Zawadi ya gari kwa mfungaji bora

Zawadi ya gari kwa mfungaji bora

decomm

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2013
Posts
726
Reaction score
666
Habari wana jamvi?

Simba sports club imeanzisha utaratibu wa kutoa zawadi / tuzo ya gari kwa mfungaji bora wa msimu... (ITV habari za michezo jana)

My take: Kwa kuwa mchezo wa mpira ni team work, naona siyo sahihi kumpa mfungaji bora peke yake wakati kazi imefanywa na wote kila mmoja kwa nafasi yake, mfungaji amemalizia tu!

Hii huenda ikasababisha kupungua morali ya watoa pasi za mwisho kabla ya goli au (na) kuleta uchoyo wa pasi kuelekea kufunga goli.

Bora zawadi ya mfungaji bora ingekuwa SIFA na cheti, ngao, au medali isiyo na thamani kuuubwa ili zawadi / tuzo kubwa kusudiwa igawanywe kwa timu yote na si vibaya mfungaji bora akizidi wenzake kidoogo KULIKO kumpa mchezaji mmoja gari peke yake.

Nini maoni yako?
 
Wameshindwa kummalizia kessy makubaliano ya mkataba wake wataweza kununua gari kwa ajili ya mchezaji bora?!!
Uwongoooooooooo....
 
Vizuri vyote viko Yanga kwingine hata ! Huu unaitwa Unazi. Yanga mmefanya jambo gani Zurich hadi mjisifie hivyo?
 
Tujadili kwa upana wake bila kuzingatia Usimba au Uyanga.

Twende mbali zaidi kuhusu mambo yote ya 'team work' halafu zawadi KUBWA kupewa mtu mmoja. Je ni Sahihi?
 
Goalkeeper na Backs wote naona hawana chao
 
Walipe kwanza madeni Ya kusajili wachezaji!!! Waache siasa za kipuuzi
 
Baada ya kumaliza malengo yao ya mwaka (kuifunga Yanga) sasa wanafanya ya ziada tu, hapo ndipo akili na uwezo wa viongozi wa MBUMBUMBU F.C zilipoishia
 
Back
Top Bottom