Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

unajua til today sijui wats the secret kubwa behind the bifu la hawa mafahali wawili MAnji na Mengi......as kama tuonavyo sasa nyasi ndio zaumia wakigombana majamaa hawa wawili....

Mtaalam, hawa jamaa wanatunishiana misuli na sisi tunacheza yenu!!!!!!! Tuachane na bifu lao halina faida halafu uone kama wataendelea, its just a marketing tool for their businesses and personality. tukiwadharau wataacha!!! Lets talk about these Naives artistes of our poor country
 
Asante Bro,
lakini Jitahidi kuangalia pande zote, pia usimpendelee mtu kwa vile ana asili ya Kiasia.


...No way Bro,

Reginald Mengi; namheshimu sana huyu mzee, tangu nimeanza kumfahamu miaka hiyo pale Coopers and Lybrand, ghorofa ya nane -IPS building.

Mbali na hilo, ni rafiki wa karibu tu wa familia, sikusudii kabisa kumtupia madongo yeye, ndio maana hata sakata la Mengi, na kashfa zake nyingine sitii neno! Namheshimu sana. Tatizo ninaloliongelea hapa ni EATV vs Ze Comedy! Binafsi 'nahisi' kuna 'wanoko' fulani wanajifanya kuwawekea roho mbaya hawa vijana, kwa maslahi yao binafsi! Sina uhakika na hilo, usijenihukumu nalo buree...ila mwenendo wa hili unaashiria hilo!

Mzee Mengi mwenyewe naamini 100% hana chembe ya roho mbaya kwa vijana hawa wanaotaka kujiwezesha, sababu RM mwenyewe ametokea mbali, na kwa jinsi mwenyewe alivyo na roho ya imani, naamini hao wanaolikweza hili, sana sana wanampa 'mtihani' tu mzee wa watu.

Yussuf Manji simjui! sana sana huwa naskia anaifadhili yanga, zaidi ya hapo hata sijui ana deal gani za biashara bongo!..atleast ungesema namtetea Azim Dewji kweli, tena sababu tu enzi hizo nilikuwa nashabikia Simba kikweli kweli!.

Zaidi ya hapo no more comment kuh; 'wenye asili ya kiasia', ...i have the right to remain silent, as anything i say may be used against me in the court of law!
 
kwani na makundi mengine kama wakina richie richie enzi hizo walivyotoka itv na kwenda tvt enzi hizo kwa maigizo mengine mbona waliendelea na majina yao haya haya ya uigizaji?!!
 
kwani na makundi mengine kama wakina richie richie enzi hizo walivyotoka itv na kwenda tvt enzi hizo kwa maigizo mengine mbona waliendelea na majina yao haya haya ya uigizaji?!!

Walikuwa hawafadhiliwi na "FISADI YUSUF MANJI"
 
Nadhani hapa tunagombea fito huku wenye ngoma wanatuangalia....
Suala la manji kufadhili si hoja hapa. ina maana imekuwa dhambi kwa yeye kuwafadhili hawa wajasiriamali?

Manji hapaswi kulipa na mengi hapaswi kushikilia haki za hawa wasanii. kwanza ikumbukwe Mengi amekimbilia kushtaki cosota na kupewa umiliki wakati yeye ni kiongozi wa MOAT ambao kwa sauti moja wanapinga kulipa mirabaha kwa kazi za wasanii, na kwa taarifa yenu ni kwamba cosota walipofika ITV walitolewa nduki na wakurugenzi.... Angalieni namna ambavyo IPP media inavyowahadaa wananchi kwa kuweka alama ya copyright ktk soaps za kiswahili zinazorushwa ktk televisheni zake. Huu ni uhuni na kuutetea lazima uwe na wazimu kichwani au sanasana uwe jasiri wa kiharamia.

Kuwakataza akina masanja kuendeleza game lao nje ya IPP media ni sawa na kumwambia kaseja kuwa asitumie style na mbinu zake za kudaka alizotumia simba awapo yanga... Ni sawa na kumwambia Ali choki asitumie jina na sauti yake aliyokuwa anatumia twanga pepeta awapo ktk bendi yake mpya ya t-rispekti. Kwa taarifa ni kwamba sheria zooote zaweza kuwa nyepesi kuadopted na wanasheria wengi, ila kwa ushahidi nilionao hasa wa kesi mahakamani wanasheria wengi wanapigwa bao kirahisi ktk sheria ya hakimiliki, you'll have to at least understands arts ukitaka kuitetea. tunaposema kuwa tunaifahamu sana sanaa kwa kuwa tunaiangalia jukwaani (production) siyo excuse ya kusema kuwa waifahamu sana,

Kwa hili Mengi amechemsha na COSOTA wanapaswa kuirevise hii kesi kama walivyofanya kwa ile ya Sister P ambaye alikwiba lyrics za mtu na kuwahi kuzijasili na kuzitumia akidhani dawa ni kuwahi lakini haki ikatolewa kwa uhalisia wa production proccess ili kumpata mmiliki. Inawezekana EATV walikwenda na hadithi nzuuuri yenye vivutio kisha jamaa wa Cosota wakaingia king, ila naamini sheria ilivyo ni kwamba endapo wakigundua wamedanganywa kasheshe lake si dogo. Kila kesi ina apeal yake.

Think think think think think before you bask
 
Sawa Msanii, tusubiri tuone kama hakuna Sheria ya Hati Miliki Tanzania.
 
Kwa kweli mimi binafsi nilianza kupata shaka na ishu ya hawa jamaa baada ya kusikia wanaondoka EATV.nahisi kuna mambo mawili yanajionesha hapa.maslahi ya kibiashara na politiki.

Jamaa walivuma sana kule EATV na kibiashara kituo kilipata matangazo mengi.Nao ze comedy wamejua kuwa wana jina hivyo wanatizama maslahi zaidi ambayo TBC1 wamediriki kuyatoa kuvutia ngoma kwao.

Si wajua kuna ishu za kibiznes na kipolitiki zinazoendelea kuvuma kichinichini kati ya mzee meng... na manj...? mimi naona kuna kamchezo ze comedy wameingizwa bila kujijua.

Natabiri japo kwa machungu kufififa ama kupotea kwa umarufu wao.
 
Hawa hawakumbuki aliyewafikisha hapo
Hawana hata aibu ya kufadhiliwa na Adui wa Mengi (Fisadi Manji)
Waswahili tunasemaga hivi: - Usiache Mbachao kwa Msaala Upitao.
Pia Mtaka yote kwa Pupa hukosa yote.

Vijana ninawashauri mrudi EATV, muombe Msamaha ili muendeleze Libeneke kule.

Ninawatakieni kila la heri.
 
Hawa hawakumbuki aliyewafikisha hapo
Hawana hata aibu ya kufadhiliwa na Adui wa Mengi (Fisadi Manji)
Waswahili tunasemaga hivi: - Usiache Mbachao kwa Msaala Upitao.
Pia Mtaka yote kwa Pupa hukosa yote.

Vijana ninawashauri mrudi EATV, muombe Msamaha ili muendeleze Libeneke kule.

Ninawatakieni kila la heri.

....shekhe unatetea????
biashara haina adui zaidi ya hasara
 
Waungwana wa JF,
Wapo wapi Original Comedy (Ze comedy)
Siku hizi vipindi vyao vinaboa sana pale TBC-1

Walikuwa wanawaita wenzao mdebwedo, sasa ni zamu yao.

Ze Comedy au Original comedy in MDEBWEDO.
 
Ebwana wakubwa hivi haya maneno ya ze comedy ni ya kweli au ndiyo jamaa wanajitafutia umaarufu kunuka? Eti wadau nyi mnalionaje hili? Ikiendelea hivi ze comedy wata eksizist kweli?
 
aah sheikh mbona maneno yako yanapandiana bwana?? mie sipo kwenye mood ya mijadala mirefu leo..........ma-friday haya na bootycall, sitaki nianze kuulizwa mbona upo serious namna hiyo!!???

Msipokuwa kwenye mood si msichangie jamani? mbona kwenye EPA mnshabikia lakini pesa za WALEMAVU mnawalaumu ze comedy? BIAS
 
Back
Top Bottom