Nadhani hapa tunagombea fito huku wenye ngoma wanatuangalia....
Suala la manji kufadhili si hoja hapa. ina maana imekuwa dhambi kwa yeye kuwafadhili hawa wajasiriamali?
Manji hapaswi kulipa na mengi hapaswi kushikilia haki za hawa wasanii. kwanza ikumbukwe Mengi amekimbilia kushtaki cosota na kupewa umiliki wakati yeye ni kiongozi wa MOAT ambao kwa sauti moja wanapinga kulipa mirabaha kwa kazi za wasanii, na kwa taarifa yenu ni kwamba cosota walipofika ITV walitolewa nduki na wakurugenzi.... Angalieni namna ambavyo IPP media inavyowahadaa wananchi kwa kuweka alama ya copyright ktk soaps za kiswahili zinazorushwa ktk televisheni zake. Huu ni uhuni na kuutetea lazima uwe na wazimu kichwani au sanasana uwe jasiri wa kiharamia.
Kuwakataza akina masanja kuendeleza game lao nje ya IPP media ni sawa na kumwambia kaseja kuwa asitumie style na mbinu zake za kudaka alizotumia simba awapo yanga... Ni sawa na kumwambia Ali choki asitumie jina na sauti yake aliyokuwa anatumia twanga pepeta awapo ktk bendi yake mpya ya t-rispekti. Kwa taarifa ni kwamba sheria zooote zaweza kuwa nyepesi kuadopted na wanasheria wengi, ila kwa ushahidi nilionao hasa wa kesi mahakamani wanasheria wengi wanapigwa bao kirahisi ktk sheria ya hakimiliki, you'll have to at least understands arts ukitaka kuitetea. tunaposema kuwa tunaifahamu sana sanaa kwa kuwa tunaiangalia jukwaani (production) siyo excuse ya kusema kuwa waifahamu sana,
Kwa hili Mengi amechemsha na COSOTA wanapaswa kuirevise hii kesi kama walivyofanya kwa ile ya Sister P ambaye alikwiba lyrics za mtu na kuwahi kuzijasili na kuzitumia akidhani dawa ni kuwahi lakini haki ikatolewa kwa uhalisia wa production proccess ili kumpata mmiliki. Inawezekana EATV walikwenda na hadithi nzuuuri yenye vivutio kisha jamaa wa Cosota wakaingia king, ila naamini sheria ilivyo ni kwamba endapo wakigundua wamedanganywa kasheshe lake si dogo. Kila kesi ina apeal yake.
Think think think think think before you bask