Zawadi ya Wizkid yampa Alikiba umaarufu Nigeria

Zawadi ya Wizkid yampa Alikiba umaarufu Nigeria

Supervision

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
265
Reaction score
203
Habarini,kama habari inavyojieleza hapo juu,ndivyo ulivyokuwa huko Nigeria.

Mara tu baada ya EMA kueleza kinagaubaga,vyombo vya habari vya burudani nchini Nigeria vimemwelezea Alikiba kama msanii aliyepaswa kubeba tuzo ambayo Wizkid amechukua.

Kitu kilichoibua hoja zaidi ni baadhi ya mashabiki wa East Africa kuja juu na kudai kuwa msanii wao yuko vizuri kuliko Wizkid kitu ambacho kiliandikwa pia na vyombo vya habari ikiwemo magazeti,blag na redio.
Baadhi ya watu walionekana kushangaa lakini huku wengine walidai ni msanii aliyeko chini ya Son.

Post ya Alikiba iliyoeleza uungwana wake kuhusu wanao mtukana Wizkid imeandikwa pia katika vyombo vya habari pia TV mbalimbali zimetoa habari hii.
Hapo karibuni kuna mitandao iliyoeleza uwepo wa msuguano baina ya Wizkid na Alikiba juu ya nani atangulie stejini na chombo hicho kimeeza kuwa hiyo ilipelekea kuchelewesha show lakini haikuwa proved kama ndivyo.
 
duuuh mi sijaelewa naomba kwa alielewa anifahamishe ana maana gani juu hapo??
 
Ivi umeeona ulichokiandika? wewe huku siyo instagram au facebook umesikia yaaan unaleta ujinga wako hapa hebu rudi kwenye mitandao yenu kule.ndo kuna wenzio wenye uandishi wako
 
Maneno yako nikilisoma neno moja moja naelewa, ila sasa nikiunganisha yote kwa pamoja ndio naona hayaleti maana .
Kuna shida kwenye uandishi wako
 
Baada ya Alikiba kupewa tuzo vyombo mbalimbali vya habari nchini Nigeria vimemwadika Alikiba kama ndiye aliyestahili kupewa tuzo.
Nimeona magazeti mbalimbali,blog,na TV za Nigeria zikimtangaza huku baadhi yao wakionekana kumfahamu na wengine kutomfahamu.
Alianza kuwa gumzo mara baada ya kutokea sintofahamu Kenya ile ambayo ilidaiwa walikuwa wakishindana nani apande habari hii imeandikwa na chombo kimoja cha habari ikisema"Wizkid amepigana akashindwa kwa Alikiba"
Inaweza ikawa moja ya habari njema kwake ama kwa watu wake...niliona nishare baada ya kuona sana habari zake Nigeria
 
Huku mkiendelea kumlazimishia awe juu zaid,mwenzake anakaribia kuzindua perfurme yenye brand yake.Kiba ndo kwanza yupo dunia ya kuuza tshirt na kapero
 
daah ebana eeh we ndo jamaa wa jana umerud tena na post yako ya kipumbavu??hv hawa moods hawaoni huu ujinga???habar yako peleka jukwaa jengine maana nyie mnaujingakwel mnataraj mumshushe mmoja lii aje mwengine kwa upumbv wenu hamtafanikiwa.
 
Kiba yuko juu sana ila mashabiki wa fulani ndio wanajitahidi sana kumshusha, wao hawaoni mwingine wa kukosoa isipokuwa KIBA utafikiri tasnia ya bongo fleva ina watu wawili tu., kiba na mondi?! acheni kulazimisha bifu ambazo wasanii wenyewe hawazihitaji.
 
King Kiba....Wao wanazindua perfume sisi tunabeba Tuzo
 
Kwakweli huna kipaji cha kuandika na kueleweka. Hahahah maana nilidhani sijaelewa pekee
 
nonsense,yani kichwa na yaliyomo ndan ni hakuna uhusiano.kuwa makin GT.
 
Habarini,kama habari inavyojieleza hapo juu,ndivyo ulivyokuwa huko Nigeria.

Mara tu baada ya EMA kueleza kinagaubaga,vyombo vya habari vya burudani nchini Nigeria vimemwelezea Alikiba kama msanii aliyepaswa kubeba tuzo ambayo Wizkid amechukua.

Kitu kilichoibua hoja zaidi ni baadhi ya mashabiki wa East Africa kuja juu na kudai kuwa msanii wao yuko vizuri kuliko Wizkid kitu ambacho kiliandikwa pia na vyombo vya habari ikiwemo magazeti,blag na redio.
Baadhi ya watu walionekana kushangaa lakini huku wengine walidai ni msanii aliyeko chini ya Son.
Post ya Alikiba iliyoeleza uungwana wake kuhusu wanao mtukana Wizkid imeandikwa pia katika vyombo vya habari pia TV mbalimbali zimetoa habari hii.
Hapo karibuni kuna mitandao iliyoeleza uwepo wa msuguano baina ya Wizkid na Alikiba juu ya nani atangulie stejini na chombo hicho kimeeza kuwa hiyo ilipelekea kuchelewesha show lakini haikuwa proved kama ndivyo.
Mkuu kumshindanisha Wizkid na Alikiba ni sawa na kukutanisha mbingu na ardhi, kamwe haitatokea[emoji39][emoji39]
Cha mbolea endeeleni kumshindanisha na Domo japo pia kuna utofauti mkubwa sana.
I stand to be corrected
 
Back
Top Bottom