Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Zaytun Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha; Serikali ina mpango gani wa kuunga mkono juhudi za Wananchi kwenye Umaliziaji ujenzi wa Zahanati!
"Wananchi wa Kitongoji cha El'gong'we Wilayani Longido wanatembea zaidi ya Kilomita 35 kutafuta huduma za afya. Je, ni lini Serikali itaunga Mkono juhudi za Wananchi katika kumalizia Zahanati?" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha
"Nitumie nafasi hii kumkumbusha na kumsisitiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido kuanza kutenga fedha kwa awamu kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ili kuunga mkono juhudi za Wananchi katika ukamilishaji wa Zahanati na kama mapato ya ndani hayatatosheleza Mkurugenzi alete taarifa Ofisi ya Rais TAMISEMI ili Serikali iweze kuunga mkono Umaliziaji wa Zahanati" - Mhe. Dkt. Festo Dugange, Naibu Waziri TAMISEMI