Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM) Kapten John Komba, amelipiga kundi la Ze Cimedy, kuigiza sauti yake kwenye vipindi vyao vya ucheshi ambacho hurushwa hewani kupitia Luninga ya EATV.
Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa kundi la Maonesho la TOT, alisema ameshawasiliana na Ze Comedy na kulitaka kuacha mara moja kuiga sauti yake, lkn ameshagaa kuona bado wanaendelea.
"hii ni sauti yangu ambayo nimepewa na Mungu ili niitumie mimi mwenyewe siyo kwa ajili ya kuigizwa na watu wengine" Kepten Komba aliliambia gazeti hili(Ijumaa) kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mbunge huyu alisema ingawa kundi hilo limekuwa likiigiza sauti za watu mbalimbali, lakini kila mtu anaweza kupokea kulingana na mtazamo wake, hivyo alidai kwamba analichukulia kama dharau juu yake.
Alimtaja msanii wa Ze comedy, Mjuni sylvery 'Mpoki' kuwa ndiye humuiiga mara kwa mara ktk maonesho ya kikundi hicho. Vitendo ambavyo humdhalilisha yeye, familia yake na wananchi anaowaongoza.
Niliwahi kumpigia simu Mpoki nikamuonya, kwanza nilikuwa simjui, nilipoambiwa hiyo tabia yake ya kuiga sauti yangu, nilitafuta namba yake mpaka nikaipata lakini nashangaa yule kijana hataki kuacha.
"Hashangai mimi mbunge mzima kuhangaika kumtafuta mpaka nilivyompatana nikamuonya. Anachofanya ni kiburi ndio maana hataki kuacha. Hivi kwanini asitumie sauti yake ya kawaida kama kweli yeye ni msanii wa kweli? alihoji mh Kapt. Komba.
Alipoelezwa kwamba Ze Comedy huwa hawamuigizi kwa mabaya bali ni kwa lengo la kufikisha ujumbe, Komba alijibu " Kufikisha ujeube siyo lazima watumie sauti yangu, watumie sauti za watu wengine, ya kwangu sitaki kwa sabatu sipendi.
"Nimemkanya hajasikia, kwa hiyo wacha aendelee, lakini kuna siku ataona moto wangu kwa sababu makaidi hafaidi mpaka siku ya idd."