundi gani kwenye mtiririko huo wa zawadi?
 
Nani kakupa ruhusa ya kuhifadhi haki zote? Sisi wanajukwaa haki yetu iko wapi?
 
Eti wanawake wenye matako makubwa..😂😂
 
Back
Top Bottom